Punguza size ya video bila kupoteza quality (100%)

DX2018

Member
Nov 24, 2018
55
45
Wakuu mambo vipi.

Leo nimekutana na hii software inaitwa jen-free video compressor.

Hii ni software ambayo hupunguza size au ukubwa wa video bila kupoteza quality. Kiukweli suala la MB hasa kwenye ku-upload video kwa sisi Youtubers ni tatizo.

Unakuta ume edit na ku export video yako vizuri tu, kuja kucheki size 2GB au hata 590MB. Kwa wenzangu na mimi wabahili na kubana matumizi hizi ni MB nyingi sana na inachukua muda mrefu mpaka video kuwa completely uploaded.

Sasa bana leo nimejaribu kupitia hii software baada ya kuiona kwa watu wengi sana hasa wahindi wanapenda sana kutumia hii. Nilikuwa naiona icon tu ila jina sijui sasa leo nikafanikiwa kuifuma sehemu.

Kiukweli kama una video ina MB 500 ina uwezo wa kushusha mpka 128 au 98 MB kwa nilivyotest, na nimejaribu kuiupload Youtube upande wa kudownload katika machaguzi ya quality 720p ipo pamoja nimeicompress.

Unaweza pakua hapa MEGA

Kwa wale creators wenzangu mimi nimejaribu na Kinemaster na Adobe iko poa. Na kama una alternative software yako please share nasi tupate enjoy.

Best-Video-Compressor.jpg
 
Ushauri tu kwa watakaotumia kama una video kubwa na una PC ndogo utaihurumia PC yako mimi yangu ilikuwa feni inalia kama machine ya kusaga. Kama una video kubwa sana tafuta PC nzuri.
Kwa sisi watumiaji wa simu unatusaidiaje?
 
Okay mimi nilikuwa nafanya hivi, naedit kwenye simu na kinemaster kisha na export kwenye output yenye high standard and quality mfano QHD then natumia Vivavideo Pro kucompress. Vivavideo ina compressor nzuri sana na utashangaaa ukijaribu. Ingiza ile video yako ulioexport na kinemaster kisha export tena na Viva, video inakuja kuwa high compressed na unaweza upload YouTube
Kwa sisi watumiaji wa simu unatusaidiaje?
 
Thanks for sharing mkuu.

Kwa upande wangu huwa ninapunguza ukubwa wa video mtandaoni kupitia website ya PS2PDF. Ipo vizuri, kuna wakati video ya MB 10 inapunguzwa mpaka MB 1 au KB 900. Ubora wa video hauathiriki; na logo ya PS2PDF haitokei kwenye video husika.

Link:

 
Mimi natumia Vimady Video Compressor kuedit na kucompress video kwenye simu bila kupunguza ubora. Search Chrome Vimady for Androids & IOS.
 
Kwenye simu kinemaster ndio mshindi na ndio best video editor yenye uwezo mkubwa kama wewe ni mtundu
Mimi natumia Vimady Video Compressor kuedit na kucompress video kwenye simu bila kupunguza ubora. Search Chrome Vimady for Androids & IOS
 
Hii ina app kwel
Thanks for sharing mkuu.

Kwa upande wangu huwa ninapunguza ukubwa wa video mtandaoni kupitia website ya PS2PDF. Ipo vizuri, kuna wakati video ya MB 10 inapunguzwa mpaka MB 1 au KB 900. Ubora wa video hauathiriki; na logo ya PS2PDF haitokei kwenye video husika.

Link:


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom