Pwani: Askari Polisi agoma kusema CCM oyee. Afukuzwa kwenye mkutano na kiongozi wa CCM, aambiwa atakiona

angalia nyuma hapo ni kituo cha polisi wako kwa nje
Wamejipeleka wenyewe hapo walipo kama wangekua wanatenda haki hakuna ambae angewaona si chochote. Ila matendo yao yamewafanya wafanyakazi wa CCM kuona kama ni tawi lao.
 
Huyu kijani anacheza na chatu shingoni.Hao askari mmezoea kuwaburuza hadi mnaanza kuwanyanyasa hivi?!Aisee nawatahadharisha CCM endeleeni kutuchezea raia ila sio askari,mtakuja shangaa kitachotokea just overnight,na askari hawasalitiani,akili zao kama sisimizi,umoja ni mafunzo yao na code ya kazi,huku mlikofika mbali aisee!yaani kijana mdogo huna uoga na crown kisa umevaa nguo ya chama cha kisiasa?awamu ya tano mnawatoa wapi walevi wa kisiasa hawa?mbona ccm haikuwa hivi?!nimechukizwa sana kuona mlinzi wetu anafanyiwa maskhara ya ulevi wa kisiasa hivi.Anyway,endeleeni na maskhara yenu,mnachokitafuta mtakipata,vinginevyo Polepole toa tamko kulaani huu ulevi wa kisiasa na huyu mlevi mumchukulie hatua.
Hakuna watu wabaya kama askari

Hasa wakiona mambo hayaendi sawa ni dakika mbili tuu
 
Kwani hawa viongozi wa CCM awamu hii walipikwa wapi? Mbona wanafanya mambo ya aibu kiasi hiki?

Kiongozi wa chama anamlazimisha Police akiuke sheria na kanuni za kazi?

Hawa sasa wameshindwa kwa hoja wanahangaika kuwaonesha wapinzani kwamba hata hawa polisi ni wetu. Aibu!

Pongezi kwa askari kwa kusimamia maadili ya kazi yake.

Halafu sijui ni nani amawajaza hawa watu ujinga kwamba CCM ndiyo inayolipa watumishi mishahara.
Napenda unavyoandika kiongozi

Doooh
 
August 15, 2019
Vianzi, Mkuranga
Pwani, Tanzania

Katika ziara ya mjumbe wa wa Halmashauri Kuu ya CCM NEC Bw. Haji Abuu Jumaa mkoani Pwani Tanzania Bara, Askari wa Jeshi la Polisi alipoombwa kuelezea suala la kituo cha Polisi kutokuwa wazi masaa 24 kuhudumia wananchi. Askari Polisi kama kawaida alitoa salamu za kawaida siyo za kisiasa za ''CCM Oyee'' au ''Kidumu Chama CHA MAPINDUZI'' halafu askari huyo mwenye weledi wa kazi yake akatoa sababu za kwanini baadhi ya vituo mkoani Pwani havifunguliwi masaa 24.

Hali hiyo ilimkera Mjumbe huyo wa Halmashauri ya CCM maarufu kama MNEC. Mjumbe huyo MNEC Bw. Haji Abuu Jumaa akaenda mbali katika mkutano huo wa wazi kuumbana askari huyo sababu ya kutosalimia ki-CCM huku kuna askari wengine wa vyeo vya juu huwa wanasalimia na kuuliza kama ni CHADEMA. Lakini Askari huyo kwa utulivu alimjulisha MNEC wa CCM kuwa taratibu na kanuni za uaskari Polisi hawaruhusiwi kusalimia ki-CCM au kwa kauli mbiu yoyote ya chama kingine cha siasa.

Mtendaji wa Kata akaingilia katika kuendelea kuelezea hali ya usalama Mkuranga baada ya Polisi huyo kutimuliwa kutoka katika mkutano na MNEC wa CCM. Mtendaji alisema Kutofunguliwa masaa 24 katika baadhi ya vituo vya Polisi ni kuwa kutokana na hali ya usalama ilivyokuwa mbaya huko nyuma siyo vituo vyote



Source: DARMPYA TV
 
Inauma pale sheria na taratibu zinapopindishwa kisa kuwapendeza kundi la watu.
 
