QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

Ni makusudi na maringo tu
APA ukute anatuchora na acc nyingine na kujifanya mmoja wa wanataka story,
Ana
Unaah Huyu
Kila akiweka story matatizo , wakati ukitizama mahudhurio yake huko nyuma sii hivi
Acha unaa
Luge
Aisee!! kweli una hasira, LEGE hebu njoo huku, hali sio nzuri
 
wakuu msilalamike sana na poleni sana msione kama nafanya kusudi kama wengine mnavyosema hapana but ni majukum yamekuwa mengi kweli kweli.leo nilipanga nikate kiu yenu yote lkn hapa nimekatika stimu hatari.now ndio nafika home nafungua begi nakutana na laptop bila chaji. hivyo mkiona nimeweka sehem mbili tatu msishangae sanaa ila kesho asubuhi kabla ya saa 5 nauhakika nitakuwa nimeweka sehem za kutosha sanaa.nitafidia na nitahakikisha namaliza season namba 1.
 
Jamaa amekausha jumla, hasemi chochote. Mwanzo alikua anakuja japo kutujulisha kwamba ana tatizo hivyo tuvute subira, tofauti na sasa ambapo amepotea kabisa. LEGE popote ulipo, kama umepata matatizo tunakuombea sana, lakini kama uko salama tunaomba ujitahidi uje huku utushushie muendelezo.
sijakausha mkuu but mambo nayo kama yamepeana taarifa vile maana yamepandana na kupandana.usawa wa anko magu huu sio wakulemba na kulegea legea wakuu.JF story nitatupia mpaka nukta ya mwisho kama ilivyokuwa kwenye peniela wakuu.natamani kweli nifanye mtakavyo lkn ndio siwezi uzuri kuna member humu nimeshinda nao siku mbili hizi na wao ndio wamenifanya niwe adimu hapa kuweka mwendelezoo
 
SEHEM YA 54

Kichwa cha Dr Marcelo Richard kilikuwa
kizito kwa mawazo mengi aliyokuwa nayo
baada ya kuachana na Monica.
“ Nahisi kama vile kichwa changu
kimebeba mzigo mzito .Suala hili linaanza
kunichanganya kichwa changu sana na
sielewi nifanye nini kumpata mtu
aliyeingia chumbani kwangu na kufungua
kasiki langu.Kinachonishangaza zaidi kwa
nini mtu huyu atake Monica afahamu
kama ninasumbuliwa na saratani ya
damu? Jibu la haraka haraka ninalopata ni
kwamba lengo lake ni mimi na Monica
tusiwe karibu na kwa hilo nadhani
amefanikiwa kwani I’ve already lost
Monica.Mipango yangu yote niliyokuwa
nayo kuhusu Monica imeyeyuka.Tayari
kila kitu kilianza kwenda vizuri na Monica
alionyesha kila dalili ya kunikubali lakini
baada ya kufahamu kwamba mimi nina
maradhi ya saratani ya damu na kwamba
sina maisha marefu hayuko tayari kuwa
na mimi tena.Nani huyu lakini
aliyenifanyia ukatili huu mkubwa? I’ve
never been happy in my life.Nilitegemea
japo kwa mara ya kwanza katika maisha
yangu niwe na furaha baada ya kukutana
na Monica lakini binadamu wakatili
wameivuruga mipango yangu yote .I swear
I must find the person who did this to me.”
Akawaza Dr Marcelo na kuuma meno kwa
hasira.
Alielekea moja kwa moja nyumbani
kwake.Ndani alikuwepo mtumishi wake
wa kazi za ndani ambaye huja asubuhi na
kuondoka saa kumi za jioni akiendelea na
kazi.Dr Marcelo akashuka garini na moja
kwa moja akaelekea katika mlango
mkubwa wa kuingilia sebuleni akajaribu
kuuchunguza kwa makini lakini haukuwa
umevunjwa sehemu yoyote.
“ Mvamizi huyo lazima alitumia
funguo bandia kufungua mlango kwani
hakuna sehemu mlango huu ulikovunjwa
.Siwezi kabisa kumuhusisha mama Salama
katika jambo hili kwani yeye ana funguo
za milango mitatu tu.Huu wa sebuleni ,wa
nyuma ya nyumba na wa geti.Hajawahi
kungia chumbani kwangu kwani hata
kama ni usafi huwa ninafanya mimi
mwenyewe.Aliyeingia chumbani kwangu
ni mtu mtaalamu sana” akawaza na
kuelekea chumbani kwake.Akalifungua
kasiki akalichunguza halafu akaenda
kukaa kitandani
“ Niwataarifu polisi kuhusu
kupatikana kwa faili hili la taarifa zangu
za ugonjwa? Akajiuliza
“ Nikiwataarifu lazima watakwenda
kuanza kumuhoji Monica,jambo ambalo
sitaki litokee kwani hahuski chchote na
jambo hili.Ngoja niachane na wazo hili
.Monica ana mambo mengi kwa sasa kwa
hiyo sitaki kumbughudhi kwa mambo
mengine “ akajilaza kitandani na kuzama
mawazoni lakini ghafla akakurupuka
baada ya kukumbuka kitu.
“ A book..!! akasema
“ NImekumbuka kile kitabu..!!
akaenda haraka katika kasiki
akachungulia
lakini
kitabu
hakikuwemo.Akafungua kabati lake
kubwa la kuhifadhia vitabu akapangua
kitabu kimoja kimoja lakini kitabu
anachokitafuta hakikuwemo
“Nakumbuka kitabu nilikihifadhi
humu katika kasiki .Wamekichukua.oh my
God” akasema Dr Marcelo na kushika
kiuno.
“ Kulikuwa na tsh milioni thelathini
na nane katika kasiki lakini hizo
hazikuguswa hata senti moja badala yake
 
