Mkuu jisomee kidogo kwanza kabla ya kuleta uzi jf huku kunawatu wanafikiri kwa kutumia vichwa
Baada ya kutolewa kwa Hati ya kukamatwa kwa rais wa Urusi Vladimir Putin watu wengi wamekuwa na shahuku ya kujua hati hii itafanyaje kazi? Na je raisi huyu anawezaje kukamatwa huku akiwa madarakani tena nchi yake (Urusi) pamoja na nchi aliyotuhumiwa kuifanyia uharifu (Ukraine) zikiwa sio wanachama wa ICC?
Tuanze na swala la uanachama, ICC ni mahakama ya kimataifa inayoshughulikia makosa ya kivita(War crime), uharifu dhidi ya binadamu( Crime against humanity), Mauaji ya Kimbali (Genocide) na Uvamizi (Act of Agression) Mahakama hii ilianzishwa Julai 1, 2002 huku ikiwa na wanachama 60 kufuatia Mkataba wa Roma wa Mahakama ya Jinai ya Kimataifa (Rome Statute) wa mwaka 1998. Baadhi ya mataifa ambayo hayakukubali kuwa wanachama wa Mahakama hii ni Marekani, China, Iran, Israel, Qatar, na Libya.