UZUSHI Putin aitaka Kenya kumaliza njaa badala ya badala ya kuifunza Urusi namna ya kumaliza migogoro ya Kimataifa

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Source #2
View Source #2
Rais wa Urusi Vladimir Putin, amelitaka Taifa la Kenya kumaliza kwanza njaa nchi Kenya badala ya kuifunza Urusi namna ya kumaliza migogoro ya Kimataifa.

Putin amemfananisha Balozi wa Kenya Umoja wa Mataifa kama kijana mdogo anayejaribu kuutikisa mbuyu na kuishia
 
Tunachokijua
Balozi wa Kenya, Martin Kiiman, ambaye ni muwakilishi wa Kenya katika Umoja wa Mataifa(UN) katika mkutano wa UN alitoa kauli ya kulaani tukio la Urusi kuipiga Ukraine tukio lililoanza February 24, 2022.

Baada ya kauli yake ya kulaani tukio hilo, kulikuwa na uvumi kuwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin alijibu kwa kusema Kenya inabidi ijizatiti kwenye kuondoa njaa nchini mwao na sio kuzungumzia sera za nje za Urusi.

Hata hivyo, suala hilo limeonekana kuwa si kweli kuwa Rais Putin aliisema Kenya. Kauli ya Rais Putin ilikuwa kwamba watapambana na yeyote anayetaka kuwazuia kufanya oparesheni yao. Hakuitaja Kenya wala nchi yoyote moja kwa moja.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…