SEHEM YA 55

wakachukua baadhi ya vitu kama faili hili
na hicho kitabu.Ninachojiuliza kwa nini
wachukue kitabu waache fedha? Kitabu
kile kina thamani gani? akajiuliza na
kuanza kurudisha kumbu kumbu nyuma.
DAR ES SALAAM 2005
Hali ya jiji la Dar es salaam ni ya
mvua kubwa na mitaa miingi imefurika
maji,katika uwanja wa ndege wa kimataifa
wa Julius Nyerere, Dr Marcelo Richard
anawasili na ndege ya shirika la ndege la
Tanzania akitokea masomoni nchini
China.Uwanjani hapo alipokewa na dada
yake Julieth
“ Vipi hali ya mzee anaendeleaje?
Akauliza Dr Marcelo wakiwa garini
“ Mzee hali yake si nzuri na
madaktari wametueleza ukweli kwamba
he wont make it.Imekuwa vizuri umekuja
kwani mzee hana muda mrefu sana wa
kuishi” akasema Julieth.
Waliwasili nyumbani kwao ambako
kila aliyekuwapo alikuwa na sura ya
majonzi makubwa kutokana na hali ya Dr
Richard Wendelic Richard bingwa wa
magonjwa ya moyo kuzidi kudhoofika .Dr
Richard aliyekuwa akifahamika kwa
umahiri wake katika upasuaji wa moyo
alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya
saratani ya damu .Pamoja na jitihada zote
za familia yake kujaribu kumtibu lakini
hakukuwa na unafuu wowote na
madaktari waliihakikishia familia yake
kuwa Dr Richard hataweza kupona
maradhi yanayomsumbua.
Baada ya Dr Marcelo kuwasili
akitokea nchini China alikokuwa
akisomea masuala ya neva za fahamu Dr
Richard akawataka watu wote mle
chumbani watoke wamuache yeye na Dr
Marcelo .
“ Marcelo nashukuru sana umekuja
kwa wakati kama nilivyoagiza.” Akasema
Dr Richard akavuta pumzi ndefu na
kuendelea
“ Nadhani tayari umekwisha pewa
taarifa na ndugu zako kwamba matibabu
yameshindikana na hakuna namna tena so
I have to die.Ninafurahi kwamba ninakufa
lakini mmoja wa wanangu ni daktari
lakini ningekushauri baada ya kumaliza
masomo yako kuhusu neva za fahamu
,usomee pia kuhusu maradhi yanayokuja
kwa kasi na kuua watu wengi hivi sasa
,maradhi
ya
saratani
ya
damu.Nimekushauri kwa muda mrefu
sana usomee kuhusu maradhi haya lakini
haukuwa tayari.Nataka leo niweke wazi
kwa nini nilikuwa nakusisitiza sana
kuhusu kusomea maradhi ya saratani ya
damu.” Dr Richard akavuta pumzi ndefu
akamtazama mwanae kwa makini.Mvua
kubwa ilikuwa inanyesha huko nje na radi
zikimulika
“ Marcelo wewe pia una saratani ya
damu”
“ What ?? Dr Marcelo akastuka sana
“ Una saratani ya damu pia” akasema
Dr Richard.Dr Marcelo akastuka kama vile
ameona dudu la kutisha akamtazama baba
yake kwa macho makali
“ Tell me its not true dady !! akasema
Dr Marcelo
“ Its true Marcelo” akasema Dr
Richard.
 
SEHEM YA 56

r Marcelo akamtazama baba yake
kwa karibu dakika mbili huku machozi
yakimtoka akasema
“ No that’s not true .Kama ningekuwa
na tatizo hilo kwa nini miaka hii yote
nisijue kama nina saratani hiyo ya damu?
I’m fine na sina tatizo lolote.Please dady
don’t lie to me kwa sababu tu unataka
nkasomee kitu unachokitaka wewe”
“ I’m not lying to you my son.Its
true.Una chronic mylegonous leukemia.Hii
ni saratani ya damu ambayo husambaa
taratibu sana na mtu mwenye aina hii ya
saratani anaweza akapata dalili chache au
asiwe kabisa na dalili kwa miaka mingi
kabla ya ugonjwa kufumuka na kuanza
kumshambulia.Kwa hiyo Marcelo naomba
unsikilize
ninachokushauri
mwanangu,hakikisha umesomea maradhi
haya ya sarataniya damu ili uweze
kujisaidia wewe mwenyewe na vile vile
kuwasaidia wengine wanaosumbuliwa
nayo” akasema Dr Richard
“ Dady no ! that’s not true..!!
“ Its true my son.Samahani sana kwa
kutokufahamisha kuhusu jambo hili
mapema sikutaka nikuchanganye katika
masomo yako.Tafadhali zingatia hayo
ninayokwambia na utaishi miaka
mingi.Jambo lingine ambalo ninataka
ulifanye baada ya mimi kufariki,ukisha
hitimu masomo ya saratani ya damu
nataka kama familia mjenge hospitali
kubwa ya kuwahudumia wagonjwa wa
saratani ambayo itakuwa ni kwa kumbu
kumbu yangu. “ akanyamaza kidogo halafu
akaendelea
“ Jambo la mwisho ambalo nataka
ulifanye,..” akasema Dr Richard
akamuomba
Marcel;o
amsaidie
kunyanyuka pale kitandani akatembea
taratibu hadi katika kasiki lililokuwa
ukutani akalifungua na kutoa kitabu
“ Kitabu hiki ni muongozo wako kila
pale utakapokuwa umepatwa na tatizo
lolote katika kazi zako za kitabibu.Mimi
kimekuwa ni msaada mkubwa sana
kwangu katika maisha yangu ya kitabibu
na kwa kuwa sasa maisha yangu ya
kitabibu yanakwenda kufikia mwisho
ninakukabidhi wewe.Kitabu hiki kitakupa
muongozo wa mambo mengi hususan
mambo ya kitabibu .Mimi nimekuwa
daktari mkubwa na kuheshimika afrika ni
kwa sababu ya kitabu hiki.Kitabu hiki si
kitabu rahisi kukielewa na kabla hujaanza
kukisoma kuna mtu ambaye unapaswa
kuonana naye ambaye atakupa maelekezo
ya jinsi ya kukisoma kitabu hicho.
Naomba uchukue kalamu na uziandike
namba hizi ntakazokutajia.Halafu jambo
lingine kitabu hiki ukitunze sana
asiruhusiwe kukishika mtu mwingine
yeyote zaidi yako” Akasema Dr Richard na
kumtajia Dr Marcelo namba za simu
akaziandika katika kijitabu.
Dr Marcelo akafuta jasho baada ya
kumbukumbu ile kumjia
“ Sikuwahi kukifungua kitabu kile
kukisoma kwani toka nilipokabidhiwa na
baba siku ile nilizunguka nacho nchi mbai
mbali nilizosoma na niliporejea hapa
nyumbani nilikihifadhi katika kasiki na
kukisahau kabisa hadi leo hii
nilipokikumbuka.Nini kiliandikwa katika
kitabu kile? Aliyekichukua anafahamu
umuhimu
wake?
Anafahamu
kilichoandikwamo? Akajiuliza Dr Marcelo
“ Ninakumbuka siku ile baba
wakinikabidhi kitabu hicho alinitajia
namba Fulani nikaiandika katika kitabu
 
