TCCA Yatoa Semina kwa Kamati ya Miundombinu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

TCAA YATOA SEMINA KWA KAMATI YA MIUNNDOMBINU

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Selemani Kakoso akitoa maelekezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Mhe. Atupele Mwakibete, Katibu Mkuu-Uchukuzi, Gabriel Migire na Wataalam wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TCAA) hawapo pichani, baada ya kamati hiyo kupewa semina na Mamlaka hiyo Bungeni jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Mhe. Atupele Mwakibete akifafanua jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu shughuli mbalimbali za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini (TCAA), wakati mamlaka hiyo ilipotoa semina kwa kamati hiyo Bungeni jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,(Sekta ya Uchukuzi) Mhe. Atupele Mwakibete akizungumza na Katibu Mkuu-Uchukuzi, Gabriel Migire kabla ya kuanza semina iliyotolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini (TCAA) kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Bungeni jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini (TCAA), Hamza Johari akifafanua jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu shughuli za mamlaka wakati alipokutana na Kamati hiyo, Bungeni jijini Dodoma.

Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini (TCAA), Hamza Johari (hayupo pichani) kuhusu masuala mbalimbali ya mamlaka hiyo, wakati walipopewa semina hiyo, Bungeni jijini Dodoma.

Sehemu ya wataalam wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini (TCAA), wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka, Hamza Johari (hayupo pichani) wakati Mamlaka ilipotoa semina kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Bungeni jijini Dodoma.
 

Attachments

  • 1-1536x1024.jpg
    1-1536x1024.jpg
    71.4 KB · Views: 1
  • 2-1-1536x1024.jpg
    2-1-1536x1024.jpg
    65.5 KB · Views: 1
  • 3-1536x1024.jpg
    3-1536x1024.jpg
    75.9 KB · Views: 1
  • 4-1536x1024.jpg
    4-1536x1024.jpg
    67 KB · Views: 1
  • 5-1536x1024.jpg
    5-1536x1024.jpg
    80.2 KB · Views: 1
  • 6-1536x1024.jpg
    6-1536x1024.jpg
    80.7 KB · Views: 1
Back
Top Bottom