Kuna mambo hapa duniani yanatokea Tz tu.Huwezi kuyaona popote duniani.
Kuulizwa swali la kwa Nini kituo hakifunguliwi masaa 24 nalo Ni swali la Askari yule kujikanyaga? Hadi kusema sihojiwi na chama? Yule Askari alitoka nje ya ulingo wa kazi Yake.Angejibu tu na Wala haikuwa kesi .Askari yule ana uelewa mdogo wa kazi Yake.Alipanic alipoona watu wamevaa nguo za CCM .Swali lile lilikuwa la kawaida kabisa la kikwzi Wala SI la kisiasa kwake.
 
Huyu polisi anajielewa sana, polisi hapaswi kudeclare uanachama hadharani.

Kaonyesha ukomavu wa kifikra.
IGP ashughulike na huyo polisi simtetei kabisa yeye Ndie kaingiza uchama kwenye jibu.Muuliza swali kaulize vizuri tu swali lake Huyo polisi ghafla akaingiza mambo ya chama kwenye jibu.IGP jionee mwenyewe.Hivi kweli Hilo jibu huyo Askari ndio alitakiwa atoe mbele ya hao wananchi? Wawe CCM au la.?
 
Kuulizwa swali la kwa Nini kituo hakifunguliwi masaa 24 nalo Ni swali la Askari yule kujikanyaga? Hadi kusema sihojiwi na chama? Yule Askari alitoka nje ya ulingo wa kazi Yake.Angejibu tu na Wala haikuwa kesi .Askari yule ana uelewa mdogo wa kazi Yake.Alipanic alipoona watu wamevaa nguo za CCM .Swali lile lilikuwa la kawaida kabisa la kikwzi Wala SI la kisiasa kwake.
Angalia hyo video clip vizuri tuliza mchecheto uelewe vizuri alafu urudi kutoa comment.

Polisi alikuwa anaanza kujibu swali akakatishwa na kulazimishwa kuanza na salamu ya ccm. So, wameona kama hataki kuwasalimu kichama hawataki majibu yake?? Wewe umeona hiyo ni sawa?? Hii nchi bado tuna safari ndefu sana!!!!
 
Angalia hyo video clip vizuri tuliza mchecheto uelewe vizuri alafu urudi kutoa comment.

Polisi alikuwa anaanza kujibu swali akakatishwa na kulazimishwa kuanza na salamu ya ccm. So, wameona kama hataki kuwasalimu kichama hawataki majibu yake?? Wewe umeona hiyo ni sawa?? Hii nchi bado tuna safari ndefu sana!!!!
Sio kweli hapo kwenye jibu la Askari ndipo Tatizo lilipo alisema hawezi jibu swali la chama wakati kaulizwa la kikazi
 
kweli kabisa comrade huyu afatwe saa sita usiku kwake,atakachofanyiwq iwe onyo kwa wengine wanaodharau chama tukufu chama kinachokubalika vibaya mno,watumwe wale vijana wa kazi the unknown assailants wakamshikishe adabu au apewe kesi ya ubakaji na uhujumu uchumi
Sio kweli hapo kwenye jibu la Askari ndipo Tatizo lilipo alisema hawezi jibu swali la chama wakati kaulizwa la kikazi
 
Kakosea swali aliloulizwa Ni la kawaida na angeulizwa hata na mwananchi wa kawaida kabisa na wa chama chochote.Kaulizwa Mbona kituo Cha polisi hakifanyi kazi masaa 24? Angejibu tu sababu Basi.Hayo ya kujitoa ohh Sio chama kihoji kachemka.Hata kiongozi wa chadema angehoji alitakiwa atoe jibu .Angechukulia tu kirahisi kuwa wananchi waliopo pale wanataka jibu hakutakiwa kuangalia hata muuliza swali Ni Nani angejibu tu Basi yangeisha wananchi wangeridhika na jibu Basi .Huyo Askari haelewi kuwa swali Hilo halikuwa la chama Bali la wananchi wa eneo lake .
Mkuu! Mbona video ipo wazi hapo juu, jamaa amemuuliza askari kuwa Kwanini kituo hakifanyi kazi masaa 24,na askari alipoanza kutoa majibu,huyo kada akamkatisha kwa kutaka aseme CCM OYEE kwanza then ndo aendelee kutoa majibu.lakini huyo askari anajua kuwa ni marufuku kwa askari wa jeshi lolote kujihusisha na siasa au kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa nchini,haki aliyopewa ni ya kupiga kura tu.Na hata kama ni mkereketwa wa chama fulani, yampasa iwe moyoni mwake na siri yake. Na sio kujiweka hadharani kwa umma.
 
Back
Top Bottom