SEHEM YA 57


changu cha kumbu kumbu na sikuwahi
kupiga namba hiyo.Aliniambia kwamba
kabla ya kukisoma kitabu hicho
ningehitaji maelekezo toka kwa huyo mtu
aliyenipa namba zake .Nakumbuka kitabu
kile cha kumbu kumbu nilichoandika
namba zile kilijaa na nikakihifadhi katika
kabati langu la kutunzia vitabu. “ akawaza
Dr Marcelo na kutoka mbio hadi katika
chumba chake cha kusomea akafungua
kabati kubwa la kuhifadhia vitabu na
kuanza kukitafuta kitabu alichoandika
namba zile alizopewa na baba
yake.Haikuwa kazi rahisi kutokana na
vitabu vingi alivyokuwa navyo.Ilimchukua
zaidi ya saa mbili kuweza
kukipata.Alikuwa ameloa jasho mwili
mzima.Haraka haraka akaanza kuzitafuta
namba zile na akazipata.
“ Nimezipata namba za mtu huyu
ambaye angenipa maelekezo kuhusu
kitabu kile ,nifanye nini sasa? Akajiuliza
na mara akapata wazo,akachukua simu na
kumpigia Monica
“ Dr Marcelo” akasema Mnica baada
ya kupokea simu
“ Monica samahani kwa
kukusumbua.”
“ Bila samahani Dr Marcelo”
“ Monica nina tatizo nahitaji
kuonana nawe sasa hivi” akasema Dr
Marceo na zikapita sekunde kadhaa
“ Uko wapi sasa hivi? Akauliza
Monica
“ Niko nyumbani kwangu” akasema
“ Naomba tukutane Savana garden”
akasema Monica
Bila kupoteza wakati akatoka haraka
kwenda kukutana na Monica
 
SEHEM YA 58

“ Dr Macelo kuna tatizo gani? akauliza
Monica baada ya kukutana na Dr Marcelo
mahala walikopanga wakutane.Uso wa Dr
Marcelo ulionyesha wazi kwamba kuna
jambo lililokuwa linamsumbua akavuta
pumzi ndefu na kusema
“ Monica naomba kwanza
nikushukuru kwa kusimamisha shughuli
zako na kuja kunisikiliza.Ahsante sana
kwa kunithamini” akasema Dr Marcelo
“ Usijali Dr Marcelo,nieleze kuna
tatizo gani? akauliza Monica.Dr Marcelo
akainamisha kichwa kwa sekunde kadhaa
halafu akasema
“ Monica,tulipoachana nilielekea
moja kwa moja nyumbani kutuliza akili na
kujaribu kulitafakari suala lililotokea kwa
makini zaidi. Wakati nikijaribu
kulitafakari suala hilo na kuitafakari
dhamira ya mtu aliyefanya jambo lile
nikakumbuka kitu Fulani” akanyamaza
“ Jambo gani hilo Dr Marcelo?
Akauliza Monica
“ Wakati baba yangu akiwa katika
siku za mwisho za uhai wake ,nilikuwa
masomoni nchini China ikanilazimu
kurejea nyumbani na siku niliyorejea
nilikuwa na maongezi naye.Alinieleza
kwamba kutokana na ugonjwa wake wa
saratani ya damu uliokuwa unamsumbua
hataweza kupona.Alinieleza mambo mengi
ikiwa ni pamoja na kunisisitiza kwamba
nihakikishe nimesomea kuhusu saratani
ya damu.” Akanyamaza kidogo halafu
akaendelea
“ Katika maongezi hayo ndipo
aliponipa wazo la kujenga hospitali ya
kuwahudumia wagonjwa wa saratani ya
damu kwa kumbu kumbu yake.Pamoja na
yote aliyonieleza kuna mambo mawili
makubwa.Kwanza alinieleza kwamba
nilikuwa na saratani ya damu pia.Sikuwa
nikilifahamu hili kwani sikuwahi kuwa na
dalili zozote za saratani lakini akanieleza
kwamba aina ya saratani niliyokuwa nayo
ni chronic myelogenous leukemia ambayo
ni aina ya saratani inayosambaa taratibu
na huchukua miaka hadi kugundua.”
Marcelo akanyamaza tena akainamisha
kichwa na baada ya sekunde kadhaa
akasema
“ Tukiachana na hilo kuna jambo
lingine ambalo sikuwa nimelitilia maanani
lakini leo nikiwa natafakari juu ya hiki
kilichotokea ndipo nilipolikumbuka.Siku
ile nilipoongea na baba alinipa kitabu
Fulani chenye jalada gumu la kijani
akanieleza kwamba ni kitabu muhimu
sana ambacho natakiwa nikitunze na
nihakikishe hakuna atakayekisoma zaidi
yangu.Alinieleza kwamba kitabu kile ni
muongozo wangu katika kazi zangu za
kitabibu na mambo mengine mengi.Kwa
maelekezo aliyonipa ni kwamba kila pale
nitakapokuwa na tatizo katika masuala
yangu ya kitabibu au masuala binafsi basi
nikitumie kitabu hicho chenye kila kitu
ndani yake lakini akanieleza kwamba
kabla sijakisoma kitabu hicho kuna mtu
ambaye natakiwa kuwasiliana naye
ambaye atanipa maelekezo ya namna ya
kukitumia .Alinipa namba za simu za mtu
huyo nikaziandika katika kijitabu
Fulani.Toka aliponipa kitabu hicho
sikuwahi kukisoma au hata kukifungua
kujua kilichomo ndani yake.Baada ya
kumaliza masomo yangu nilikihifadhi
kitabu hicho katika kasiki langu na
sikuwahi kukigusa tena.Leo hii ndipo
nilipokikumbuka na nilipokiangalia lakini
hakikuwemo
katika
kasiki.Mtu
aliyefungua
kasiki
alikichukua
.Nikazikumbuka namba za Yule mtu
ambaye baba alisema kwamba nimpigie ili
anipe maelekezo ya namna ya kukitumia
kitabu
hicho.Nilikitafuta
kitabu
nilichoandika namba hizo nikakipata na
 
