Radio Clouds Mtavunja Ndoa za Watu

Kuna mambo mawili yaliyonifanya nisiwe nasikiliza clouds. Hapana mambo matatu.

1. Kipindi cha nyuma, nilikuwa msikilizaji mzuri sana wa njia panda. Nakumbuka hiyo jumapili mtangazaji alikuwa ana mhoji au anasoma barua ya mdada (sikumbuki vizuri). Huyo mdada alikuwa anasema ameambukizwa HIV na jamaa ambaye ni mfanyakazi wa ubalozi (sikumbuki ni nchi gani).

Alivyoelezea ni kwamba walikuwa na mahusiano na huyo jamaa, lakini akamwambukiza huyo mdada HIV makusudi. Kuna mdada mwingine alipiga simu studio wakati kipindi kinaendelea kutokana na maelezo yaliyotolewa, akasema anamfahamu huyo jamaa aliyemwambukiza mdada na akamtaja jina na na ubalozi anaofanya kazi.

Wakati haya yote yanaendelea, moyoni nikasema kama jamaa wa ubalozi ana mke, basi itakuwa imekula kwake. Lakini wakati kipindi kinaendelea huyo jamaa anayesemekana ameambukiza HIV, akapiga simu na kukanusha hiyo taarifa. Akasema alishaenda kupima na ikaonekana hana HIV.

Hiyo issue japo siikumbuki vizuri, sijui iliishia wapi. Lakini nilisikitika sana kwa chombo cha habari kupokea tuhuma kumhusu mtu, halafu hawahoji upande wa pili kupata ukweli.

Vipindi vya live, vina masharti yake na inatakiwa kama mtangazaji uwe maakini sana.

2. Kuna kipindi kilikuwa kinarushwa na mtangazaji wa kike usiku. Yule mdada akawa anatoa chance ya msikilizaji kupiga simu, na kumkumbuka mpenzi wake wa zamani na kuulizia yuko wapi na jinsi gani anamiss.

Hii ndiyo niliona utoto kabisa. Nikajiuliza, mume au mke akisikia mwenzake anakumbukwa na lijamaa atajisikiaje? ''kwamba nimeyamiss mahaba yetu ya zamani''. Nikasema huu ni utoto.

3. Matangazo muda wote na hasa vipindi vya asubuhi.
 
Mimi nilidhani ungelalamika yule bidada anavyobumba bumba habari ambazo hana hata uhakika nazo...ameongea habari ya Jammeh, kwamba alipewa siku tisini na bunge na zimeshaisha ili hali ndio kwanza bunge walipitisha hilo azimio jana jumatano...nilimsikia nikabaki like 'wtf'

Yaani hawa Wanahabari sikuhizi usipojiongeza kufuatilia vyombo vingine wanakupoteza mazima.
 
Lakini jamani!!!ewe mume/mke kwanini mtu ukafanye uzinzi na mtu ambaye sio mumeo/mkeo?uliowa/olewa kwa sababu gani,why hukusubiri umalize michezo yako ya ujana(japo ni dhambi vile vile)ndo uowe kuliko unaingia ktk taasisi ungali na tamaa zako.tatizo watu tunaona ni haki kabisa kwa wanandoa kufanya ngono nje ya ndoa zao,mimi nasema acha awabumbulue waijue hiyo app ili wakakamatane ugoni wenye kuachana waachane ili hatimaye heshima kwa Mungu aliyeweka ndoa irudi na taasisi ya ndoa kwa ujumla.
 
Wewe ndo umeamplfy kikamilifu bola ungekaa kimya mie nlikua sijui ninejua kupitia wewe
 
Hii ni zaidi ya hatari wallahi.
 
Si msikilizaji wa radio. Ilitokea tu mara moja nikasema ngoja leo niweke radio ndo nikasikia hayo.
 
Na hili tangazo la kutumia 'kondom' mkuu si sahihi kwa wana ndoa.
Eti mtumiapo hiyo kila mtu mawazo yote yanakuwa katika kitendo hicho. Pamoja na kupata pesa hatufikirii kuwa si kila tangazo ni jema, mbona tunakuwa sawasawa na Yuda Eskarioti.
 
Sijaona kosa lao....
 
Kama mkeo hajiheshimu hata umfanye nini hawezi kuacha
hata umpe milioni ataziacha hapo ndani na atachepuka tu;
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…