Punguza marafiki feki

madeinmusoma

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
322
386
Punguza marafiki ambao ukiwaambia unataka kufanya kitu wanakujibu "utawezaaa?" Punguzaaaa!

Punguza marafiki ambao kutwa wanataka mchafue meza bar. Punguzaaaa!

Punguza marafiki ambao umeongea nao kitu mkiwa wawili mwisho wa siku unakikuta kimeenea sehemu nyingine. Punguzaaaa!

Punguza marafiki ambao wako right kila siku wenyewe hawataki kuambiwa wamekosea. Punguzaaaa!

Punguza marafiki ambao wakija kwako wao urafiki unahamia kwa mumeo au mkeo aliyekaa sebuleni wakati wewe kakuacha nje. Punguzaaaa!

Punguza marafiki ambao wanakuwa na urafiki na maadui zako kwa ukaribu zaidi. Punguzaaaa!

Punguza marafiki wa kwenye raha tu ukiwa na shida unajikuta peke yako. Punguzaaaa!

Punguza marafiki wanaokusifu huku wakijua umekosea. Punguzaaaa!

Punguza marafiki ambao kila ukiwapigia simu na wao utawasikia yaani nilitaka kukupigia sasa hivi. Punguzaaaa!

PUNGUZA MIZIGO ISIYOKUWA NA UMUHIMU
 
sasa unatafutaje pesa bila kuwa na involvement na marafiki mkuu..au pesa unatafutiaga angani ww mkuu.jamaa yuko very right na mada yake
Usichanganye 'marafiki' na 'wafanyakazi wenzio' au 'wafanyabiashara wenzio' rafiki si lazima ahusike ktk utafutaji wako, ila unaweza kutengeneza uhusiano mzuri na watu wanaokuzunguka kazini lakini haina maana ni marafiki zako.
 
me nafanya biashara na marafiki zangu niwafanya biashara wenzangu kwaio hakunaga biashara bila rafiki pale ambapo huwa nashindwa kuuza kazi zangu lazima nitengeneze urafik kwanza maana huyo ninae target tyr anamarafik zake nawanamapa bidhaa kwaio hawez kuwaangusha ili mm nimpatae lazima niwe rafik yake ndo system yangu ya hela zangu na kaz zangu, mara nyingi sana nashindwa kupenya kwa wale finance giant kwakuwa tyr wana marafiki hivo inanipaga ugumu sana
 
Bado hujaelewa ulichojibiwa hapo, soma tena kwa utulivu... au kubali kipo juu ya uwezo wako!
 
Umezunguka sana mkuu,yaan kupunguzanyama hapo chini,jitengeneza ww ndio ufuatwe na watu kuliko ww kuwafuata wengine
 
Punguza marafiki ambao ukiwaambia unataka kufanya kitu wanakujibu "utawezaaa?" Punguzaaaa!

Punguza marafiki ambao kutwa wanataka mchafue meza bar. Punguzaaaa!

Punguza marafiki ambao umeongea nao kitu mkiwa wawili mwisho wa siku unakikuta kimeenea sehemu nyingine. Punguzaaaa!

Punguza marafiki ambao wako right kila siku wenyewe hawataki kuambiwa wamekosea. Punguzaaaa!

Punguza marafiki ambao wakija kwako wao urafiki unahamia kwa mumeo au mkeo aliyekaa sebuleni wakati wewe kakuacha nje. Punguzaaaa!

Punguza marafiki ambao wanakuwa na urafiki na maadui zako kwa ukaribu zaidi. Punguzaaaa!

Punguza marafiki wa kwenye raha tu ukiwa na shida unajikuta peke yako. Punguzaaaa!

Punguza marafiki wanaokusifu huku wakijua umekosea. Punguzaaaa!

Punguza marafiki ambao kila ukiwapigia simu na wao utawasikia yaani nilitaka kukupigia sasa hivi. Punguzaaaa!

PUNGUZA MIZIGO ISIYOKUWA NA UMUHIMU
Mambo mengine ukiyafatilia unaweza kujikuta uko peke yako,tujifunze kuishi na kila mtu kutokana na mazingira
 
Back
Top Bottom