SEHEMU YA 59

kuzipata hizo namba ambazo ni hizi hapa”
akasema Dr Marcelo na kumpatia Monica
zile namba .
“ Umejaribu kupiga namba hizi?
Akauliza Monica
“ Hapana sijajaribu kupiga.I’m
scared” akasema Dr Marcelo
“ Kwa hiyo hujui kitabu hicho kina
nini ndani yake? Akauliza Monica
“ Ndiyo Monica.Kama nilivyokueleza
kwamba sikuwahi kukifungua toka baba
alivyonikabidhi.Sikutaka kabisa kujua
ndani yake kuna nini” akasema Dr
Marcelo.
“ Unadhani aliyekichukua anaweza
kuwa na ufahamu wa kilichomo ndani ya
kitabu hicho? Akauliza Monica
“ Sifahamu Monica ila ninahisi kitu
kama hicho kwa sababu mtu huyo hakuwa
na nia na fedha bali baadhi tu ya vitu
kwani ndani ya kasiki kulikuwa na fedha
kiasi cha shilingi milioni milioni thelathini
na nane lakini hazikuguswa hata senti
moja badala yake akachukua faili langu la
matibabu pamoja na hicho kitabu.Ninahisi
yawezekana labda alilenga katika vitu
hivyo pekee” akasema Dr Marcelo
“ Hili suala mbona linanikanganya
sana.” Akasema Monica
“ Kweli Monica suala hili
limenikanganya hata mimi na sielewi
malengo ya huyo mtu.Lengo la kwanza ni
kuufichua ugonjwa wangu kwako lakini
sijui lengo la kukichukua hicho kitabu ni
nini.Laiti nigekuwa nafahamu kilichomo
ndani ya kitabu hicho ningeweza kupata
walau mwanga lakini sikuwahi
kukifungua kitabu hicho na sielewi
kuliandikwa nini.” akasema Dr Marcelo
“ Piga hizo namba za huyo mtu
ambaye ulielekezwa kwake ili akupe
maelekezo ya kukisoma kitabu hicho
uongee naye ” akasema Monica
“ Monica I’m scared.Ni miaka mingi
imekwisha pita ” akasema Dr Marcelo
“ Hutakiwi kuogopa Dr Marcelo.Nina
hakika huyo mtu anaweza akakupa
mwanga ili tufahamu kilichomo ndani ya
kitabu hicho na tukijua kilichomo basi
inaweza kuturahishia kufahamu lengo la
mtu aliyekichukua kitabu hicho.” Akasema
Monica.Dr Marcelo akaziandika namba
zile katika simu yake halafu akataka
kupiga akasita.
“ Piga Dr Marcelo usiogope” akasema
Monica lakini Dr Marcelo bado alionyesha
uoga.Monica akaichukua ile simu ya Dr
Marcelo na kupiga zile namba simu
ikaanza kuita
“ Simu inaita” akasema Monica na
kumpatia Dr Marcelo simu
“ Hallow” ikasema sauti nzito ya
kiume upande wa pili baada ya kupokea
simu
“ Hallow..” akasema Marcelo
“ Naongea na nani tafadhali” akauliza
Yule mtu upande wa pili
“ Naitwa Dr Marcelo,nilipewa namba
hiz......” Kabla hajamaliza kujieleza simu
ikakatwa
“ Amekata simu” akasema Dr
Marcelo kwa wasi wasi
“ Kwa nini hakutaka kukusikia
ulichotaka kumueleza na kukata simu
haraka haraka? Au ulikosea
namba?Akauliza Monica
“ Monica namba hizi sikuzikosea
niliziandika kwa makini sana na baba
alinitaka nizirudie mara mbili ili
ahakikishe kama nimeandika kwa
usahihi.” Akasema Dr Marcelo
 
SEHEMU YA 60


Mimi nadhani kuna umuhimu wa
kuwashirikisha polisi suala hili ili
wafahamu kinachoendelea na ikwezekana
wazifanyie
uchunguzi
hizo
namba.Nimeanza kuwa na wasi wasi sana
Dr Marcelo”
“ NI wazo zuri lakini nataka kwanza
nifanye uchunguzi wangu mwenyewe
kuhusiana na kitabu hicho na baada ya
hapo ndipo nitavishirikisha vyombo vya
uchunguzi” akasema Dr Marcelo
“ Kwa hiyo umepanga kufanya nini
Dr Marcelo?
“ Sijapata jibu bado nifanye nini
lakini nitapata tu jibu wapi pa kuanzia
uchunguzi wangu” akasema Dr
Marcelo.Ukimya mfupi ukapita halafu
Monica akasema
“ Is your mother still alive? Akauliza
Monica
“ Sikuwahi kumfahamu mama
yangu.Niliambiwa kwamba mama yangu
alifariki baada ya kufanyiwa upasuaji
wakati akijifungua mimi.Kwa hiyo
sikupata bahati hata ya kukaa naye kwa
dakika moja.Baada ya mama kufariki baba
alioa mwanamke mwingine ambaye ndiye
aliyenilea na ambaye hadi sasa bado yuko
hai.”
“ Dah pole sana kwa kuwapoteza
wazazi wako wote wawili” akasema
Monica
“ Ahsante Monica.Ni kazi ya Mungu”
“ Umefikiria kumuuliza mama yako
kuhusiana na kitabu hicho? Hudhani kama
anaweza kufahamu chochote juu ya kitabu
hicho? Akauliza Monica
“ Uhhm sikuwa nimelifikiria hilo
kwani kitabu kile baba alikuwa anakificha
sana na sina hakika kama mama alikuwa
anakifahamu” akasema Dr Marcelo
“ Dr Marcelo you have to ask
her.Wanandoa wana tabia ya kuelezana
mambo hata yale ya ndani kabisa kwa hiyo
usiogope kumuuliza pengine anaweza
kuwa anafahamu jambo Fulani kuhusiana
na kitabu hicho ambalo linaweza
kukusaidia.” Akasema Monica
“ Monica wazo lako ni zuri
sana.Nadhani hiyo ni sehemu nzuri kwa
kuanzia.Nitakwenda kuongea na mama na
kama ana lolote analolifahamu najua
lazima atanieleza” akasema Dr Marcelo
“ Dr Marcelo kuna kitu kingine
ambacho nataka nikushauri.”
“ Kitu gani hicho Monica?
“ Tukio hili lililotokea limenipa wasi
wasi sana na kwa kuwa hatuelewi lengo la
huyu mtu aliyediriki kuingia chumbani
kwako na kuchukua baadhi ya vitu vyako
vya muhimu.Kwa kuwa bado uchunguzi
unaendelea nashauri uchukue tahadhari
kubwa kuhusu usalama wa maisha
yako.Ulinieleza
kwamba
unaishi
mwenyewe na nyumbani kwako hakuna
mlinzi .Nakushauri kwa hali ilivyo sasa
hivi undoke pale nyumbani kwako kwa
muda.Njoo uishi kwangu kuna ulinzi na
usalama wa kutosha.Nina nyumba kubwa
ya kutosha hata watu mia moja.I don’t care
what people will say but what I care is
your safety.Come live with me for a
while.Mambo yakitulia utarejea nyumbani
kwako “ akasema Monica
” Monica ahsante sana kwa wazo hilo
na kwa kujali usalama wangu lakini
Usijali nitaendelea kukaa pale pale
kwangu,nitaweka walinzi wa kulinda.I’ll
be safe”
“ Are you sure? Akauliza Monica
“ yes I’m sure.I’ll be fine Monica”
“ Sawa Dr Marcelo kama
umenihakishia kwamba utakuwa salama
mimi sina tatizo.”
“ Monica naomba niende nikaonane
na mama sasa hivi.Nitakujulisha
atakachonieleza nitakapoongea naye”
akasema Dr Marcelo
“ Sawa Dr Marcelo mimi naelekea
nyumbani nakwenda kujiandaa kuonana
na David Zumo rais wa Kongo usiku wa
leo”
“ Rais wa Kongo? Akauliza Marcelo
kwa mshangao kidogo
“ Ndiyo”
“ Do you know each other? Akauliza
Dr Marcelo
“ Yes we do” akasema Monica na kwa
sekudne kadhaa Dr Marcelo akabaki
anamtazama Monica halafu wakaanza
kutembea kueleka katika maegesho yaliko
magari yao.
“ Dr Marcelo if you change your
mind,my place is the best place for you”
akasema Monica
“ Ntakujulisha Monica usijali”
akasema Dr Marcelo wakati anaingia
garini akaondoka
 
