Ni kipi kinakosekana kwenye ndoa za siku hizi?

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
8,184
11,608
Kwanza ni rahisi sana kuvunjika, kuvumiliana ni zero, kusameheana ni finyu mno.
Migogoro na mafarakano kwenye familia hayaishi.
Visasi na vinyongo kama vyote.

Ndoa nyingi ni kama uwanja mapambano au harakati flani tu. Ni mwendo wa kuviziana na kutegeana, nani miongoni mwa wanandoa alianzishe au across the line wa kwanza ili vita, uharibifu na msambaratiko ulipuke.

Kwa mkemia mkuu foleni kwenda kupima DNA ni kubwa sana.

Uhakika wa members wazaliwa kwenye familia za wanandoa ni zero.

Halafu sasa vikumbo na mashindano ya madingii wenye ndoa zao, dhidi ya vijana wanao jipanga na maisha ya ndoa, struggles za kuwin pisi kali baina ya vijana na wazee hao wenye ndoa zao, mchuano ni mkali mno.
Pesa imekua silaha muhimu sana kwenye mapambano haya.

Imefikia mahali nyumbani kwa pisi kali akiingia mzee huyu, akitoka anaingia kijana yule.

Na wote ni walipaji kodi ya nyumba bila kujijua.

Wanapangiwa na pisi kali waje lini.

Na vilevile imekua ni rahisi sana kwa wamama wenye ndoa zao kuchepushwa nnje ya ndoa au kuchepuka nje ya ndoa yake. Imekua rahisi mno siku izi na kawaida kweli.

Nini sababu za yote haya.

Wapi makosa yamefanyika yarekebishwe.

Ndrugu zangu..
 
Wengi machoni wako pamoja rohoni kila mtu ana lake
FB_IMG_1701962175685.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndoa za zamani zilidumishwa kwa ubabe na kipigo. Hao wazazi tunawasifia walipendana sana sivyo hata kidogo. Ubabe na vipigo ndiyo vilidumisha ndoa
Ongezea na adabu Yani mtu akimkosea mumewe anawaza atawaambia nn wazee na wazee wakiwaita Kwa kwaajili ya usuluhishi unaenda Kwa kutambaa na magoti😃😃😃

Sikuhiz ukipigwa kibao simu moja tu kwenu wazazi wanasema turudishie mtoto wetu hatujamfukuza😂😂😂
 
Ongezea na adabu Yani mtu akimkosea mumewe anawaza atawaambia nn wazee na wazee wakiwaita Kwa kwaajili ya usuluhishi unaenda Kwa kutambaa na magoti

Sikuhiz ukipigwa kibao simu moja tu kwenu wazazi wanasema turudishie mtoto wetu hatujamfukuza
Ukweli wazazi wanachangia kuvunjika kwa ndoa nyingi yaani mzazi hawezi kusema uchafu wa binti yake au kijana wake
 
Kwanza ni rahisi sana kuvunjika, kuvumiliana ni zero, kusameheana ni finyu mno.
Migogoro na mafarakano kwenye familia hayaishi.
Visasi na vinyongo kama vyote.

Ndoa nyingi ni kama uwanja mapambano au harakati flani tu. Ni mwendo wa kuviziana na kutegeana, nani miongoni mwa wanandoa alianzishe au across the line wa kwanza ili vita, uharibifu na msambaratiko ulipuke.

Kwa mkemia mkuu foleni kwenda kupima DNA ni kubwa sana.

Uhakika wa members wazaliwa kwenye familia za wanandoa ni zero.

Halafu sasa vikumbo na mashindano ya madingii wenye ndoa zao, dhidi ya vijana wanao jipanga na maisha ya ndoa, struggles za kuwin pisi kali baina ya vijana na wazee hao wenye ndoa zao, mchuano ni mkali mno.
Pesa imekua silaha muhimu sana kwenye mapambano haya.

Imefikia mahali nyumbani kwa pisi kali akiingia mzee huyu, akitoka anaingia kijana yule.

Na wote ni walipaji kodi ya nyumba bila kujijua.

Wanapangiwa na pisi kali waje lini.

Na vilevile imekua ni rahisi sana kwa wamama wenye ndoa zao kuchepushwa nnje ya ndoa au kuchepuka nje ya ndoa yake. Imekua rahisi mno siku izi na kawaida kweli.

Nini sababu za yote haya.

Wapi makosa yamefanyika yarekebishwe.

Ndrugu zangu..
Mahusiano hayanaga kanuni ikiwa Wahusika wenyewe hawajitambui na kujiheshimu.
 
Kutojuwa haki za ndoa ni zipi mke au mume
sababu zilizotajwa na wananzengo humu Jukwani mpaka sasa...

Bado nasubiri zaidi...

1. marafiki miongoni mwa wanandoa wanachochea wanandoa kusambaratika.

2. wazazi wanachochea msambaratiko kwa wanandoa, mathalani baada ya kutofautiana kidogo ndoani.

3. kukosekana adabu miongoni mwa wanandoa, hawaheshimiani.

4. kukosekana ufahamu na uelewa mdogo juu ya haki na wajibu wa wanandoa katika ndoa.

5. kukosekana malengo na nia ya pamoya miongoni mwa wanandoa.

6. kukosekana upendo wa dhati baina ya wanandoa.

7. kujimwambafai miongoni mwa wandandoa ndani ya ndoa
 
8. Kukosekana huruma baina ya wa ndoa,

9. Kukosekana uvumilivu pale mwanaume anaporudi nyuma kimaendeleo Au mwanamke anapochelewa kupata mtoto
 
Back
Top Bottom