Duuu hii hali inatisha, Poleni sana wafiwa kwa masaibu hayo ambayo binadamu yoyote kwenye akili timamu na hofu ya Mungu hawezi tenda.
Nimefuatilia mijadala huku ndani maana nilikuwa sijui na najiuliza kwanini haya yatokee na ukimya na usiri mkubwa huu wa kutojulikana wahalifu? Kuna vitu Vingi sana vinatajwa na watu na wengine wanasema huenda serikali inajua ukweli wake ila haitaki kuusema maana ni kama msemo ule usemao, "Jini ulilifuga mwenyewe liwadhuru wengine sasa linakurudia"
Sasa swali LA kujiuliza kwanini hali hii mpaka sasa, je, ukweli kila siku kuhesabu idadi ya waliouawa ni sawa? Poleni sana sana Kibiti, Mkuranga & Rufiji. Je, haya yanayosemwa kuna ukweli wowote?
HYPOTHESIS zilizopo kwa mijadala ya humu ndani.
(1)Haya yanayotokea ni kutokana na dhuluma kwa wananchi kupigwa na kuteswa na viongozi wa huko kwa ishu za kiuchumi za mazao ya misitu, yasni Mbao, Mkaa, Kuni na kulima kwenye misitu hiyo, sasa baadae ya kuzuiwa wamekosa shughuli za kiuchumi hivyo hasira kurudi kwa viongozi wasimamizi wa maeneo hayo.
(2)Huenda yanatokana na kubanwa kupitisha nyara za serikali kama Magogo na Vipusa (pembe za ndovu), maana inasemekana kutokana na misitu ya huko sasa wale majangili ndo ilikuwa njia yao rahisi kupita, sasa wamebanwa na waneona warudishe hasira zao kwa hao wasimamizi?
(3)Huenda ni kutokana na nadharia ya kuwa mikoa ya kusini kusahaulika katika rasilimali za nchi, hawafaidiki kwa chochote na haya ishu ya bomba LA gesi na umeme kanda hiyo ilipata msukosuko sana, waliteswa na kupigwa walipotaka kuleta upinzani gesi isitoke kwanza kabla hawajafaidika. Maana ukweli tulisoma na kuona kwenye vyombo vya habari watu wa kanda hiyo kusumbuka, sasa huenda wameona ndo pakutolea hasira, sasa swali tena linakuja, hawa wanaouawa je, ndio wasimamizi wa hiyo gesi na umeme? Inabaki haieleweki.
(4)Huenda ni kutokana na siasa na utofauti na chuki tuuu bila kuwa na uhalisia. Hii nayo inaacha maswali kama ni chuki ya kisiasa, je kanda hiyo ndo wanajua siasa kulikoni maeneo mengine? Mbona maeneo mengi kuna mchanganyiko wa siasa lakini haya hayaonekani?
(5)Huenda ni mambo ya utofauti wa kiimani na nini, hili pia nalo linaacha maswali mengi, mbona maeneo mengi nchini yana mchanganyiko wa imani tifautitofauti na misimamo tofautitofauti mbona haya yanayotokea huko, huko kwingine hayapo? Au wa huko ndo kwenye imani na misimamo mikali tofauti na mahala pengine nchini?
(6)Huenda ni kutokana na tetesi na haya kipindi Fulani cha nyuma iliwahi kusemwasemwa na haya humu jamvini wengine wamewaza hivyo. Kulisemekana kuna makundi ya vijana walikuwa wanakusanywa na kusafitishwa nje ya nchi kufundishwa mambo mbalimbali, ila familia zao waliahidiwa kupewa hela na wao pia kulipwa kwa mafunzo hayo. Na inasemekana viongozi wa maeneo ya huko ndo walikuwa na tenda hiyo kukusanya vijana nao pia kufaidika kwa idadi ya aliowarecruit, sasa swali linakuja, makundi kama hayo serikali yetu na wanausalama wetu walilijua? Je, hatua gani zilichukuliwa? Je, hao vijana kwa makundi hayo wanajulikana? Na je, wapo wapi kwa sasa wanafanya nini? Je, viongozi waliohusika kufanya udahili huo wanajulikana?, wapo wapi? Na je, hayo mafunzo yalilenga nini? Nadhani hapa kunaacha maswali mengi sana yasiyo na majibu kwa sisi RAIA, ila serikali na wanausalama lazima wanamajibu.
(7)Huenda ni ugaidi ndo unajijenga nchini, kama ilivyo BokoHaram, Alshaababy mmmh Mungu atuepushie hili, ila nalo linaacha maswali, hao magaidi woote huwa wsnalengo lao na huelezea nini wanataka ili waache dhuluma hiyo, sasa hawa mbona hakuna Maelezo yoyote? Au huenda Mimi ndo sijui, maana kwa kufuatilia media za habari sijaona lolote.
Sasa tuje Hypothesis nyingine hii ya uwezo wao wa kufanya matukio kila Mara na hawakamatwi. Hii inaonesha hao wafanyadhuluma wapo Trained na kwenye siri Kubwa sana, je, watu wa namna hiyo ni RAIA wa kawaida kweli? Je, wanaishi wapi na akina nani bila kujulikana? Je, wenyeji wa maeneo hayo hawana chochote cha kusema ili hili likomeshwe? Je, wananchi kwanini wawafiche wahalifu wanaowasababishia kula na kulala SAA 12jioni kila siku? Je, wanausalama wetu huko wanaushirikiano mzuri na wananchi ili wawape ya ndani wanayojua? Maana wakati mwingine RAIA wema huogopa kusema anachojua maana siri zake zitavuja na anajikuta yupo matatani kwa yule aliyetajwa kuhusika.
Kwa mantiki hii, haya maswali tukijiuliza kwa uzalendo na kuyapatia ufumbuzi unaweza saidia kutuliza na kumaliza tatizo. Binafsi bado ninaimani kwa vyombo vyetu vya usalama, wanaweredi wa kutosha. Na huenda haya niwazayo wanamajibu yao. Kila LA kheri kwa vyombo vyetu vya usalama, na Mungu atusimamie kama nchi kadhia hii iishe kabisa.