SEHEMU YA 61

Saa mbili na dakika kumi za usiku
iliwakuta
Mzee
Benedict
mwamsole,mkewe Janet na mtoto wao
Monica katika hoteli ya kifahari ya Kobe
village alikofikia David Zumo.Usoni kwa
mzee Benedict hakukukauka tabasamu
pana alikuwa na hamu sana ya kuonana na
David Zumo kiongozi mwenye sifa kubwa
afrika na dunia.
Monica na wazazi wake walipokewa
na wasaidizi wa David wakapelekwa
bustanini ambako ndiko David alipanga
akutane nao .Ilikuwa ni sehemu
iliyoandaliwa vizuri na kulikuwa na ulinzi
mkali kama kawaida ya kila mahala
anapokuwapo
David
Zumo.Walikaribishwa na wahudumu
waliovalia nadhifu wakaendelea na
vinywaji wakati wakimsubiri David
“ This place is amazing.Pamoja na
utajiri wangu wote sijawahi kufika mahali
hapa.Tumezoea kuona sehemu kama hizi
zenye uzuri wa kushangaza katika
mahoteli makubwa ya huko ulaya
.Nimefurahi sana kuona hata hapa
nyumbani tuna sehemu nzuri kama hizi”
akasema mzee Ben.
Wakati wakiendelea na maongezi
,David Zumo akiwa na walinzi wake
akashuka ghorofani na kueleka moja kwa
moja bustanini kukutana na wageni
wake.Wote wakasimama baada ya David
kuwasili pale bustanini wakasalimiana
.David alikuwa na furaha kubwa kuonana
na wazazi wa Monica.Walinzi wa David
wakajitenga mbali kidogo na mahala
walipokuwa wamekaa akina David ili
kuwapa nafasi ya kuzungumza mambo
yanayowahusu kwa uhuru zaidi
“Nimefurahi sana kuwafahamu
Bwana na Bi Benedict na Janet
Mwamsole.” Akaanzisha maongezi David
Zumo.
“ Hata sisi tumefurahi sana kukutana
nawe mheshimiwa rais .Ni heshima kubwa
umetupa ya kukutana nawe.” Akasema
mzee Benedict
“ Nisingeweza kuondoka bila
kuonana nanyi.Leo tumemaliza mkutano
wetu wa marais wa nchi za maziwa makuu
lakini nimelazimika kubaki ili kukutana
nanyi.” Akasema na kunywa funda la
mvinyo kisha akaendelea

Jana
nimekutana
na
Monica,nilimualika hapa kwa chakula na
maongezi baada ya kuguswa sana na
mambo anayoyafanya kwa jamii.Nilipofika
hapa Tanzania nilisikia kuhusiana na
mradi wake wa kujenga shule ya watoto
wenye ulemavu wa kutokuona na
kusikia.Niliguswa sana na jambo hilo na
nikaona siwezi kuondoka bila kuunga
mkono juhudi kama hizi za Monica na
ndiyo maana nikamualika hapa nionane
naye ili niweze kutoa mchango wangu
mdogo na nikajikuta nikitaka kuonana na
wazazi wake.Kwa hiyo karibuni sana
wazee wangu tule tunywe tufurahie
mafanikio ya Monica” akasema David
“ Tunashukuru sana mheshimiwa
rais .Kama nilivyokueleza mwanzo kuwa
hii ni heshima kubwa umetupa .Binafsi
sikuwahi kuhisi kama siku moja
ningeweza kukutana nawe ana kwa ana
kwa hiyo leo ni siku yangu ya furaha sana
kukutana na rais ambaye nimekuwa
nikitamani sana kukutana naye katika
maisha yangu “ akasema mzee Benedict na
sura ya David Zumo ikajenga tabasamu
kubwa .
Walipata chakula na kisha
wakaendelea na maongezi .Wakati
maongezi yakiendelea simu ya Monica
 
