PUTIN vs NETANYAHU: Njooni tumalize ubishi wa miamba hii miwili ya dunia

6 Pack

JF-Expert Member
Apr 17, 2022
1,997
4,289
Niaje waungwana

Leo nimeamua nilete kwenu uzi huu ili tumalizie ubishi uliopo mtaani kwetu kwa muda wa week tatu sasa bila kumpata mshindi wa kweli, huku kila kundi likivutia kamba upande wake.

Ubishi wenyewe unahusu miamba miwili yenye roho ngumu, maamuzi mazito na misimamo mikali isiyoyumba, wala kuyumbishwa na watu wengine. Na miaka hiyo sio mingine isipokuwa ni raisi wa Russia Vladimir Putin na waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu.

Kwanza kabla ya watu wengine hawajaingia hapa kutoa maoni yao kuhusu nani bora kati ya raisi Putin na waziri mkuu Netanyahu, naomba kwanza na mimi na mimi nitoe maoni yangu juu ya nani zaidi ya mwenzake.

1. Nikianza na raisi Vladimir Putin, huyu kwangu ni mwamba kweli kweli ambae kumlinganisha na bwege mpenda kulia lia kama Netanyahu ni kumkosea heshima Putin. Netanyahu ni mchumba na hawezi kufit kwa Putin hata kwa nusu ya sifa zake.

Putin ni kiongozi makini, mwenye akili kubwa, misimamo thabiti na intelejensia kali kuliko Netanyahu. Kwa kuthibitisha hili angalia uchaguzi wa uraisi wa 2016 alivyoweza kupachika vijana wake katika mifumo ya Marekani ili wamletee raisi anaemtaka yeye. Ni nani mwengine katika dunia ya leo mwenye uwezo wa kufanya kile alichofanya Putin, tena ndani ya ardhi ya Marekani na mifumo imara ya Marekani? Ni nani mungine?

I hope jibu hakuna maana hata China imeshajaribu kutuma mpaka maputo ili na yenyewe ifanye yake lakini yote yakashushwa. So Putin yeye aliweza tena kwa kuingilia mifumo ya ndani ya nchi bila kugundulika mpaka pale mission yake ilipokamilika, ndo alipokuja kushtukiwa ila akawa ashafanikiwa kwa 100%.

Tukija kwenye misimamo thabiti, jamaa amesimamia kile anachoamini yeye tu, bila kujali vitisho, vikwazo na kelele za nchi za magharibi including NATO. Ameingia nchini Ukraine kukamilisha mission zake bila kujali kelele za mtu yoyote. Si Marekani, NATO wala Umoja wa Ulaya aliethubutu kuingiza jeshi lake Ukraine kupambana na uvamizi wa Russia. Sana sana wameishia kutuma visilaha tu ili kujaribu kudhoofisha mission zake bila mafanikio.

Putin hajawahi kulia hadharani kuwa kaishiwa silaha au mbinu za kijeshi, NEVER. Yeye ni kutoa dozi tu na kusonga mbele daima, huku Marekani na washirika wake wakiendelea kuangamiza silaha zao kuipa Ukraine ili iizuie Ruusia kusonga mbele bila mafanikio.

Putin yeye anapambana na nchi kamili yenye raisi wake, serikali yake, jeshi lake (lenye mamilioni ya wanajeshi), silaha zake (za zamani na kisasa), ulinzi wake (juu na ardhini) Lakini bado haoneshi kushindwa wala kurudi nyuma. Nchi yake bado imeendelea kuogopwa hata na nchi zinazojifanya ni watemi wa dunia. Pia maangamizi yake yamekuwa yakiwalenga zaidi adui zake (wanajeshi na viongozi wa serikali) ikitokea raia ameuwawa basi ni kwa bahati mbaya ile tunaita ajali kazini. Ndiomaana toka vita vianze wanajeshi waliouwawa na wengi kuliko raia wa kawaida.

Putin pamoja na kuwa katika vita vinavyoshirikisha mataifa kibao ya Ulaya kuwa upande wa adui yake, lakini bado economic yake ipo imara mno, na ni nchi ya tatu kwa bajeti kubwa ya kijeshi duniani baada ya Marekani na China. Nchi yake haitegemei bajeti ya kijeshi kutoka nchi yoyote ile hapa duniani. Inajisimamia yenyewe miaka yote ya utawala wa Putin.

2. Tukija kwa waziri mkuu Benjamin Netanyahu, huyu kwangu ni mchumba tu mbele ya Putin, kwa sababu maamuzi yake hutegemea misimamo ya magharibi inasemaje. Yani inaonesha wazi kuwa huwa anapewa maelekeza ya nini cha kufanya na wakubwa zake kutoka huko West, na haswa Marekani.

Kila analolifanya Netanyahu sio ni la kwake bali ni la waliomtuma. Ndomaana wanapocheleweshaga kumtumia silaha za kufanikisha mission aliyopewa, hukimbilia katika vyombo vya habari na kuanza kulalamika kuwa wanamtelekeza na kumuacha apambane kivyake bila msaada wao.

