Rafiki wa kike wa mume wangu ananitesa

Rafiki wa kike wa mume wangu ananitesa

Pole sana dada kwa changamoto hiyo.
Nakushauri usiendelee kuhangaika kuvunja huo urafiki maana wa kuuvunja ilitakiwa awe mmeo baada ya kukuoa, ila inaonekana bado kwenye eneo hilo kichwa chake hakijakubali kuwa ameshahama kutoka daraja moja la maisha na kuingia daraja jingine.

Nakushauri ww tengeneza mazingira ya ndoa, nyumba na privacy yenu kuheshimiwa ongea na mumeo umwambie unachotaka na uchore mstari ambao mmeo na huyo binti hawatakiwi kuvuka mfano hiyo kupigiana simu hadi usiku mrefu mwambie hutaki, kuja nyumbani kwako wakati ww haupo piga marufuku kama wanataka kuonana waende bar but not in ur house tena in ur absence, nk nk nk.

Ukiona anaendelea kuzingua omba kikao cha familia akakutane na wanaume wenzake wamweke sawa.

NB: Acha kupekua pekua simu ya mmeo.
 
Na wewe unasema una Mume???Huyo ni rafiki yako ilaa ni mume wa huyo dada unaedhani ni rafiki yakee... Maana anamasikiliza yeye zaidi kuliko wewe..

NB:HAKUNA URAFIKI KATI YA MUME WA MTU NA MWANAMKE MWINGNE...HAUPOOO
 
Sawa mchepuko nitakuroga, hahaaaaa
Alikuwa Na urafiki kabla ata ajafunga ndoa Na wewe . Utamchagulia mpaka lini mumeo marafiki ... Lipiza Basi nayeye aumie si 50/50 .. mpe limbwata awe zuzu Na akiwa zuzu yeye Na kizazi chake watoto wenu watakuwa masikini mbwa milele amini ... Dai talaka Basi ...ko kama nimefunga ndoa Na ww nisiambatane Na rafiki zangu ... Kunywa sumu Basi ...jichome kisu Basi
 
Nimekuwa mfuatiliaji wa mikasa ya watu humu leo na mimi nikaona nilete jambo langu linalonitesa kwa muda mrefu ili nijue nini cha kufanya. Mimi ni binti niko ndani ya ndoa, wakati naolewa mume wangu alikua na rafiki yake wa kike ambaye wenyewe wanadai urafiki wao ni wa kawaida tu kwani wanajuana muda mrefu. sasa tatizo huu urafiki wao umekuwa kero kwangu yani ni ule urafiki uliopitiliza kiasi kwamba kilasiku nikiangalia kwenye cm ya Mr lazima nikute wamewasiliana hata mara 50 text ndo usiseme. Kila sehemu wanaenda wote na huyo binti yani kama kumbikumbi mimi niko chuo wakati mwingine nikiwa chuo nikirudi hom namkuta huyo binti na Mr sebuleni inamaana ana courage ya kuja kwangu mimi nikiwa sipo, mara nyingine weekend tuko nyumbani na Mr, binti anampigia Mr cm njoo nyumbani kwangu ule nimepika, mume naye kilasiku lazima aripoti nyumbani kwa binti, mara binti aje nyumbani kumpitia Mr amsindikize sehemu, wakati mwingine tumelala weekend asubuh saa 1 binti kapiga cm kwa mr unafanya nini amka twende kwa fulani {mshikaji wao} yani full tafrani hana adabu kabisa ila nilichogundua ni kua mr nae ndo anampa ujeuri coz kuna kipindi niligombana sana na huyu binti kuhusu tabia zake huwezi amini alinijibu kuwa mimi siwezi kuwatenganisha kamwe nikitaka nimwambie mume wangu ndio ampige yeye marufuku kua na ukaribu nae ila sio mimi. Jamani cm wanapigiana mpaka saa 6 usiku. wenyew wanadai wao ni marafiki wa kawaida tu na hakuna kinachoendelea. nimejaribu kuuvunja urafiki huo unaoniumiza nimeshindwa mimi wenyewe hawana hata habari. Je kuna urafiki wa aina hii kweli kati ya mwanamke na mwanaume tena mume wa mtu? kwanini kusiwe na mipaka jamani..Huyo mwanamke ni mjeuri hatari ukimwambia anakujibu kwa dharau sana, mume naye ndo kwanza hana habari nisaidieni jamani nifanyaje?
Nawe tafuta rafiki wa kiume ngoma iwe droo
Maana hamna namna
 
Dada

Huna rafiki wa kiume?????

