Qatar: Nchi inayomiliki rasilimali zake

Princemwalejr

JF-Expert Member
Nov 9, 2017
496
488
WANASEMA ni nchi ya mfalme na mwanawe. Hawapotezi muda kwenye malumbano ya siasa!

QATAR ilipata uhuru mwaka 1971 kutoka kwa mwingereza. Ni nchi inayoongozwa na mfalme. Kumbe mambo yasipoenda hata mfalme hutumbuliwa. Alianza Ahmad Al Thani baada ya uhuru. Mwaka 1972 alipinduliwa na mjomba wake Khalifa Al Thani. Huyu alipinduliwa na mwanawe prince Hamad Al Thani mnamo mwaka 1995. Prince Hamad aliachia madaraka kwa Tamim Hamad Al Thani mnamo mwaka 2013. Ukoo huo wa Al Thani hauruhusu ukoo mwingine kuchukua madaraka na hakuna chama cha siasa hata kimoja. Baraza la mawaziri huchaguliwa na kutumbuliwa wakati wowote mfalme akiamua.

UCHUMI wa Qatar unategemea mafuta. Kampuni ya serikali ya Qatar Petroleum (QP) inasimamia utafiti, uchimbaji, usafishaji, usafirishaji na kuhifadhi mafuta. Mwenyekiti wa kampuni hiyo pia ni waziri wa nishati na viwanda. Mafuta na gesi vinatoa asilimia 60 ya kipato cha Qatar.

MAISHA ya waqatari yanategemea kipato cha mafuta ya Qatar. Serikali inaweza kuwapa waqatari huduma za maji, afya, mpaka nyumba bila ya malipo. Elimu ni bure. Wanafunzi wanapata chakula shuleni. Wanasafiri bure, hata nguo wanapewa bila ya malipo. Vilevile serikali inalipia wanafunzi wasomao nje ya nchi. Kuna habari kutoka kwa wenyeji kuwa mqatari hata akiwa hana kazi analipwa mshahara kila mwezi.

ZOEZI hilo linawawezesha waqatari kuachia wageni kazi nyingi huku wenyewe wakiwa wanashikilia nyadhifa muhimu hasa kwenye kazi za serikali. Waafrika hasa kutoka Misri, waasia, wazungu ni katika orodha kubwa ya wafanyakazi wa kigeni nchini humo. Wakenya wanajiona tamu sana Doha airport, kama vile wako Nairobi. Waajiri ni wakali kwenye mikataba na kubana wafanyakazi hasa kwenye masuala ya kubadilisha kazi.

UTAIFISHAJI wa mafuta ulifanywa kwa awamu. Mafuta yaligunduliwa kwenye miaka ya 1950. Mwanzoni mafuta yalimilikiwa na kampuni ya British Petroleum (BP) na baadhi ya makampuni ya Iran. Wakati huo serikali ilikuwa ikimiliki asilimia 25, huku hisa zikiongezeka kidogo kidogo kila mwaka. Kufikia mwaka 1975 serikali ilishavunja mikataba ya awali. (kwa staili ile ya Acacia) Na kuanzia mwaka 1976 kampuni ya Qatar Petroleum imekuwa ikimiliki mafuta ya Qatar kwa ASILIMIA 100. Sambamba na utaifishaji huo vituo vya kuuzia mafuta, teksi, mabasi na treni vinamilikiwa na serikali. Uber na teksi bubu zipo lakini ni marufuku kufika maeneo muhimu kama uwanja wa ndege.

UTALIPENDA jengo la makao makuu ya kampuni ya QP. Ni mnara mrefu sana wa bluu uliopanda ki-New York. Chini kuna kama tufe kubwa lenye maandishi ya Qatar Petroleum na juu ya gorofa hilo kuna kibaraza kinachozunguka usiku huku kikiwa na maandishi ya bluu yanayosomeka QATAR PETROLEUM, ikiwa ni uthibitisho tosha kuwa kinachoendelea ndani ya jengo hilo ni mafuta ya Qatar tu.

SHIRIKA la ndege la Qatar pia linamilikiwa na serikali. Lina ndege kubwa za aina ya Boeing na Airbus zaidi ya 320. Ni ndege mpya za kisasa nyingine zina uwezo wa kuweka na kuondoa kivuli kwenye madirisha. Qatar hawana vivutio vingi vya utalii lakini ndege hizi hubeba watalii wengi waendao Afrika ya mashariki. Wanajaza ndege ya watalii kutoka Doha mpaka Kilimanjaro, halafu wanawarudisha kutoka Kilimanjaro kwenda Doha kwa kupitia Dar-es-salaam. ATCL wajipange vizuri na mtihani huu. Vilevile huduma za shirika hili ni nzuri sana. Achana na mashirika ya ndege za wazungu wanabania chakula. Qatar airways wanakupa mpaka chapati.

