Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari amesema rada iliyofungwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Junius Nyerere imezeeka.
Rada hiyo ilinunuliwa kwa mabilioni ya shilingi kutoka kampuni ya vifaa ulinzi ya BAE Systems ya uingereza na kuzua mtafaruku kwa madai ilikuwa kuukuu.
Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es salaam jana Johari alisema rada hiyo ilinunuliwa mwaka 2002 na uhai wake ulikuwa kati ya miaka 10 hadi 12 hivyo haina uwezo tena wa kufanya kazi.
Kutokana na hali hiyo mamlaka itanunua rada nne ambazo zitafungwa katika mikoa ya Dar es salaam, kilimanjaro, Mwanza na Mbeya.
Kwenye mawasiliano hatuna tatizo kubwa ila rada iliyopo imezeeka na imepitwa na muda, imechokachoka hivyo tukifunga rada hizo anga yetu itaonekana vizuri tofauti na ilivyo sasa.
Chanzo.. Gazeti Jambo Leo.