Yaani anayoyafanya mumeo na rafiki yake wewe umfanyie na nyongeza

Wakati mwingine mpe mtu taste of his own medicine

Ukishindwa sepa mwbie aendelee na rafiki yake wasikuzeeshe
 
Kwa uzoefu mdogo nilionao kwenye ndoa,wewe hapo umeshapinduliwa na kinachofuata hapo ni wewe kuondoka lakini kabla ya wewe kufika huko jaribu kuzungumza na mmeo nadhani utapata pa kuanzia.
 
Huyo mwanaume si sahihi kwako, m'ume yeyote asiejali na kuweka hisia zako mbele huyo si wako.. Hivi alishajiweka kwenye viatu vyako hata kidogo kama angeweza?! Wew ndio first priority yake lkn anampomtanguliza huyo rafiki alafu ndio wew, basi wew ndio ulieingilia mahusiano ya watu.. Peleka hilo suala kwa mshenga aongee na mumeo labda hajui wajibu wake kama mume na hajui kuwa ukishaoa masuala ya usela na kuishi kama bachelor kunakufa kifo kitakatifu. Achague moja Ndoa au Ubachelor?! Kama anampenda sana huyo rafiki yake si angemuoa ili muda wote wawe pamoja kuliko anavyohangaika sasa
 
Pole sana, huyo mume bado ana akili za kitoto sana. Sidhani kama anajua sababu za yeye kuingia kwenye ndoa, huenda alilazimishwa au hakukubali kama mke, ameamua kukuletea visa.
 
Pole! Jitahidi kuwa karibu na Huyo Dada,lkn nimegundua ww inawezekana unajifanya much know! Haumpi mmeo time ya kuwa na ww mpaka anaona bora kutafuta/kiendeleza company na watu wengine hata baada ya ndoa! Nadhani ww una udhaifu somewhere! Sorry kama nimetumia maneno makali!
 
Nimekuwa mfuatiliaji wa mikasa ya watu humu leo na mimi nikaona nilete jambo langu linalonitesa kwa muda mrefu ili nijue nini cha kufanya. Mimi ni binti niko ndani ya ndoa, wakati naolewa mume wangu alikua na rafiki yake wa kike ambaye wenyewe wanadai urafiki wao ni wa kawaida tu kwani wanajuana muda mrefu. sasa tatizo huu urafiki wao umekuwa kero kwangu yani ni ule urafiki uliopitiliza kiasi kwamba kilasiku nikiangalia kwenye cm ya Mr lazima nikute wamewasiliana hata mara 50 text ndo usiseme. Kila sehemu wanaenda wote na huyo binti yani kama kumbikumbi mimi niko chuo wakati mwingine nikiwa chuo nikirudi hom namkuta huyo binti na Mr sebuleni inamaana ana courage ya kuja kwangu mimi nikiwa sipo, mara nyingine weekend tuko nyumbani na Mr, binti anampigia Mr cm njoo nyumbani kwangu ule nimepika, mume naye kilasiku lazima aripoti nyumbani kwa binti, mara binti aje nyumbani kumpitia Mr amsindikize sehemu, wakati mwingine tumelala weekend asubuh saa 1 binti kapiga cm kwa mr unafanya nini amka twende kwa fulani {mshikaji wao} yani full tafrani hana adabu kabisa ila nilichogundua ni kua mr nae ndo anampa ujeuri coz kuna kipindi niligombana sana na huyu binti kuhusu tabia zake huwezi amini alinijibu kuwa mimi siwezi kuwatenganisha kamwe nikitaka nimwambie mume wangu ndio ampige yeye marufuku kua na ukaribu nae ila sio mimi. Jamani cm wanapigiana mpaka saa 6 usiku. wenyew wanadai wao ni marafiki wa kawaida tu na hakuna kinachoendelea. nimejaribu kuuvunja urafiki huo unaoniumiza nimeshindwa mimi wenyewe hawana hata habari. Je kuna urafiki wa aina hii kweli kati ya mwanamke na mwanaume tena mume wa mtu? kwanini kusiwe na mipaka jamani..Huyo mwanamke ni mjeuri hatari ukimwambia anakujibu kwa dharau sana, mume naye ndo kwanza hana habari nisaidieni jamani nifanyaje?
Njoo tuanze urafiki. Uwe unakuja ghetto kupika, kufua, kufanya usafi n.k ili tuwarushe roho.
 
