'Radio Call' ya Kamanda Barlow yakamatwa...

'Radio Call' ya Kamanda Barlow yakamatwa...

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Joined
Sep 7, 2011
Posts
3,295
Reaction score
2,505
mengi yanazidi kufichuka. sasa zamu ya radio call kupatikana.

Sheilla Sezzy, Mwanza

POLISI mkoani hapa wamefanikiwa kuipata simu ya upepo ‘radio call' iliyokuwa ikitumiwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, marehemu Liberatus Barlow ambayo ilichukuliwa baada ya kuuawa kwa kupigwa risasi usiku wa manane eneo la Minazi Mitatu Kitangiri.

Mbali na simu hiyo, jeshi hilo pia limefanikiwa kupata ufunguo wa gari la marehemu Barlow ambaye aliuawa wakati akimsindikiza mwanamke mmoja aliyeitwa Doroth Moses walipokuwa wakitoka kwenye kikao cha harusi ya ndugu yake.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Lili Matola, alisema jana kwamba vitu hivyo vilipatikana vikiwa vimefichwa katika shimo la majitaka katika nyumba moja iliyopo maeneo ya Nyashanya.

Pia jeshi hilo limefanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa wengine wawili wanaodaiwa kuhusika katika mauaji hayo na Kamanda Matola alisema wataunganishwa kizimbani na wengine watano Novemba 15, mwaka huu.

Alisema watuhumiwa hao wawili (majina tunayahifadhi kwa sasa), mmoja wao akiwa ni ndugu wa mtuhumiwa namba moja katika mauaji hayo, ndio waliotaja sehemu vilikokuwa vimefichwa vitu hivyo baada ya kuhojiwa.

"Baada ya kuonyesha vilipokuwa vimefichwa, ilibidi kumtaarifu mwenye nyumba ambaye alitoa idhini ya kubomolewa kwa shimo hilo la majitaka na mmoja wa watuhumiwa aliingia na kutoa ‘radio call' pamoja na funguo za gari la marehemu," alisema Kamanda Matola.

Alisema kuwa baada ya kutekeleza mauaji hayo, mtuhumiwa namba moja alitoa maelekezo ya wapi pa kuficha vifaa hivyo. Kabla ya kuficha simu hiyo, waliitenganisha na betri yake.

Kamanda Matola alisema katika msako waliofanya nyumbani kwa watuhumiwa hao, pia walikuta sare za moja ya kampuni ya ulinzi pamoja na magwanda ya mgambo.

Mbali na watu hao, Matola alisema polisi pia inamshikilia mtu mmoja (jina tunalihifadhi) mkazi wa Nyakabungo akituhumiwa kufadhili kundi hilo la majambazi.
 
Kuna taarifa pia za mtuhumiwa mmoja kuachiwa huru lakini sijapata uhakika sana, nikipata hakika nitakuja kuwathibitishieni hapa
 
Kumbe polisi wetu wanaweza kufanya kazi yao. Mbona kesi ya Dr. Ulimboka imeachwa inaning'inia?
 
Kuna taarifa pia za mtuhumiwa mmoja kuachiwa huru lakini sijapata uhakika sana, nikipata hakika nitakuja kuwathibitishieni hapa

Mkuu, majina ya watuhumiwa nakumbuka kama yaliwekwa wazi nadhani baada ya kupandishwa kizimbani

Ningependa kujua jina la mtuhumiwa namba moja, tafadhari
 
Kumbe polisi wetu wanaweza kufanya kazi yao. Mbona kesi ya Dr. Ulimboka imeachwa inaning'inia?

ile ya Ulimboka ndugu yangu unadhani nao polisi hawajipendi? kweli unadhani dada anaweza kumchunguza kaka yake na kumtuhumu kwa makosa aliyofanya au atamlinda?
 
  • Thanks
Reactions: awp
Sasa nimeamini yale mauaji hayahusiani na wivu wa kimapenzi kama walivyokuwa wengine wanasema,,,,,,,!!! Kamata woote tena na huyo mwenye nyumba inawezekana anashirikiana nao
 
  • Thanks
Reactions: awp
Sasa nimeamini yale mauaji hayahusiani na wivu wa kimapenzi kama walivyokuwa wengine wanasema,,,,,,,!!! Kamata woote tena na huyo mwenye nyumba inawezekana anashirikiana nao

bado mapema sana mkuu
 
kulipiza kisasi kuzuri ni kurudisha uhai wa Barlow.
 
Mwana Mpotevu Jamani baada ya kutuwekea picha feki ya mwalim Doroth basi upepo umepita hivi2 tunaomba picha halisi ili tuendelee
na uchunguzi pleaseeeeeeeee!!!!
 
Last edited by a moderator:
images

Mambo yanafinyangwafinyangwa na mwishowe huyu mwanamke atatoka bila dhamana huku akijua mengi nyuma ya pazia. Kifo cha Kamanda huyu utetezi mwingi ni utelezi tu kama hatutaki kuamini kiini macho cha kiini cha kisiasa. Ye yote asiyetekeleza matakwa ya CCM ni adui namba one hata ungekuwa na cheo na nyota hadi mgongoni.

Baada ya kamanda Barlow kumwendea baba wa Milele, haya mapya yanaingia Mwanza kamata kamata ya magwanda. Je, Barlow wakati wake mbona hayakutokea?
 
Kumbe polisi wetu wanaweza kufanya kazi yao. Mbona kesi ya Dr. Ulimboka imeachwa inaning'inia?

Na ile ya kutekwa kwa kiongozi wa uamsho, ile ya kurishwa sumu kwa Mwakyembe, ile ya kuuwawa kwa muuza magazeti pale Moro town, na ........ Mbona hawajachukua hatua, au Kamanda alikufa sana kuliko hao baadhi?
 
  • Thanks
Reactions: awp
Mganga anajiganga kwa mbinu zote kusaka mdudu aliye kata kidole chake,

Wakati raia wamekatika miguu na mikono kabisa na bado mdudu hajaoneka wala juhudi za kumsaka zimeishia ukingoni tu
 
Na ile ya kutekwa kwa kiongozi wa uamsho, ile ya kurishwa sumu kwa Mwakyembe, ile ya kuuwawa kwa muuza magazeti pale Moro town, na ........ Mbona hawajachukua hatua, au Kamanda alikufa sana kuliko hao baadhi?

hahahahaha nimeipenda hii, kumbe kuna kufa sana na kufa kidogo duh
 
  • Thanks
Reactions: awp
Mpaka afe polisi ndipo utajua polisi wamefunzwa namna gani kukamata wahalifu.
 
Barlow alipata alichonunua. Wamezidi kutumia vyeo vibaya. Huu ni ushahidi kuwa wakubwa wetu ni wazinzi watupu kuanzia juu hadi chini. Heri wote wanaojihusisha kwenye mchezo huu yangewapata yalimpata Barlow. Ujinga na ulimbukeni mtupu. RIH Barlow. Siwezi kusema RIP wakati kifo chenyewe kimetokea kwenye mazingira ya kishetani. Napata kinyaa nikiona viongozi wa kidini eti wakiwaombea mapumziko mema peponi.
 
Kwani picha ya mwalimu doroth imeshindikana kabisa kupatikana?
 
Alisema watuhumiwa hao wawili (majina tunayahifadhi kwa sasa), mmoja wao akiwa ni ndugu wa mtuhumiwa namba moja katika mauaji hayo, ndio waliotaja sehemu vilikokuwa vimefichwa vitu hivyo baada ya kuhojiwa.

Sasa hivi majina yanahifadhiwa lakini muda si mrufu tutawaona sura zao zinaanikwa kwenye Tv zetu zote. Hii ni sawa kwenye suala zima la upelelzi makini hasa katika suala la utambuzi? Maelezo yote yameanikwa hapa na magazetini halafu unawachukuwa watu hawa unawapeleka kwa mlinza wa amani/hakimu kuandika maelezo ya ungamo ( confession), baada ya kuunganisha stori toka siku ya tukio mpaka leo ni mlizi gani wa amani/hakinu atakataa kuandika maelezo ya ungamo?

Na wanaochukua maelezo hayo wataamini nini endapo hawaelezwi upande wa pili i.e kutoka kwa waliokamatwa.

Vijana wa saidi mwema wawe objective, wasipende kufanya kazi na press, media na blogs.

Wataachieve zaidi with credibility kuliko wanavyofanya sasa.
 
Barlow yaonekana ni MFU SAFI kuliko WAFU wote...! Kule Ziwa Magharibi wanasema hivi "abafu bakilana okununka"...!
 
Sasa hivi majina yanahifadhiwa lakini muda si mrufu tutawaona sura zao zinaanikwa kwenye Tv zetu zote. Hii ni sawa kwenye suala zima la upelelzi makini hasa katika suala la utambuzi? Maelezo yote yameanikwa hapa na magazetini halafu unawachukuwa watu hawa unawapeleka kwa mlinza wa amani/hakimu kuandika maelezo ya ungamo ( confession), baada ya kuunganisha stori toka siku ya tukio mpaka leo ni mlizi gani wa amani/hakinu atakataa kuandika maelezo ya ungamo?

Na wanaochukua maelezo hayo wataamini nini endapo hawaelezwi upande wa pili i.e kutoka kwa waliokamatwa.

Vijana wa saidi mwema wawe objective, wasipende kufanya kazi na press, media na blogs.

Wataachieve zaidi with credibility kuliko wanavyofanya sasa.

Jamaa mmoja anaitwa Mganyizi, ITV imebainisha tukio zima akifukua choo kuchomoa simu na Radio call. Kaeleza mbele ya umma kuwa yeye ndie alieenda na mwenzie kutupa hivyo vitu kwenye tundu la choo baada ya kutakiwa kufanya hivyo na kiongozi wao. Jamaa anaonekana kama washamvuruga akili kwa jinsi anavyomwaga taarifa hewani!
 
Back
Top Bottom