tatum
JF-Expert Member
- Jan 16, 2018
- 5,786
- 4,490
Hapo ni Ruvu mbogamboga zikiharibiwa kwasababu zipo ndani ya mita 60 kutoka mtoni kwa amri ya Bodi ya maji bonde la Wami na Ruvu.
BODI YA MAJI YAFYEKA MAZAO YA WAKULIMA MTO RUVU
Bodi ya Maji Bonde la Wami/ Ruvu imefika na kufyeka mazao mbalimbali yaliyolimwa pembezoni mwa Mto Ruvu na ndani ya Mita 60 kutoka kwenye mto huo katika eneo la Ruvu Darajaji mkoani Pwani.
Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu, Simon Ngonyani amesema kuwa zoezi hilo ni muendelezo wa operation ya kuwaondoa watu wanaofanya shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo na kujenga makazi yao ndani ya Mita 60 kutoka Mto huo ili kulinda chanzo hicho cha maji.
"Sasahivi maji yamepungua katika Mto huu nilikuwa naongea na ndugu yangu CEO wa DAWASA aliniambia kwamba mitambo yake sasa inaungua kwasababu kina cha maji kimepungua sana na maji yanapungua kwasababu watu wanalima hivyo michanga inaingia kwenye mto kina kinapingua" -Ngonyani.
Aidha amesema kuwa kutokana na wakulima hao wanaolima kando ya Mto kwa kutumia mbolea za chumvi chumvi kunapelekea usalama wa maji hayo kupotea kwa watumiaji hivyo watu wafuate sheria ili kulinda maji ya Mto huo.
"Tumeamua kusimamia sheria hatutawabakisha, leo tunafyeka mazao yote yaliyopo ndani ya Mita 60 lakini kinachofuatia nyumba ambazo zipo ndani ya Mita 60 zenyewe pia tutazifanyia kazi"- Ngonyani.
Habari zaidi, soma=>Kyaka, Kagera: Rais awapiga marufuku viongozi wanaowazuia wananchi kulima kandokando ya mito - JamiiForums
UPDATES:
Siku nne zimepita tangu Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu kufyeka mazao yaliyolimwa na Watanzania Mbalimbali pembezoni mwa mto Ruvu.
Afisa wa Maji, Simoni Ngonyani amefafanua hatua hiyo kwamba walifanya jitihada za kutosha kwa kutoa elimu, kuweka mabango na kukubaliana na wakulima wenyewe juu ya kusitisha shughuli ya kulima mazao kwenye Bonde hilo.
Hata hivyo Bodi inaendelea kutoa elimu na kuchukua hatua dhidi ya watu wote wanaovamia vyanzo vya maji na kutumia maji ya mito pasipo vibali.