"Puppets":Namna ya Kujitambua Kama Uu Miongoni Mwao!. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"Puppets":Namna ya Kujitambua Kama Uu Miongoni Mwao!.

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Pascal Mayalla, Jun 7, 2012.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,547
  Likes Received: 18,204
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,
  Puppets ni watu ambao wanaamini kila lisemwalo au lifanywalo na mataifa mabeberu ndio right hata kama ni la uongo!.

  Natoa darasa dogo la bure jinsi ya kujitambua kama na wewe ni puppet au la, maana kuna baadhi yetu humu ni pupoets wengine kwa kujijua hivyo kuwa puppets kwa makusudi lakini wengine bila kujijua wao wanajihesabu ni wazalendo wa kweli wa nchi hii lakini at the end of the day huishia kuwa puppets, hawa ni wa kusaidiwa kujitambua zaidi na hivyo kuoachana na u puppets na kugeuka wazalendo wa kweli!.

  Kipimo cha kujijua kama wewe uu miongoni mwa wazalendo wa kweli au uu miongoni mwa puppets, ni kwa kujiangalia wewe unasisimama kati ya Mabeberu wakuu ambao ni US na wapambe wao wakuu ni UK! katika migogoro ya kimataifa.

  Nitatoa mifano michache.

  Iraq, Libya na Afghanistan.

  Iraq US na washirika wake waliishambulia kwa kisingizio cha kuzitafuta WMD ili waziangamize. Baada ya kuzikosa wakaendeleza mashambulizi mpaka kumuangamiza Saadam kwa kisingizio cha gross human right violation!.

  Mmerekani ndipo hapo akaweka msimamo kuwa lazima au uwe nasi au ni adui yetu!. At the end of the day, Mmarekani amesababisha maafa makubwa zaidi kwa wananchi wa Iraq kuliko madhara waliyoyapata katika kipindi chote cha Saadam!.

  Katika mgogoro huo, jee wewe ulisimama wapi?. Kama ulisimama na mabeberu jihesabu uu miongoni mwa puppets!.

  Vivyo hivyo kwenye mgogoro wa Libya, kama ulisimama na Ghadafi then wewe ni mzalendo wa kweli, lakini kama ulisimama na Waingereza, wewe nawe uu puppets kwa kujijua au bila kujijua!. The same applied to Afghanistan, watu wangapi wasio na hatia wameuwawa na Wamarekani na washirika wao to persue Osoma?!. Only to be found in Pakistan!.

  Kuwa puppet kwa kujijua sio kitu kibaya kwa vile unakuwa you have made your choice kuwaunga mkono mabeberu, lakini ukiwa puppet bila kujijua, hii thread ni fursa kwako kujitambua na kubadilika toka puppet na kuwa mzalendo wa kweli!.

  Jee wewe umesimama wapi?.

  Wasalaam.

  Pasco!.
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Yaani tuko Bar afu tunaongelea 'kilimo kwanza'
  Elimu haina mwisho, okay!

  Ni bora puppet asiyejijua kuliko anayejijua na anaamua kwa makusudi kuwa puppet.

  Asiyejijua mie naona ni 'Ignorance' na anayejijua naona ni 'Evil Intention'

  Sasa ina maana bora kukaa na mtu mwenye evil intention kuliko ignorant?
   
 3. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Hii nimeikuta kwenye dikshenari...............Puppet is somebody who can be manipulated:a person, government, or organization whose actions are controlled by others.


  Lakini Pasco hii habari ya kwamba kama unawaunga mkono mabeberu wewe ni "puppet' na kinyume chake mzalendo sikubaliani nayo.........Kwa sababu rahisi tu...Kwamba inawezekana anachokifanya yule anayepingana na mabeberu ni cha hovyo.

  Kwa mfano imetokea kwamba serikali yetu inafuta vyama vya upinzani bila shaka kwanza nchi za magharibi (kibeberu) zitapiga kelele na kwa maana hiyo hata sisi wenyewe tutapiga kelele...na haina maana tutakuwa "puppet"
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,866
  Likes Received: 6,218
  Trophy Points: 280
  nitarudi, mshanichanganya kichwa nyie....
   
Loading...