wengi tulipenda kukuita James bond, akili kubwa,master, Michael scofield,Mr fursa,jasiri mfungua njia,the don,boss ruge na mengine mengi.
hayo majina yote hapo juu uliendana nayo kutokana na moyo uliokuwa nao namna ulivoweza kusaidia watu katika sekta mbalimbali kwa kuwainua wengi kuichumi ambao mpaka leo wanaishi kwa busara zako wewe,ingawa juu ya sifa zote hizo wapo baadhi ambao walilalamika juu ya fitina zako juu yao kwa kuwarudisha nyuma kimaendeleo lakin wengi walikuombea mema mana ulisaidia wengi kuliko uliowaumiza.
karibu mwezi mzima nimekaa nikitathimin yale ambayo uliyasimamia na yalienda vizuri katika kila sekta lakin leo yameanza kupotea na nazani baada ya mwaka hamna litakalokuwepo kati ya haya;
1.Wasanii wakubwa uliowatengeneza wewe leo wamebaki hata hawaelew wanaimba nn wengine wanatoa nyimbo leo wiki hawaeleweki nyimbo zao zimeenda wap mfano Tanzania one(Nasibu) kwenye muziki amebaki anaimba matusi sio yule ambae ulimtunza ww akaimba nyimbo zinazoishi mpaka leo na mwenzie Tanzania two(Ally)toka ulipolala kitandani pale kairuki ndo basi tena wanaishi kwa nguvu za mashabiki waliotengeneza kipindi wapo chini yako.
2.T.H.T kuna siku nilikaa nikamsikiliza muki wa makomando aliongelea nidhamu mbovu iliopo pale shuleni kwako baada ya kuondoka wewe na namna wanafunzi wako walivyokata tamaa,kwa hiyo wengi hawaendi tena kujifunza mziki bali wanashinda studio kwa ma producer kutafuta nafasi na kututolea nyimbo mbovu mwisho hawapati hata shoo na kuishia kuwa vibaka tu mtaani sababu ya stress.
3.Ofisi(Clouds) siku hizi limekuwa sio jengo la kushtua tena kama zaman tulivokuwa tunapapalikia kisa kutafuta nafasi ya kuonana na wewe ili utupe njia jasiri wetu,asaiv mjengoni tunapaona kama ofisi ya ebony fm iringa mana tunajua nafasi za kuingia pale ni nyepesi sio kama kipind upo wewe kwanza lingine nikuambie huko uliko ofisi asaiv hata rangi haipakwi na kila mtu kawa papa kisa hawamuogopi tena Sheba na Tirarira kama kipind ulivokuwepo ww.
4.Upcoming artists ambao uliweza kuwatengeneza kila mwaka asaiv hawapo tena toka umewatoa Benson na Jay melody ingawa nao washapotea mana nguvu yao ulikuwa ww,hawajatokea tena zaid hao upcoming asaiv wapo kwenye vigodoro huko wanakomaa na Boss wao Majizzo.kwa hiyo ule mziki mzuri wa vijana uliowatengeneza hakuna tunasikia tu mitusi kwenye nyimbo za vijana wako WCB.
5.Siasa imebaki kwa rafiki yako kipenz January tu,hao wengine uliosaidiana nao wamebak kama waimba taarabu tu mpaka unajiuliza Ruge aliwezaje kukaa na marafiki viazi namna hii au aliwavumilia vipi basi unabak na jibu kuwa sasa alikuwa mtu wa watu.
6.Fiesta huu mwezi wa saba tena kipind cha jua mikoa yote lakin naona hata uhamasishaji hamna sijajua kuwa wanauogopa upand wa pili mana kuna monsters uliowatengeneza ww bila kujua wangekuja kukugeuka na leo ndo wanaisambaratisha tamasha ulilojivunia ww na uliowaacha hawana nguvu tena ya kushindana na wale uliowapa njia zote.
5.Mwisho wale wanamziki ambao kuimba ilikuwa zero sema uliwabeba hvo hvo kutokana na nguvu uliokuwa nayo kwenye industry asaiv wanasikiliza music yao vyumban mana hata hatuwaelew wanaimba nini na wengine asaiv wanajishughulisha na shughul zingine kama kuuza vyakula mana wanajua kimziki hawawez au walikuwa hawajui ila ww ndo uliwabeba.
NINAYO MENGI YA KUKUONGELEA LAKINI ACHA NIISHIE HAPA MSALIMIE SANA DR.MENGI