SEHEMU YA 62

ikaita.Akaitoa na kutazama mpigaji
,alikuwa ni Daniel.
“ Excuse me” akasema na kusogea
pembeni kuipokea simu ile
“ Hallow Daniel” akasema Monica
kwa sauti ndogo
“ Monica where are you? Akauliza
Daniel.Monica akagundua kitu katika sauti
ya Daniel
“ Niko hapa Kobe village hotel
“Akajibu Monica..Ukapita ukimya wa
sekunde kadhaa
“ Daniel kuna nini You sound
strange” akasema Monica
“ Sikiliza Monica kuna taarifa
ambazo si nzuri hata kidogo nimezipokea
muda si mrefu”
“ Taarifa gani hizo Daniel? Akauliza
Monica kwa wasiwasi
“ Monica I know you are strong
woman and please I want you to be strong
for what I’m going to tell you” akasema
Daniel
“ Daniel please tell me.What
happened? Akauliza Monica
“ Dr Macelo amepigwa risasi muda
mfupi uliopita na watu wasiojulikana”
“ What ?!! akauliza Monica kwa
mshangao
“ Dr Marcelo amepigwa risasi”
akarudia Daniel
“ Oh my God !! akasema Monica na
kukaa kimya.Alistuka mno.
“ Monica..” akaita Daniel
“ Daniel tell me he’s not dead”
“ Nimepigiwa simu na dada yake
Julieth na amesema kwamba Marcelo
amekimbizwa hospitali kuu ya St Lucia
.Mimi ninaelekea huko .Tafadhali kama
utapata nafasi uje huko hospitali”
akasema Daniel
“ Oh my God! ninakuja huko sasa
hivi? Akasema Monica na kukata simu
akarejea mezani akamuita mama yake
“ Mama nimepokea simu sasa hivi
kuwa Dr Marcelo amepigwa risasi”
“ What ??Lini? bi Janet akashangaa
“ Jioni hii.” Akajibu Monica
“ Oh my God !!!... is he dead?
“ Sifahamu hali yake ikoje ila
amekimbizwa hospitali kuu ya St
Lucia.Mama nahitaji kwenda huko sasa
hivi ”
“ Monica huwezi kuondoka katikati
ya maongezi.Mheshimiwa rais ametupa
heshima kubwa sana.Subiri hadi
tutakapomaliza
maongezi
ndipo
utakwenda lakini kwa sasa hapana.Wewe
ndiye uliyetuunganisha sisi na David kwa
hiyo huwezi kuondoka hapa na kutuacha
peke yetu” akasema bi Janet
“ Dr Marcelo is my friend mother so I
need to get there at once !! akasema
Monica
“Hata kama ukiwahi kufika pale
what will you do?.Utamponya? Hebu tuliza
kichwa Monica .Kitu cha muhimu kwa sasa
ni kumuombea ili aweze kupona kwa
sababu kama amekimbizwa hospitali ni
jukumu la madaktari kuokoa maisha
yake.Lets us get back to the table now and
keep your smile on!! akasema bi Janet
wakarejea mezani Monica alijitahidi
kutabasamu lakini bado sura yake
ilionyesha kuna kitu kinamsumbua.Sura
yake ilionyesha mstuko.
“ Monica kuna tatizo lolote? Mbona
unaonekana kubadilika ? akauliza David
Zumo baada ya kuona mabadiliko katika
sura ya Monica
 
SEHEMU YA 63

amahani sana mheshimiswa rais
nimepokea simu ambayo si nzuri,kuna
rafiki yangu amepigwa risasi jioni hii yuko
hospitali.”
“Pole sana Monica,unahitaji kwenda
hospitali sasa hivi?
“ Kama sintakuwa nimeivuruga
ratiba ya leo ,ndiyo”
“ Hakuna kitakachoharibika
Monica.Nenda hospitali .Kama kuna
chochote ninachoweza kusaidia tafadhali
usisite kunieleza” akasema David Zumo na
kumuita moja wa walinzi wake
akamnong’oneza kitu kisha mlinzi Yule
akamuomba Monica amfuate.Monica
akainuka akamuaga David na wazazi wake
lakini ghafla mama yake naye akainuka.
“ Nadhani itakuwa vyema
nikiongozane naye “ akasema bi Janet
“ Hilo ni wazo zuri pia “ akasema
David.Monica na mama yake wakaondoka
kuelekea hospitali.
“ Mr Benedict,sasa baada ya
wanawake kuondoka mezani tuongee
kama wanaume.” Akasema David Zumo na
kumimina mvinyo katika glasi akapiga
funda kubwa na kusema

Benedict
nimekufuatilia
nimegundua wewe ni mmoja wa
mabilionea wakubwa wa hapa
Tanzania.Biashara zako zinakwendaje?
Akaulzia David Zumo
“ Ni kweli mheshimiwa rais mimi ni
mmoja wa wafanya biashara
wakubwa.Ninamiliki biashara kadhaa
kubwa hapa nchini na hata nje ya
nchi.Kibiashara ninaendela vizuri
japokuwa changamoto hazikosekani na
hasa ushindani katika masoko umekuwa
mkubwa sana bain aya viwanda vyetu vya
afrika na bidhaa toka viwanda vya ulaya.”
Akasema mzee Benedict
“ Benedict ninafurahi kwa kuwa
kuanzia sasa utakuwa mmoja wa watu
wangu wa karibu kibiashara.Ninawapenda
wafanya biashara kwani hata mimi pia ni
mfanya biashara kwa hiyo usijali kuhusu
changamoto zilizopo” akasema David
Zumo na kunywa tena funda la mvinyo
kisha akaendelea
“ David tuweke mambo mengine yote
pembeni ,kuna jambo moja la muhimu
sana ambalo nataka kulijadili nawe”
akasema David halafu akatoa sigara toka
katika mkebe akaiwasha na kuvuta
mikupuo kadhaa akapuliza moshi kisha
akasema
“Benedict wewe ni mtu mkubwa na
ajiri lakini bado haujafikia kile kiwango
cha kimataifa.Nina mawazo ya kukufanya
mtu mmoja mkubwa na mwenye nguvu
yaani tajiri mkubwa.Nataka kulipaisha
jina lako liwe miongoni mwa matajiri
wakubwa wanaojulikana dunia kwani kwa
sasa unajulikana zaidi hapa Tanzania na
afrika mashariki na baadhi ya nchi chache
za ulaya unakouza bidhaa zako za
mvinyo.Nataka ujulikane dunia nzima,na
siku moja ushiriki katika vikao vya
matajiri mia moja wa dunia hii.”
“ Matajiri mia moja? Sijawahi kusikia
kitu hicho” akasema Benedict
“ Huwezi kufahamu kwa kuwa wewe
bado ni mfanya biashara mdogo licha ya
kuwa bilionea.Kuna kikao kinafanyika
mara
mbili
kila
mwaka
kinachowakutanisha matajiri mia moja wa
dunia kutoka katika kila kona ya
dunia.Katika kikao hiki mambo mbali
mbali huzungunzwa na nikuibie siri
kwamba kikao hiki kina nguvu kubwa ya
 
