Matatizo Mengi katika nchi yalitokana na awamu ya tatu ya BWM.
1. Ubinafsishaji wa mashirika ya umma.
hili lilikuwa kosa namba moja ambalo ndio
lilianzisha ufisadi mkubwa unaolitia taifa
hasara.
2. Kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari,
kutoruhusu uwazi kwenye utendaji
na utemi kwenye mambo ya msingi.
3. Ushemeji kwenye mali za umma.
Leo ukiangalia kila skendo iliyoibuka awamu ya nne ya JK utaona mwanzo wake ni awamu ya tatu na mzizi uliwekwa awamu ya tatu, makosa makubwa yaliyofanywa kwenye utawala wa awamu ya tatu ya BWM yameligharimu taifa kuanzia awamu ya nne, tano mpaka awamu ya sita yatatugharimu tusipo kuwa serious.
Siku unafiki utakapoachwa na ukweli ukasemwa kwenye taifa hili kwa maslahi ya tanzania na watanzania wote basi ni hapo taifa la tanzania litakapokuwa taifa lililoendelea..