MIPANGO miji ya Qatar ni ya kukata na shoka. Si Ulaya si Marekani wanaowafikia. Waarabu hawa wana taa za barabarani zenye mwanga wa maua kwenye mlingoti mzima wa taa. Hakuna mashimo barabarani, na wana magari ya kifahari mno. Sio city kama Tanga ni Metropole. Wana masoko na maduka ya kisasa likiwemo lile wanaloliita Villagio. Juu ya soko hili wamechora rangi ya mawingu inayofanya mtu akiwa ndani aone kama anatembea nje. Mjengo wa aina hii hupatikana sehemu chache duniani ikiwemo Las Vegas, Johannesburg na Macau. Mahoteli yao ni ya kimataifa na ya hadhi za juu.

UWANJA wa ndege wa Doha ni mkubwa, unavutia na wa kisasa. Umbali wa kutokea temino mpaka kwenye ndege kuna mama wa kizungu aliuliza kama safari ni ya basi au ya ndege. Boeing tano au sita za Qatar zinaweza kujipanga mstari zikisubiri zamu ya kuruka. Inawezekana ni uchache wa ardhi lakini huu uwanja huu umejengwa kwa kufukia mchanga baharini.

HALI ya hewa si nzuri kama ya Tanzania. Waqatari wako jangwani. Joto la nyuzi 108 f, 44 (c) ni kawaida wakati wa majira ya joto. Ukitaka upate uhalisia wake ingiza kichwa kwenye oven. Lakini wanalimudu joto hili. Nyumba zao hata kwenye masoko kuna mizizimo ya viyoyozi usawa wa winter kali.

KILIMO kimewatupa mkono kutokana na kuwa jangwani. Wana mashamba machache ya ngano na tende. Lakini hakuna wanachokosa. Ukitaka kujua tofauti ya nyama za plastiki za MacDonald na nyama ya ukweli agizia mpunga na nyama Doha. Halafu kakae bichi ule biriani yao hawa jamaa.

WENYEJI ni waislamu na mavazi ya kiislamu yametawala barabarani. Misikiti huanz kuadhini saa tisa za usiku. Hawana uislamu ule wa kushikana mashati. Wageni wanachotakiwa ni kuzingatia sheria za msingi za nchi. Kwenye ndege zao na maduka yao hasa ya uwanja wa ndege wanauza pombe tena hata zike kali. Hata hivyo ndani ya ndege zao una chaguo la kusikiliza Quran badala ya kuangalia movie au vipindi vya televisheni. Vibaka barabarani wala hofu ya kutapeliwa hakuna.

MAJAHAZI ya kizamani yale ni kivutio kikubwa baharini. Usiku yanawaka mataa na kutembeza watalii baharini kwa malipo. Muziki mororo ndani ya majahazi. Kukiwa na dj wa kikenya atapiga sana nyimbo za Diamond.

WANA mafuta na jangwa tu. Hah!hawana mlima Kilimanjaro, hawana Serengeti, hawana Ngorongoro, hawana Olduvai gorge, hawana Tanzanite, hawana dhahabu, hawana almasi, hawana mito, maziwa na mabonde. Hawana mvua za uhakika, hawana kahawa, hawana korosho, hawana kitu tuseme.

PENGINE walianza maendeleo zamani. La hasha, Qatar ni nchi changa kuliko nchi nyingi za Afrika. Ilipata uhuru mwaka 1971. Picha za Doha ya 1970 na picha ya Doha ya leo, tofauti yake ni kama usiku na mchana.

KUBWA walilolifanya ni kumiliki kikamilifu rasilimali yao moja waliyopewa na Mungu.

Tembea ujifunze!

IMG_9723.JPG
IMG_9700.JPG
IMG_9719.JPG
IMG_9727.JPG
IMG_9716.JPG
IMG_9717.JPG
IMG_9718.JPG
IMG_9721.JPG
IMG_9722.JPG
IMG_9659.JPG
IMG_9643.JPG
IMG_9705.JPG
IMG_9702.JPG
IMG_9703.JPG
i
IMG_9704.JPG
 
Doha ni jiji zuri limejengwa vizuri lina Gardens nyingi na nzuri sana. Kitu ambacho sikukipenda barabara zao ni nyembamba kidogo, nyingi japo si high ways hazina sehemu za watembea kwa miguu halafu miezi ya May to September joto lao si la kawaida. Kuna Wakenya wengi sana wanaofurahia kuishi Doha. Bado wamewekewa vikwazo vya kiuchumi na Saudi Arabia, UAE, Bahrain na Egypt vikwazo ambavyo havina athari kubwa kwao hadi sasa kutokana na kutumia vizuri utajiri wao.
 
There is something about these cities that rubs me the wrong way.
 
WANASEMA ni nchi ya mfalme na mwanawe. Hawapotezi muda kwenye malumbano ya siasa!

QATAR ilipata uhuru mwaka 1971 kutoka kwa mwingereza. Ni nchi inayoongozwa na mfalme. Kumbe mambo yasipoenda hata mfalme hutumbuliwa. Alianza Ahmad Al Thani baada ya uhuru. Mwaka 1972 alipinduliwa na mjomba wake Khalifa Al Thani. Huyu alipinduliwa na mwanawe prince Hamad Al Thani mnamo mwaka 1995. Prince Hamad aliachia madaraka kwa Tamim Hamad Al Thani mnamo mwaka 2013. Ukoo huo wa Al Thani hauruhusu ukoo mwingine kuchukua madaraka na hakuna chama cha siasa hata kimoja. Baraza la mawaziri huchaguliwa na kutumbuliwa wakati wowote mfalme akiamua.

UCHUMI wa Qatar unategemea mafuta. Kampuni ya serikali ya Qatar Petroleum (QP) inasimamia utafiti, uchimbaji, usafishaji, usafirishaji na kuhifadhi mafuta. Mwenyekiti wa kampuni hiyo pia ni waziri wa nishati na viwanda. Mafuta na gesi vinatoa asilimia 60 ya kipato cha Qatar.

MAISHA ya waqatari yanategemea kipato cha mafuta ya Qatar. Serikali inaweza kuwapa waqatari huduma za maji, afya, mpaka nyumba bila ya malipo. Elimu ni bure. Wanafunzi wanapata chakula shuleni. Wanasafiri bure, hata nguo wanapewa bila ya malipo. Vilevile serikali inalipia wanafunzi wasomao nje ya nchi. Kuna habari kutoka kwa wenyeji kuwa mqatari hata akiwa hana kazi analipwa mshahara kila mwezi.

ZOEZI hilo linawawezesha waqatari kuachia wageni kazi nyingi huku wenyewe wakiwa wanashikilia nyadhifa muhimu hasa kwenye kazi za serikali. Waafrika hasa kutoka Misri, waasia, wazungu ni katika orodha kubwa ya wafanyakazi wa kigeni nchini humo. Wakenya wanajiona tamu sana Doha airport, kama vile wako Nairobi. Waajiri ni wakali kwenye mikataba na kubana wafanyakazi hasa kwenye masuala ya kubadilisha kazi.

UTAIFISHAJI wa mafuta ulifanywa kwa awamu. Mafuta yaligunduliwa kwenye miaka ya 1950. Mwanzoni mafuta yalimilikiwa na kampuni ya British Petroleum (BP) na baadhi ya makampuni ya Iran. Wakati huo serikali ilikuwa ikimiliki asilimia 25, huku hisa zikiongezeka kidogo kidogo kila mwaka. Kufikia mwaka 1975 serikali ilishavunja mikataba ya awali. (kwa staili ile ya Acacia) Na kuanzia mwaka 1976 kampuni ya Qatar Petroleum imekuwa ikimiliki mafuta ya Qatar kwa ASILIMIA 100. Sambamba na utaifishaji huo vituo vya kuuzia mafuta, teksi, mabasi na treni vinamilikiwa na serikali. Uber na teksi bubu zipo lakini ni marufuku kufika maeneo muhimu kama uwanja wa ndege.

UTALIPENDA jengo la makao makuu ya kampuni ya QP. Ni mnara mrefu sana wa bluu uliopanda ki-New York. Chini kuna kama tufe kubwa lenye maandishi ya Qatar Petroleum na juu ya gorofa hilo kuna kibaraza kinachozunguka usiku huku kikiwa na maandishi ya bluu yanayosomeka QATAR PETROLEUM, ikiwa ni uthibitisho tosha kuwa kinachoendelea ndani ya jengo hilo ni mafuta ya Qatar tu.

SHIRIKA la ndege la Qatar pia linamilikiwa na serikali. Lina ndege kubwa za aina ya Boeing na Airbus zaidi ya 320. Ni ndege mpya za kisasa nyingine zina uwezo wa kuweka na kuondoa kivuli kwenye madirisha. Qatar hawana vivutio vingi vya utalii lakini ndege hizi hubeba watalii wengi waendao Afrika ya mashariki. Wanajaza ndege ya watalii kutoka Doha mpaka Kilimanjaro, halafu wanawarudisha kutoka Kilimanjaro kwenda Doha kwa kupitia Dar-es-salaam. ATCL wajipange vizuri na mtihani huu. Vilevile huduma za shirika hili ni nzuri sana. Achana na mashirika ya ndege za wazungu wanabania chakula. Qatar airways wanakupa mpaka chapati.

MIPANGO miji ya Qatar ni ya kukata na shoka. Si Ulaya si Marekani wanaowafikia. Waarabu hawa wana taa za barabarani zenye mwanga wa maua kwenye mlingoti mzima wa taa. Hakuna mashimo barabarani, na wana magari ya kifahari mno. Sio city kama Tanga ni Metropole. Wana masoko na maduka ya kisasa likiwemo lile wanaloliita Villagio. Juu ya soko hili wamechora rangi ya mawingu inayofanya mtu akiwa ndani aone kama anatembea nje. Mjengo wa aina hii hupatikana sehemu chache duniani ikiwemo Las Vegas, Johannesburg na Macau. Mahoteli yao ni ya kimataifa na ya hadhi za juu.

UWANJA wa ndege wa Doha ni mkubwa, unavutia na wa kisasa. Umbali wa kutokea temino mpaka kwenye ndege kuna mama wa kizungu aliuliza kama safari ni ya basi au ya ndege. Boeing tano au sita za Qatar zinaweza kujipanga mstari zikisubiri zamu ya kuruka. Inawezekana ni uchache wa ardhi lakini huu uwanja huu umejengwa kwa kufukia mchanga baharini.

HALI ya hewa si nzuri kama ya Tanzania. Waqatari wako jangwani. Joto la nyuzi 108 f, 44 (c) ni kawaida wakati wa majira ya joto. Ukitaka upate uhalisia wake ingiza kichwa kwenye oven. Lakini wanalimudu joto hili. Nyumba zao hata kwenye masoko kuna mizizimo ya viyoyozi usawa wa winter kali.

KILIMO kimewatupa mkono kutokana na kuwa jangwani. Wana mashamba machache ya ngano na tende. Lakini hakuna wanachokosa. Ukitaka kujua tofauti ya nyama za plastiki za MacDonald na nyama ya ukweli agizia mpunga na nyama Doha. Halafu kakae bichi ule biriani yao hawa jamaa.

WENYEJI ni waislamu na mavazi ya kiislamu yametawala barabarani. Misikiti huanz kuadhini saa tisa za usiku. Hawana uislamu ule wa kushikana mashati. Wageni wanachotakiwa ni kuzingatia sheria za msingi za nchi. Kwenye ndege zao na maduka yao hasa ya uwanja wa ndege wanauza pombe tena hata zike kali. Hata hivyo ndani ya ndege zao una chaguo la kusikiliza Quran badala ya kuangalia movie au vipindi vya televisheni. Vibaka barabarani wala hofu ya kutapeliwa hakuna.

MAJAHAZI ya kizamani yale ni kivutio kikubwa baharini. Usiku yanawaka mataa na kutembeza watalii baharini kwa malipo. Muziki mororo ndani ya majahazi. Kukiwa na dj wa kikenya atapiga sana nyimbo za Diamond.

WANA mafuta na jangwa tu. Hah!hawana mlima Kilimanjaro, hawana Serengeti, hawana Ngorongoro, hawana Olduvai gorge, hawana Tanzanite, hawana dhahabu, hawana almasi, hawana mito, maziwa na mabonde. Hawana mvua za uhakika, hawana kahawa, hawana korosho, hawana kitu tuseme.

PENGINE walianza maendeleo zamani. La hasha, Qatar ni nchi changa kuliko nchi nyingi za Afrika. Ilipata uhuru mwaka 1971. Picha za Doha ya 1970 na picha ya Doha ya leo, tofauti yake ni kama usiku na mchana.

KUBWA walilolifanya ni kumiliki kikamilifu rasilimali yao moja waliyopewa na Mungu.

Tembea ujifunze!

View attachment 1148746View attachment 1148747View attachment 1148748View attachment 1148749View attachment 1148750View attachment 1148751View attachment 1148752View attachment 1148753View attachment 1148754View attachment 1148755View attachment 1148756View attachment 1148757View attachment 1148758View attachment 1148759iView attachment 1148760
Hizi nchi zote za Mashariki ya Kati zimshukuru Marekani kwasababu ndio mgunduzi wa Kwanza kwa matumizi ya mafuta halafu pia ndio mtumiaji na mnunuzi mkubwa zaidi. Bila mafuta au utajiri wa Marekani wangekuwa masikini
 
Nawakubali sana Qatar Aiways kwenye huduma zao ndani ya ndege kulinganisha na mashirika mengi ya ndege duniani.Kusema ATCL ajipange ni kwamba hataweza, hawa jamaa kwenye huduma wameshika number1 duniani mara nyingi.
Wajinga hawa siwapendiiii nawachukiaa, mwaka jana nilipata bahati ya kwenda London walipotezea luggage zangu na walivyo na customer care mbovu dunia nzima baada ya miezi sita wakaniambia niwe mvumilivu mpaka leo sijapata.

Kuna lingine ndio hadi nilitaka kuuwa mtu ilikuwa flight ya masaa 13 yakawa 22
 
Back
Top Bottom