SEHEMU YA 64

kufanya maamuzi kuhusiana na uchumi
wa dunia.Ni kikao kizito na hata wakuu wa
nchi nyingi hasa zile tajiri huwa
wanakuwa makini sana na maamuzi ya
kikao hiki kwa hiyo nataka siku moja na
wewe ushiriki kwani katika ukanda huu
wa afrika mashariki kati na kusini hakuna
mtu mwingine anayeingia katika kikao
hicho zaidi yangu.Kwa afrika tuko watatu
tu mimi na raia wengine wawili wa kutoka
Nigeria.” Akasema David Zumo
“ Dah ! Mwili umenisisimka sana kwa
maelezo hayo.Sikuwa nikilifahamu jambo
hilo na nItashukuru sana kama
ukiniwezesha niweze kuwa na sifa za
kuingia katika kikao hicho cha matajiri
wakubwa
duniani.”
Akasema
Benedict.David Zumo akavuta mkupuo
mmoja mkubwa akatabasamu halafu
akatazama juu na kupuliza moshi mwingi
kisha akasema
“ Kuingia katika kikao hii cha
matajiri wakubwa mia moja wa dunia si
kitu rahisi.Unatakiwa uwe tajiri
kwelikweli na kuna kamati ya
kukutathmini kama una vigezo .Ni jambo
kubwa lakini endapo ukifanikiwa
linakuwa na faida hata kwa nchi pia.
Usiogope Benedict mimi nitakuwezesha
utaingia katika kikao hicho kwani mimi ni
namba nne kwa watu matajiri duniani kwa
hiyo niko katika kikao kingine cha watu
kumi ambacho kina nguvu kupita kikao
hiki cha watu mia moja.Watu hao kumi
ndio tunaoamua tuzungumze mambo gani
au tufanye nini na wapi.Nitakuwezesha
Benedict utashuhudia mwenyewe namna
mambo yanavyoendeshwa katika hii dunia
na ukiingia katika kikao hicho utaona kule
ulikotoka ulikuwa kama wale vijana
wanaozunguka na bidhaa zao mitaani
wakizitembeza hapa Tanzania kuna jina
mnawaita”
“ wanaitwa Machinga”
“ Sawa kabisa utajiona kama vile
nawe ulikuwa Machinga” akasema David
na wote wakaangua kicheko.David
akawasha sigara nyingine na kupiga
mkupuo mrefu akapuliza moshi mwingi na
kumtazama mzee Benedict ambaye
alikosa kitu cha kuongea kwa furaha
kubwa aliyokuwa nayo.
“Benedict,kama
nilivyokueleza
kwamba uwezo wa kukuingiza katika
orodha ya watu mia moja matajiri duniani
ninao lakini kuna jambo ambalo
nitalihitaji toka kwako na ambalo nina
imani liko ndani ya uwezo wako kwa hiyo
kama ukikubaliana nami basi jihesabu
kuwa ndani ya muda mfupi utapaa na
kuingia katika orodha ya matajiri wa
dunia” akasema David huku akitabasamu
“ Ni jambo gani hilo mhesimiwa rais?
Niambie na ninakuhakikishia kwamba
nitalitekeleza kwa nguvu sana” akasema
Benedict
“ Vizuri sana.” Akajibu David Zumo
na kuvuta mikupuo kadhaa ya sigara
halafu akanywa funda moja la kinywaji
kisha akasema
“ Benedict ni jambo rahisi tu kwako
na sina hakika kama litakuwa na ugumu
wowote.Ninahitaji kumuoa mwanao
Monica”
Sura ya mzee Benedict Mwamsole
haikuweza kuzuia kuuficha mstuko
alioupata.David Zumo akamtazama na
kutabasamu kisha akasema
“ Monica ni mwanao na nina imani
una uwezo wa kumshawishi akakubali
ombi langu la kutaka kumuoa.Kutoka
moyoni mwangu napenda kukuhakikishia
kwamba ninampenda sana Monica kuliko
mwanamke yeyote niliyewahi kumpenda
chini ya jua. Ninataka awe mke wangu na
nitamfanyia mambo makubwa sana
ambayo hakutegemea kufanyiwa hapa
duniani.Nitamfanya kuwa malkia wa kweli
wa afrika .Naomba sana mzee wangu
unikubalie jambo hili na umshawishi
mwanao akubaliane na ombi
langu.Endapo jambo hili likifanikiwa
nakuahidi kwamba nitakuwezesha kwa
kiasi ambacho hukukitegemea na
nitakufanya mmoja wa watu wakubwa
afrika na dunia.Utavuma kila kona ya
dunia kwa utajiri.” Akasema David na
kuvuta sigara yake.Bado Benedict alikuwa
kimya
 
