Radio Programming (Mpango Vipindi) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Radio Programming (Mpango Vipindi)

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Radio Producer, Sep 20, 2012.

 1. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2012
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Wadau,

  Leo nataka kuzungumzia kidogo suala la Programming katika radio mbalimbali.

  Nimegundua mambo mawili muhimu katika radio zetu nyingi kwasasa.

  1. Radio nyingi zinaiga radio zingine. Kwakweli hiki kitu kimekithiri sana huwa nikipita kila sehemu na kusikiliza radio nakutana na vituko vingi sana. unakuta radio ya hapo mkoani inatangaza matangazo yake, ukisikiliza na hizi radio kubwa zinazoingia kutoka mikoa mingine kama RFA, Radio One n.k unashangaa kukuta kwamba hizi radio ndogo za mikoani zimeiga mwanzo mwisho kwenye radio hizi kubwa! Ni kweli unaweza kuipiku radio na kujipatia wasikilizaji wengi kwa mtindo huu?

  2. Radio nyingi hazina wataalamu kwenye programming department. Katika radio ni mara mia sehemu zingine zisiwe na watu wenye professional kubwa lakini katika kitengo cha programming acha utani kabisa, unatakiwa kuweka mtu mwenye akili, elimu, upeo binafsi na ubunifu mkubwa, vinginevyo kila siku radio yako itakuwa kama debe tu hakuna msikilizaji.

  Radio za Kidini.
  Hapa napo kwenye upande wa hizi radio kiukweli ndo kunavichekesho na vituko vikubwa sana siku hizi. Hizi radio ukizisikiliza unaweza kucheka hadi kuzimia kama unajua vizuri masuala ya media. Hizi radio nyingi zimeshindwa zikae wapi, zingine zinaigiza kufuata radio za kidunia, na zingine zimevutika kwenye masuala ya kisiasa, ukijumlisha na dini sasa ni sangulo na wala hazifai kwa kusikiliza. Si zote ila nyingi zimeathirika. Hata zile nzima zina conflict of interest, zingine zinafukuzia pesa tu na hakuna cha maana.

  Hizi radio za dini zinahitaji operation kubwa sana tena sana. Ninaimani haya yote yanahitaji kusaidiana tu na kuelimishana kidogokidogo mwisho tutafika. Sisi tunatoa huduma zetu kwenye radio kama hizi unaweza kupata maelekezo zaidi hapa: Radio Consult Company Limited

  Asanteni.
  Radio Producer
  Radio Consultant.
   
 2. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2012
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Radio za kidini zinahitajika kugundua kuwa zenywe zipo au zimeanzishwa kwa ajili ya nini hiki ndiyo kitu muhimu na pekee.
   
 3. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2012
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Tunaandaa mkakati unaozihusu radio za kidini.
   
Loading...