Pwani: Askari Polisi agoma kusema CCM oyee. Afukuzwa kwenye mkutano na kiongozi wa CCM, aambiwa atakiona

Ukienda Roma fanya kama wafanyavyo Waroma.
Ukienda kwenye mazishi ya Imani za dini fanya ishara kama wafanyavyo wenye Imani hiyo.
Bora usiende ili kuepuka fedheha kama hutaki wafanyavyo.

Kimaadili ya Kijeshi Askari yuko sawa,kimaadili ya Kichama aliyemfukuza yuko sawa.
Kosa ni kufanya mkutano bila kibali,kwani wangelipewa kibali wangelipewa na masharti ya kuzingatia.
 
Umeangalia hiyo clip au unajibu tu bila kuelewa? Yaani wewe kichwani utakuwa umebeba kamasi.
 
Yaani wewe ni chenga kabisa
 
Kafanyiwa udharirishaji ila kakataa kujidharirisha nadhani hiyo imemjengea heshima zaidi ni mbaya kama angetii na kusema.inaonekana ni askari aliyeiva sana
Yah jamaa amekwiva mafunzo si maskhara...akae vizuri tu maana kinachofata ni kumtafutia zengwe.
 
Ile ya tabia ya kutengeneza tatizo na kisha kulipatia solution tatizo husika,huenda ndio inataka kujitokeza katika tukio la askari huyu aliegoma kusema "chama cha kijani oyeee".

Hivyo,ili kurekebisha makosa ya nyuma na zaidi ili kumpa political mileage bwana mkubwa,askari husika anaweza kupongezwa na hata kuwa promoted ili tu bwana mkubwa aonekane hakubaliani na mambo ya aina hii hivyo mimi binafsi kwa sasa nitajipa muda kabla ya kumpongeza askari husika.

Under this regime,sometimes it is safe/ wise to be pessimistic rather than being optimistic.
 
Linaweza kuwa halijatengenezwa ila jamaa akaamua kupita humohumo,si unaona ishu ya mlipuko na ofa za kutibiwa Bure nk wakati hapo nyuma hata waliokufa njaa waliambiwa wafe tu serikali haina chakula,huku wengine waliambiwa serikali haileti majanga kwahio wapambane na hali zao
 
Yote yanawezeka, hivyo nakubaliana na wewe.
 
Acha ujinga ujinga kaka. Ungejipa muda wa kuitaza hiyo video wala usingeliandika huu ujinga uloandika hapa. Naamini umehadithiwa hujatazama hicho kipande video.
 
Kweli kabisa mkuu.Mshahara wa huyu Polisi unatokana na kodi za wananchi wote,sio wanachama wa ccm pekee.Analipwa kuhudumia wananchi wote,sio ccm pekee.Ndio maana maadili ya kazi yanamkataza kufungamana na siasa.Sasa huyu kada vipi huyu?!
YEHODAYA hebu panda hapo juu ucheki hiyo clip kwanza ujue kinachoendelea kabla hujakimbilia kukomenti tu humu,unaniaibisha ndugu yangu,hivi uvccm mmekumbwa na mihemko ya wapi,mbona mnatuaibisha vijana wenzenu hivi jamani,jamani,jamaaani,ah!
 
Acha ujinga ujinga kaka. Ungejipa muda wa kuitaza hiyo video wala usingeliandika huu ujinga uloandika hapa. Naamini umehadithiwa hujatazama hicho kipande video.
Clip iko wazi kabisa kakataa kujibu swali kwa kisingizio Cha chama!!!! Wakati swali la kikazi
 
ASKARI POLISI Agoma Kusema CCM Oyee | Afukuzwa Mkutanoni na Kiongozi wa CCM

Ifike mahali Askari wetu nao wajitambue! Kwenye mkutano wa ccm alienda Kama Nani na alienda kufanya nini! Kama alienda kwa ajiri ya ulinzi wa mkutano kazi yake kubwa ingekuwa ulinzi na kama alienda kutoa elimu ya ulinzi angetoa elimu ya ulinzi
 
Ifike mahali Askari wetu nao wajitambue! Kwenye mkutano wa ccm alienda Kama Nani na alienda kufanya nini! Kama alienda kwa ajiri ya ulinzi wa mkutano kazi yake kubwa ingekuwa ulinzi na kama alienda kutoa elimu ya ulinzi angetoa elimu ya ulinzi
Siyo ule Ni.mkutano wa wananchi waweza omba ufafanuzi wowote toka kwake Kama mkuu wa kituo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…