eden kimario
JF-Expert Member
- Jun 13, 2015
- 10,355
- 16,401
PUTIN AZUNGUMZIA USAMBAZAJI GESI ULAYA
MOSCOW, Urusi
RAIS wa Urusi, Vladimir Putin amekadiria kuwa kwa mwaka huu nchi yake itakuwa imesambaza gesi mita za ujazo bilioni 200 kwa bara la Ulaya. Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza mazungumzo na kansela wa Austria, Sebastian Kurz alisema “Mwaka huu makisio yetu tutakuwa tumeuza gesi mita za ujazo bilioni 200 kwa bara la Ulaya”.
Aliongeza: “ nchi za Ulaya hazina namna zitalazimika kutumia gesi ya Urusi kwa sababu gesi za nchi nyingine ni ghali na zitapunguza ushindani kwenye uchumi wa Ulaya”. Rais Putin alisema Urusi na bara la Ulaya zote zina maslahi kwenye mradi wa bomba la kusambaza gesi la Nord Stream 2 hasa wakati huu ambao mahitaji ya gesi kwa nchi za Ulaya yanaongezeka.
“Haiwezekani Ulaya inunue gesi ghali kwa asilimia 30 kutoka Marekani… inawezekana lakini sio sahihi, hii itapunguza ushindani wa wao wenyewe duniani,”alisema. Alisema mradi huo wa bomba la gesi unatakiwa kutekelezwa kwa maslahi ya uchumi wa dunia. “Urusi inaikaribisha Austria kwenye kuunga mkono mradi huu wa bomba la gesi ambao ni muhimu kwa bara zima la Ulaya,”alisema na kuongeza: “Nchi yetu(Urusi) inasambaza gesi vizuri kwa Austria na kuelekea kweye nchi nyingine za Ulaya…haya ni matunda ya ushirikiano wetu katika eneo la nishati”.
Alisema anategemea nchi za Ulaya zitapambana kwenye ushiriki wao katika mradi wa bomba hilo la gesi na ku- sisitiza “Bulgaria ilikataa kushiriki kwenye mradi wa bomba la gesi la South stream kutokana na shinikizo, lakini sasa wanajuta na wanataka tuwapelekee gesi kupitia bomba la Turk, hakuna atakayetaka nchi za Ulaya ziwapate kama ilichokipata Bulgaria kuonesha udhaifu wao wa kushindwa kulinda maslahi yao”.