madaili
Member
- Mar 6, 2014
- 32
- 27
Kuna jamaa alikuwa hajawahi kupanda ndege, siku akapata safari ya kupanda ndege kuelekea ng'ambo.
Kabla hajaenda aliomba ushauri toka kwa wazee, mzee mmoja mbwabwajaji sana kijijini kwao akamwambia kwenye ndege inabidi uwahi siti(seat), ama sivyo utajikuta unasimama masaa yote.
Kwa hiyo jamaa baada ya kuingia kwa ndege alikimbilia kuwahi siti, kama unavyojua kawaida yetu akakimbilia siti ya mbele kabisa pembeni ya dereva(pilot) ili afike mapema. Jamaa mwingine akaingia na kumwambia kwa ustaarabu "Samahani, hii ni siti yangu, nipishe ukatafute siti yako"
Jamaa akamaka kwa hasira "Wewe usinifanye mimi mshamba, najua siti zimejaa huko sasa unataka kufanya ujanja ujanja uchukue siti yangu, nshapanda ndege mara nyingi kuliko wewe, anayechukua siti wa kwanza ndio siti yake, au unadhani hii siti imeandikwa jina lako? Ulinunua wewe hii siti? Nenda kawadanganye washamba wengine huko."
Jamaa hakujua afanye nini akaishia kumwambia "Sawa ila kama wewe mjanja leo nakuachia uendeshe hii ndege basi"
#Utani sio lazima ucheke, mara nyingine huwa ni mizaha tuu, siku njema wanajamii