Putin akienda Alaska atakamatwa?

Putin akienda Alaska atakamatwa?

Akienda Alaska hatokamatwa ila akija Kizimkazi tunamdaka, mahakama ya kimataifa tunaiheshimu.
Myahudi na Mmarekani wemeshindwa kuiheshimu,ila wao wanajidai ma bwana jela wa kusakizia wengine kwa hiyo mahakama!
 
Marekani haiwezi kumkamata huyu Mzee kama walivyokataa kumkamata Netanyau.
Vipi ingekua Duterte kabla hakakamatwa halafu akaenda Marekani kutembea na ICC wameshatoa shauri la kukamatwa na yeye wasingemkamata?
 
Marekani siyo mwanachama wa ICC hawezi kutii maagizo ya mwendesha mashitaka wa ICC.
Haya mambo msiyavamie kama hamyajui vizuri.
Kwanza duniani hakuna mtu au taifa la kumkamata raisi wa Russia, Marekani, Waziri mkuu Israel au raisi wa China.
Hizo ndoto za mchana.
 
Ndo tunajifunza hivyo kutoka kwenu wanazuoni
 
Moja kwa moja kwenye swali langu.
Mahakama ya ICC ilimhukumu Putin kwa makosa yanayohusiana na vita ya Ukraine na kutaka akamatwe.
Sasa ni wazi Putin ataenda kuongea na Rais wa Marekani Bwana Trump katika jimbo la Alaska lililoko katika nchi ya marekani.
Hapa ni kama mbuzi kafia kwa muuza supu.
Kwa hiyo nadhani Marekani wamepata nafasi ya kumtia mguvuni Bwana Putin.
Kumbuka Marekani iliunga mkono maamuzi ya mahakama hiyo.
Au wadau mnasemaje?
Nimeamua kukumbusha TU ili wasije wakasahau hao ICC.
Kama wasipomkamata atakamatwa na nani Sasa?
Maana Marekani ndio taifa kubwa kuliko yote ulimwemguni,waliweza hata kumkamata rais wa zamani wa Panama, Bwana Mannuel Antonio Noriega na kumfunga katika jela za Marekani.
Nasubiri kwa hamu Putin kutiwa pingu kama walivyotiwa pingu Marais Slobodan Milosevic wa Yugoslavia na Charles Taylor wa Liberia kwa Amri ya ICC.
Lakini pia Putin kwenda Marekani itakua rahisi kwa serikali ya marekani kumaliza hamu Yao ya muda mrefu ya Regime change kufanyika huko Urusi,Kwa kumfanya chochote ili asirudi Urusi.
Tunasubiri.
tunasema hiviii...asante kwa kutukumbusha,ila wasipomkamata wao UTAMKAMATA WEWE🤝😁
 
Badala ya kuomba PM wa Israel akamatwe unakimbilia kwa putin
 
Back
Top Bottom