Rafiki angu ananiroga

Asante. Niko mbali nae sana, analalamika sana namtenga
 
Kwahiyo baada ya kukupeleka kwa waganga na wewe umeamua kuwa member.
Vunja urafiki naye na achana na mambo ya waganga kuna ndugu yangu alikuwa anaamini uganga wakala pesa yake hata tatizo la uzembe wake anakimbilia huko.
Akaambiwa bibi yake ndiye anamroga baada ya muda akaambiwa sijui mkewe mara sijui nani alikuja kushtuka baada ya kuambiwa mama yake anamroga.
Hapo ndipo akili ilimkaa ila alikuwa ashaliwa pesa nyingu na miaka mingi akiamini hawa watu.
Ni wachonganishi sana kaa nao mbali
 
Kwa akili hizi Tanzania tuna safari ndefu ya kusonga katika nchi ya kusadikia ya viwanda.

Kapimwe akili mkuu huenda una matatizo ya kisaikolojia.
karogwa sasa akienda hosp si ataambiwa hana chochote?
 
Unajua siamini kama kweli hii thread naisoma humu jf!

Dah!Mungu alikustiri mkuu lakini umejiumbua.
 
sasa kwanini na wewe hujamloga mpaka sasa?
 
Nashukuru kwa ushauri, sitaki tena waganga. Kampani yake nayo siitaki.

Anapiga sim sana mpaka missed call 12. Sipokei wala SMS simjibu.
Anabadilisha mpaka namba nimeshtuka sipokei namba ngeni.

Amezoea ukitonga wake anakufa njaa sasa. Jamaa nilikuwa namsaidia sana, hela ya kula nilikuwa nampa, funguo ya gari nampa. Kuna siku nilimlipia mpaka guest house akaenda kupumzika na rafiki ake.

Sasa anaisoma namba
 
Hayo ya kugombana hayana maana mwambie huyo babu akupe dawa ujitibu ili maisha yasonge
 
Hiyo ni option nzuri mkuu
 
Kumbe Hizi Imani zipo za kwenda Kwa mababu Kupiga ramli. Funguka vizuri ulitozwa shilling ngapi.
 
huyo mganga akukumbia umpelekee debe la mchele na mbuzi beberu..njoo kwa yesu kijana huku hakuna ghalama
 
Kuna ck nilinunua fungu la muhogo sokoni (market) nikaenda nalo mpk kw mganga nikamwambia nimepewa na ndugu yng km zawad ila simuamin hvy aungalie vp unafaa kuliwa nahaujafanyiwa ubaya wowote.
Hapo alianza kuongea uongo eti mara anataka kukutekeza ww na familia yako na mngn mengi tu huku rohoni nacheka mpk leo hao wtu siwaamin ng'o
 
Umejiloga mwenyewe mkuu Acha mganga akule pesa.. Acha ushirikina maisha nI kupanda n kushuka achana na fikra potofu .. mrudieni Mungu
 
Sasa wewe unao uchumi gani wa maana kama mpaka chakula anachokula rafiki yako home unakichukulia kama fadhila?

Hiyo ni indicator tosha ya ufukara uliotukuka wa roho na mwili Mungu akusaidie sana.
Uchumi wangu unaujua? Katika yote hayo umeona chakula tu?
Nampa pesa, najaza gari petrol nampa funguo yoote hukuyaona??

Unaonekana mroho sana wewe

Kwangu chakula sio kitu wala magari pesa kwangu vitu vya kawaida sana.

Ata wewe ukitaka chakula njoo ule
 
Peleka ulofa huko TASAF wamekusahau unakuja kulialia hapa JF.
 
Hizo ndizo ramli chonganishi ambazo serikali inajitahidi kuzipiga vita. Acha kuwaamini saana hao waganga wako tafadhali kuna siku watakuambia mkeo au mama yako ndio wanakuroga sijui utafanyaje!?!?!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…