Kibona Dickson
Member
- Feb 13, 2011
- 37
- 14
Chadema hawawezi kuwatengezea ilani watu wa Uganda,sio rahisi kama unavyofikiria wewe. Urafiki wa kisiasa hauna maana ya kuingilia mambo ya ndani ya chama au nchi fulani.Lakini kitu kimoja dhahiri,chama cha siasa kinaweza kuazima au kuiba sera fulani kutoka kwenye chama kingine,kama akina Kizza Besegye waliazima sera kutoka CDM,wakiamini zitawafaa waganga haina maana kuwa hii itageuka kuwa pigo kwa CDM.Ni pigo kwa Waganda,kwa kuwa wamekosa fursa ya kupata maendeleo kutoka na sera mbadala.
Kumbuka,hapa Tanzania,sera za CDM,katika ilani ya uchaguzi wa mwaka jana hata kama hatukushinda urais na kupata Wabunge wengi kuliko CCM,ni sera ambazo zinakubalika kwa kiasi kikubwa na watanzania walio wengi.Kwa kutumia sera hizo,CDM imepata wabunge wengi zaidi kutoka wabunge kumi na mmoja katika uchaguzi wa mwaka 2005 hadi wabunge takribani hamsini katika uchaguzi wa mwaka jana ni mafanikio makubwa.
Bado sera na ilani ya CDM ina inflluence mpaka leo.CCM katika ilani hawakuzungumzia kuhusu katiba,wala JK ktk hotuba yake bungeni hakugusia lolote kuhusu katiba. Lakini CDM katika ilani yao waliweka kipaumbele swala la katiba mpya.Leo hii watanzania wote wanazungumzia katiba mpya akiwepo JK.
Nikukumbushe kitu kimoja cha msingi,urafiki wa vyama vya siasa unatokana na itikadi na falsafa na mahusiano ya kisiasa tu,swala la utaifa na uzalendo linabaki palepale.Huwezi kusema kwa kuwa akina Bhesigye wameshindwa huko uganda,basi CDM wanaumia. Kinachowaumiza CDM,ni kutokuwepo kwa katiba mpya hapa Tanzania Chini ya ccm,kukithiri kwa ufisadi na mafisadi ndan ya serikali ya CCM,Uwizi wa wa kimafia kupitia makampuni ya Dowanisiii,Uchakachuaji wa matokeo ya uchaguz.