Castle_Lite
JF-Expert Member
- Sep 10, 2016
- 4,505
- 9,966
Mtume alishushiwa Quran miaka 600+ baada ya Uyahudi na Ukristo kuwepo.
Kwa mtindo wa Wahyi na mara 2 kwa kuonana ana kwa ana na Jibril.
Swali langu,
1. Imewezekanaje Quran kuwe na visa vya wana wa Waisrael. Ina maana na vywenyewe Mohamed alikuwa anaoteshwa?.
(Yona au Yunus, ibrahim , sodoma na gomora nk)
Hizi zote Jibril alimfunulia Mohamed sio? Kwamba hakuwa anazijua na waarabu walikuwa hawazifahamu?.
(Hapa Nina maanisha visa ambazo haviko kwenye Torati, ) je zilishushwa na Allah kwa wahyi?.
Na Kwa ufafanuzi zaid Tourat ni kitabu kimoja alichoshushiwa Musa
Al-Isra 17:2
"Na tukampa Musa Kitabu, na tukakifanya kuwa ni uongofu kwa Wana wa Israili...
Al-Ahqaf 46:12
"Na kabla yake kilikuwa Kitabu cha Musa kilichokuwa kiongozi na rehema"
2. Ni kitabu gani ambacho Nabii Issa alipewa?.
Quran 19 : 30
"Hakika mimi ni mja wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu na amenifanya Nabii."
Ilhali Injili iliandikwa na Wanafunz wa Yesu.
3. Kwanini ilichukua miaka 23 kukamilika wakat Quran yote ilishushwa siku moja usiku kwenye mwez wa ramadhan Laylatul-Qadr
(Lauhul-Mahfuz mpaka Baitul-'Izzah).
4. Ameshushiwa Mohamed ila walioiandika ni wafuasi wake baada ya yeye kufa.
Kwanini asingekusanya na kupanga aya zote na kukamilisha kitabu kamili yeye mwenyewe?.
Kama alivyodai kuwa amepewa Kitabu.
5. Muislam wa kwanza ni Mtume Mohamed.
Kama sio sahihi naomba mnijibu kwa kutumia Quran huku ukiweka pia akilini maana ya kusilimu na shahada.
Jagina Kazakh destroyer adriz gallow bird Covax hateeb10 na wengine niliowasahau naomba mnisaidie kujibu.
Pia kwasababu Quran ina amini kwenye Torati ,Zaburi na Injili.
Ina maana maneno yote ya vitabu hivi ni ya kweli kwasababu hauwez kuchagua baadhi na kuacha baadhi.
Kukataa haya naomba uniwekee aya ya Quran inayokanusha.