Sijui wewe ni mwanamke wa Karine gani.
Mpaka hapo hujui nini kinaendelea.
Yaani angekuwa Ndo mume wangu mimi. Angechagua moja. Abaki na mimi au huyo rafiki yake wa kike.
Sasa hapo umeolewa au wewe ni mfanya kazi wake wa ndani??
 
Nimekuwa mfuatiliaji wa mikasa ya watu humu leo na mimi nikaona nilete jambo langu linalonitesa kwa muda mrefu ili nijue nini cha kufanya. Mimi ni binti niko ndani ya ndoa, wakati naolewa mume wangu alikua na rafiki yake wa kike ambaye wenyewe wanadai urafiki wao ni wa kawaida tu kwani wanajuana muda mrefu. sasa tatizo huu urafiki wao umekuwa kero kwangu yani ni ule urafiki uliopitiliza kiasi kwamba kilasiku nikiangalia kwenye cm ya Mr lazima nikute wamewasiliana hata mara 50 text ndo usiseme. Kila sehemu wanaenda wote na huyo binti yani kama kumbikumbi mimi niko chuo wakati mwingine nikiwa chuo nikirudi hom namkuta huyo binti na Mr sebuleni inamaana ana courage ya kuja kwangu mimi nikiwa sipo, mara nyingine weekend tuko nyumbani na Mr, binti anampigia Mr cm njoo nyumbani kwangu ule nimepika, mume naye kilasiku lazima aripoti nyumbani kwa binti, mara binti aje nyumbani kumpitia Mr amsindikize sehemu, wakati mwingine tumelala weekend asubuh saa 1 binti kapiga cm kwa mr unafanya nini amka twende kwa fulani {mshikaji wao} yani full tafrani hana adabu kabisa ila nilichogundua ni kua mr nae ndo anampa ujeuri coz kuna kipindi niligombana sana na huyu binti kuhusu tabia zake huwezi amini alinijibu kuwa mimi siwezi kuwatenganisha kamwe nikitaka nimwambie mume wangu ndio ampige yeye marufuku kua na ukaribu nae ila sio mimi. Jamani cm wanapigiana mpaka saa 6 usiku. wenyew wanadai wao ni marafiki wa kawaida tu na hakuna kinachoendelea. nimejaribu kuuvunja urafiki huo unaoniumiza nimeshindwa mimi wenyewe hawana hata habari. Je kuna urafiki wa aina hii kweli kati ya mwanamke na mwanaume tena mume wa mtu? kwanini kusiwe na mipaka jamani..Huyo mwanamke ni mjeuri hatari ukimwambia anakujibu kwa dharau sana, mume naye ndo kwanza hana habari nisaidieni jamani nifanyaje?
huyo ni mke mwenzio.. hiyo haina ubishi!
 
Nawewe tafuta rafiki chuoni kwenu akipitiwa na rafiki yake basi akirudi akukute nawewe na rafiki yako wa kiume, ukiona haumii uanze kumsifia kabisa how he is kind to you etc au hata binamu kama hutaki madhara makubwa wanafaa sana
 
Back
Top Bottom