Tukiachana na lile tukio la Oktoba 7, huko nyuma kabla ya Oktoba 7 jeshi la Netanyahu lilikuwa linatumika kwenda kuvamia makazi ya raia wasiokuwa na hatia, wala silaha yoyote zaidi ya mawe huko WEST BANK (katika ardhi inayokaliwa kimabavu na Israel) kuwachomoa watu katika nyumba zao, kuwapiga, kuwakata, kuwatesa na wengine kuwaua. Halafu nyumba zilizovamiwa walipewa waisrael waziishi. Sasa kiongozi (Netanyahu) unakuaje mahiri kwa kuongoza jeshi linalovamia tu raia na kuua ua hovyo eti kisa waliovamiwa wameokota mawe kuwarushia ili kupinga uvamizi?

Netanyahu na jeshi lake lenye wanajeshi zaidi ya laki 2, na wengine wa akiba wamekuwa wakitumia vifaru, meli za kivita, ndege zisizokuwa na rubani pamoja na silaha zingine nyingi za kisasa wanazopewa na Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Uholanzi na Canada kufanya mashambulizi ya kupambana na kundi la vijana elf 20 wa Hamas ambao wanatumia silaha za kawaida zilizoundwa kienyeji na wenyewe ili kujilinda. Lakini mpaka sasa Netanyahu amekuwa akionekana kuua watoto wengi na wanawake wasiokuwa na hatia bila kufikia lengo alilolipanga Netanyahu la kuhakikisha mateka wote wamepatikana katika muda mfupi aliopanga.

Netanyahu bado anategemea hela za bajeti ya jeshi, na uchumi wake zitoke katika mataifa mengine ya Ulaya ili aweze kuwalipa wanajeshi wake, kuongeza baadhi ya silaha na zingine ziishie katika tumbo lake na team yake.

So kumfananisha Putin na Netanyahu ni sawa na kumlinganisha hayati mwl Nyerere na bwana mdogo Pole pole hata kama Pole pole anajaribu kuvaa uhalisia wa mwl Nyerere.

Toa na wewe maoni yako, nikatawakilishe mtaani kwa kuangalia wingi wa comment zinazomkubali mmoja wapo ili tumalize ubishi na kufunga mjadala.

Karibuni sana...
 
images (28) (1).jpeg
 
Kumlinganisha Putin na Natenyahu ni kimvunjia heshima Putin.

Netanyahu ana nini kama yeye kila kitu anafanyiwa na Marekani na Ulaya anapewa pesa anapewa silaha.

putin anapigana vita na Nato na Ulaya na Marekani.

Netanyahu anapigana vita na watoto na wagonjwa leo unaenda mwezi wa 8 hawajui mateka wao walipo Gaza yenyewe ni ndogo kuliko Kigamboni.
 
Putin ni mwamba ila asijichanganye kwa muisrael ataaibishwa kama iran kilichompata
Sijui kama umesoma vizuri uzi hapo juu mkuu.

Jeshi la hitler liliwachinja waisrael kama vile mbuzi wanavyochinjwa kila siku pale Vingunguti machinjioni.

Jeshi la hitler lilivamia ufaransa, poland na nchi karibia zote wakateka miji na kufanya maangamizi makubwa.

Lakini jeshi hilo hilo la hitler lilishindwa vita na kuangamizwa vibaya na warusi hadi kupelekea kurudi nyuma na kupoteana.

So unapokuja kuandika kitu uwe na uhakika wa kujua unacho comment sio uandike tu kwa vile umelishwa propaganda za Israel na wenzako.

Israel bila Marekani, Ulaya na Nato ni sawa sawa na simba kibogoyo ambae hawezi kukamata windo na kulila.
 
Kumlinganisha Putin na Natenyahu ni kimvunjia heshima Putin.

Netanyahu ana nini kama yeye kila kitu anafanyiwa na Marekani na Ulaya anapewa pesa anapewa silaha...
Hata mimi nilishangaa kumfananisha Putin na Netanyahu. Ila baada ya kuona ubishi unazidi nikaona bora niulete huku, ili jibu litalopatikana hapa ndo likamalize ligi hii iliyopo mtaani.
 
Vichekesho ni vingi sana humu 😀 vile vile vya Gorbachev kupandikizwa na wamarekani😀

Kwamba Trump alipandikizwa na warusi ? Inachekesha
Kijana sijui umezaliwa baada ya mwaka 2016, au umeanza kufuatilia international news miaka hii miwili iliyopita.

Hebu soma hizo taarifa zilizotolewa na FBI wenyewe nchini Marekani.
Screenshot_20240522-161920.jpg
Screenshot_20240522-162029.jpg
 
Kijana sijui umezaliwa baada ya mwaka 2016, au umeanza kufuatilia international news miaka hii miwili iliyopita.

Hebu soma hizo taarifa zilizotolewa na FBI wenyewe nchini Marekani.
Hana anachojua huyu kazi yake kusoma habari leo na kusikiliza millard ayo atajua wapi habari kama hizi, angekuwa mfuatiliaji wa masuala ya kimataifa asingeweza kubisha vitu obvious kama hivi
 
SAsa wewe na cia nani anayejua zaidi?
Huyo anaonesha ni kijana alieanza kushika sim juzi juzi. Hivyo habari nyingi zilizopita yeye hawezi kuzijua.

Nimemuwekea na fact katika comment ya #16 kama mwenye akili ataiona na kukubali kuwa akiandika bila kujua kitu.
 
Back
Top Bottom