Waongoza Kwa Kuvunja Ndoa za Watu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waongoza Kwa Kuvunja Ndoa za Watu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Feb 9, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kutokana na vishawishi vya kimapenzi kutokana na picha na meseji zinazoandikwa kwenye Facebook zimepelekea watu wengi wazisaliti ndoa zao na matokeo yake kumekuwepo na ongezeko kubwa la kuvunjika kwa ndoa chanzo kikubwa cha kikiwa ni Facebook.
  Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni kuhusiana na matumizi ya mtandao wa Facebook umeonyesha kuwa ndoa nyingi zimekuwa zikivunjika kutokana na wanandoa kuingiwa na vishawishi na baadae kuzisaliti ndoa zao kwa kuanza mahusiano ya kimapenzi na watu wanaokutana nao kwenye mtandao huo mkubwa duniani.

  Utafiti uliofanywa nchini Uingereza umeonyesha kuongezeka kwa kasi ya kuvunjika kwa ndoa kutokana na watu kufumaniwa wakiwa na mahusiano ya kimapenzi nje ya ndoa na watu wanaokutana nao kwenye Facebook.

  Mwanasheria mmoja wa masuala ya familia alidokeza kuwa katika kipindi cha miezi tisa iliyopita, alizisimamia kesi 30 za kuvunjika kwa ndoa na kesi zote zilihusisha mtandao wa Facebook kama chanzo cha kuvunjika kwa ndoa hizo.

  Mwanasheria mwengine alisema kuwa katika kila kesi tano walizozisimamia za madai ya talaka, kesi moja ilihusisha mtandao wa Facebook kama sababu kuu ya kuvunjika kwa ndoa.

  Emma Patel, mwanasheria wa kampuni ya Hart Scales & Hodges Solicitors, alisema kuwa tovuti ya Facebook imegeuka kuwa mtu wa kati wa kuzitenganisha ndoa za watu.

  “Facebook imekuwa ikilaumiwa kwa ongezeko la kuvunjika kwa ndoa na cha kustaajabisha katika kesi zote nilizozisimamia tangu mwezi mei mwaka jana zote zilihusisha tovuti ya Facebook kwa njia moja au nyingine”, alisema Emma.

  Miongoni mwa watu waliovunjwa mioyo yao kutokana na mtandao wa Facebook ni James Wrigley, 34 wa mjini London ambaye alisema: "Mpenzi wangu alinitosa baada ya kugundua kuwa nilikuwa nikiwatumia meseji kwenye Facebook wanawake niliokuwa nikifanya nao kazi”.

  “Alipata password yangu ya Facebook, alisoma meseji zangu zote na huo ndio ukawa mwisho wa uhusiano wetu wa miaka mine, sijahuzunika sana kwa sababu hatukuwa tumeoana”, aliongeza James.

  Mfano mwengine ni mama wa mtoto mmoja, Marianna Gini, 32, ambaye ndoa yake ya miaka sita ilivunjika baada ya kugundua kwa kupitia mtandao wa Facebook kuwa mumewe Robert, 34, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwengine nje ya ndoa.

  Mwanamke mwingine wa nchini humo aliamua kuvunja ndoa yake na mumewe baada ya kugundua mumewe alikuwa akimtumia ujumbe wa kimapenzi mwanamke mwingine ambaye hata hawakuwahi kukutana.

  Msemaji wa Facebook alipoulizwa kuhusiana na lawama wanazotupiwa Facebook za kuvunja ndoa za watu alijibu kwa kusema “Ni sawa na kuilamu simu yako ya mkononi au email yako”.

  “Kwani kuingia kwenye Facebook mtu hulazimishwa kufanywa kitu asichokipenda? , jibu lingekuwa ni Hapana.”, alimalizia kusema msemaji huyo wa Facebook.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Ahhhh same old story about facebook
   
 3. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  deactivate ya selves....
   
 4. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  sio facebook mbaya bali wa2miaji ndio wabaya
   
 5. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mmmhhh :coffee:
   
 6. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #6
  Feb 9, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mbona hata hapa JF imetokea? sasa mbaya ni nani JF au watu waliohusika na skendo hiyo? watu wengine wana propaganda za ovyo kweli.
   
 7. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #7
  Feb 10, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  FB sio chanzo kwasababu haiwatumi watu kutokua waaminifu bali ni tabia zao binafsi!
   
 8. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #8
  Feb 10, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe...in the second thought, kama kungekuwa hakuna plaform kama fb watu wangekutana kwenye daladala peke yake!!!?
   
 9. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #9
  Feb 10, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwani wakati FB hamna walikua wanakutana wapi???:twitch:
   
 10. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #10
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  uchochoroni!!!!
   
 11. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #11
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hili nalo siasa!
   
Loading...