SEHEMU YA 65

Benedict hilo nililoliomba ni jambo
kubwa kwako? Liko nje ya uwezo wako?
Akauliza David baada ya kuona mzee
Benedict amekuwa kimya
“ Hapana mheshimiwa rais,hili si
jambo kubwa kwangu na liko ndani ya
uweo
wangu.Ninaweza
kumshawishi
Monica akubaliane na ombi lako na
ninataka kukuhakikishia kwamba hawezi
kukataa lakini .....”
“ Lakini nini? Akauliza David Zumo
“ Lakini wewe tayari una mke
mheshimiwa
rais”
akasema
Benedict.David akanywa funda moja la
mvinyo na kusema
“ Ni kweli nina mke lakini kwa ajili
ya Monica niko tayari kwa lolote.Mke
niliyenaye mpaka sasa hatujabahatika
kupata mtoto kwani hawezi kushika
mimba.Nina mali nyingi sana na mpaka
sasa sina mrithi.Ninataka nimuoe Monica
ili anizalie mtoto,tutengeneze familia
.Nimekwishaongea na mke wangu juu ya
jambo hilo na tumekubaliana kwamba
nikimpata
mwanamke
ambaye
nitapendezwa naye basi nizae naye na
kumpata mrithi wangu tatizo lilikuwa
kumpata huyo mwanamke .Huu ni mwaka
wa nne ninajaribu kutafuta mwanamke
ambaye atanigusa moyo wangu lakini
sijafanikiwa hadi nilipompata Monica
ambaye ameigusa sakafu ya moyo
wangu.Tafadhali Benedict naomba sana
ufanikishe hilo jambo.Nataka niwe
mwanaume mwenye furaha nikiwa na
Monica.” Akasema David Zumo
“ Mheshmiwa rais nakuomba ondoa
wasi wasi kabisa jambo hili litawezekana
na
Monica
atakubali
kuolewa
nawe.Nadhani hii ni mipango ya Mungu
kwani kwa muda mrefu sasa tumekuwa
tukijiuliza ni lini Monica atatutambulisha
mchumba wake. Amekuwa akitafuta
mchumba ambaye atamfaa na sasa Mungu
amemjibu na amemletea mtu ambaye
alikuwa
anamsubiri
kwa
miaka
mingi.Mheshimiwa rais ,naamini Monica
aliumbwa kwa ajili yako.Wewe ndiye hasa
mwanaume wa ndoto zake ,Yule ambaye
amekuwa anakusubiri .Nina hakika hata
yeye
mwenyewe
atafurahi
sana
atakaposikia taarifa hizi.” Akasema mzee
benedict na kumfanya David Zumo atoe
tabasamu kubwa.Wakagoganisha glasi
kwa furaha.
**************
Monica na mama yake waliwasili St
Lucia hospital na moja kwa moja
wakaelekea katika chumba cha upasuaji
ambako
Dr
Marcelo
alikuwa
amekimbizwa.Nje ya chumba cha upasuaji
walikuwepo watu kadhaa miongoni mwao
alikuwepo Daniel.
“ Daniel anaendeleaje Dr Marcelo?
Akauliza Monicca
“ Hali yake bado si nzuri ameingizwa
katika chumba cha upasuaji kwa hiyo
tusubiri taarifa za madaktari.”
Monica
akashindwa
kujizuia
machozi kumtoka
“ Monica please don’t cry.We need to
be strong for him” akasema Daniel
“ Inaniuma sana Daniel.Jioni ya leo
nimekutana naye tukaongea mambo
Fulani na nikamueleza kwamba nina wasi
wasi na usalama wake nikamkaribisha
akaishi
nyumbani
kwangu
lakini
akakataa.Ni kama vile nilihisi jambo baya
lingeweza kumtokea” Akasema Monica na
machozi yakaendelea kumtoka
“ Nani aliyefanya kitendo hiki?
Akauliza Monica
“ Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote
iliyotolewa na polisi wanaendelea na
uchunguzi wao juu ya tukio hili.” Akasema
Daniel halafu akamshika mkono Monica
 
SEHEMU YA 66


akaenda kumtambulisha kwa ndugu za Dr
Marcelo waliokuwa wamekaa kwa huzuni
nje ya chumba cha upasuaji.Monica na
mama yake wakawafariji na kuungana nao
kusubiri
upasuaji
umalizike.Kila
aliyekuwapo pale alionekana kuwa na
sura ya wasi wasi mkubwa.Kadiri muda
ulivyozidi kusonga ndivyo idadi ya watu
ilivyozidi kuongezeka kwani Dr Marcelo ni
mmoja wa watu waliokuwa wanafahamika
na kupendwa sana na watu wengi.
“ Dr Marcelo ni mmoja wa marafiki
zangu wakubwa na wa muda mrefu.Toka
tulipokutana
tumekuwa
marafiki
wakubwa,tumeheshimiana na hata siku
moja haijawahi kutokea tukapishana
kauli.Kila mmoja alimfahamu vizuri
mwenzake akayafahamu madhaifu yake
na hiyo ndiyo iliyotuwezesha tukawa
marafiki wakubwa.Ni mara ya kwanza
imetokea tukapishana kauli na ninakijutia
sana kitendo kile.Kinachoniuma sana,right
now Marcelo is fighting for his life and I
don’t have time to say I’m sorry.Inaniuma
sana.Sikutaka urafiki wetu uishe namna
hii” akasema Daniel na akashindwa
kujizuia machozi kumtoka
“ All its because of me.Mimi ndiye
niliyekuja kuuvuruga urafiki wenu na
kuwapelekea
mkakorofishana
hadi
kufikia hatua ya kutoleana maneno
machafu.I’m so sorry Daniel.” Akasema
Monica

Usijilaumu
Monica.Sisi
sote
tumefanya
makosa.Tunachotakiwa
kufanya hivi sasa ni kumuombea Marcelo
ili aweze kupona” akasema Daniel
Saa saba na dakika ishirini Dr
Marcelo akatolewa katika chumba cha
upasuaji na kupelekwa katika chumba cha
wagonjwa walioko katika hali ya
hatari.Daktari akawaita baadhi ya ndugu
wa Marcelo ofisini kwake akawafahamisha
kwamba upasuaji umefanyika vizuri na
kwa mafanikio lakini bado mgonjwa
alikuwa hajatolewa katika hali ya hatari
“ Can we see him? Akauliza Julieth
dada yake
“ Hata mkimuona kwa sasa hawezi
kuongea bado yuko katika usingizi”
akasema daktari
“ Daktari tunaomba turuhusiwe
kuingia kumuona ndugu yetu ili tuwe na
uhakika kama bado yuko hai ama vipi.”
Akaomba Daniel ambaye naye alikuwemo
miongoni mwa watu walioingia ofisini kwa
daktari kupewa maelezo ya kuhusu hali ya
Dr Marcelo.Familia ya Dr Marcelo
inamfahamu
sana
Daniel
na
wanamchukulia ni kama ndugu yao
kutokana na ukaribu mkubwa alionao na
Dr Marcelo.
Baada ya kuomba sana daktari
akawaruhusu waingie watu watano katika
chumba alichokuwa amelazwa Dr Marcelo
lakini
wakiwa
wamevaa
mavazi
maalumu.Haraka haraka wakajichagua
watu watano na miongoni mwao
walikuwemo
Daniel
na
Monica.Wakavalishwa mavazi maalum
wakaingia ndani ya chumba alimolazwa
Dr Marcelo.Kulikuwa na mashine mbali
mbali zilizokuwa zimeunganishwa katika
mwili wa Dr Marcelo aliyekuwa amelala
kitandani hana fahamu.

I’m
so
sorry
Dr
Marcelo.Sikutegemea kabisa kama siku
moja ungeweza kulala hapo kitandani
namna hii huna fahamu ukipigania maisha
yako.Please Marcelo fight for your life
because we still need and love you.You
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom