Radio free na matokeo ya olympic

ARV

JF-Expert Member
Sep 6, 2011
4,956
6,948
Leo asubuhi wamenikera kwenye kipindi chao cha michezo, eti wametangaza mechi kati ya Great Britain vs Korea iliyopigwa jana usiku eti hakukuwa na mshindi baada ya kuisha dakika 90 wakiwa drooo na ikaongezwa dakika 30 napo hawakufungana na katika penalt napo wakatoka droo, kwa hiyo wakatangaza eti mechi ikaahirishwa.

Ukweli
GB imetolewa na Korea kwa penalt 4-5, penalt ya tano ya GB iliyopigwa na Danny Sturridge iliokolewa na kipa wa Korea.

My take,
Hii ni Redio kubwa inayoheshimika katika ukanda huu wa nchi za maziwa makuu, wasiwe wavivu kufuatilia habari zilizo wazi kama hizo, hata kama usiku walishindwa kuangalia mechi live, wangefungua tu mitandao mbalimbali wangeona matokeo ya mwisho.
 
Back
Top Bottom