Punda wanateswa, wanaharakati za wanyama mko wapi?

Punda wanateswa, wanaharakati za wanyama mko wapi?

Myloo

New Member
Joined
Jul 13, 2021
Posts
1
Reaction score
11
Jama kwani hapa Tanzania hakuna wanaharakati wanaojihusisha na haki za wanyama?

Maana hapa Katoro Geita Punda wanateswa sana yani wanabeba tofali asubuh hadi saa 9pm. Njia zenyewe makorongo tupu yani punda unawahurumia, nakumbuka kipindi cha JPM walikuwa wanafanyishwa kazi kuanzia asubuhi mwisho saa 10:00am lakini sasa hivi duh yani punda wana vidonda balaa kwa yale mateso hapana kwakweli
 
Kwani kipindi cha Magufuli punda walikuwa wameajiriwa?
Kipindi cha JPM serikali iliajiri watumishi wa umma kwaajili ya kusimamia haki za punda na sasa watumishi wamestaafu?
Punda mikoa mingi wanafugwa ila wasukuma natural ni wakatili.
Nilikuwa usukumani 2014/2015 niliona punda wakiteswa sana.
Ni issue ya jamii husika kutokuwa na utu na ustaarabu.
Njombe punda wanaishi vizuri tu hawafi kwa mizigo ya mawe na matofali
 
Pana jamaa mmoja muhuni sana aliwasimamisha punda waliobebeshwa mzigo mzito sana akawatua harafu akawacha waende zao huko ilikua Mbeya watu walicheka sana maana jamaa aliwabebesha mkaa kama kirikuu sijui ilishaaje ila kesi maana mwenye punda alikua mbali kidogo..
 
Laiti mngefahamu kwa nini wahindi hawapendi kufuga fuga hovyo mngejiepusha na laana

Wakati mmoja roho za wa pendwa wenu hurudi kwa maumbile ya viumbe wengine kutimiliza pasiposazwa

Na nyie mbwa mnawagharikisha bila soni, mlaaniwe
 
cheki na hawa jamaa labda watakupa abc ya nn cha kufanya apo kuwaokoa hao punda.

Arusha Society For the Protection Of Animals (0736 500678/0786 533 399)
 
Yapo mashirika yanayolinda wanyama ila tatizo hiyo miradi inahitaji ufadhili pia. Ila kuna watu kama MAWO hawa wanalinda hao Punda alafu kuna wengine Mbwa Africa hawa kama jina lao lilivyo.
 
Inasikitisha sana,mara nyingi wanaotesa punda kutajirika huwa ni ngumu
 
Hata sisi tunaweza kuwapa elimu na kuwaelewesha vizuri tu bila ghadhabu wala ugomvi
Hao wenye Punda ni binadamu wasiokuwa na huruma.
Kwa hiyo wanataka kupewa maneno kuntu

Hii ni kweli kabisa
Kuna siku nilikuwa nimo chumbani kwangu (ilikuwa alfajiri)
Mara nikasikia fimbo za uhakika na sauti ya kitu kizito karibu na dirisha langu.

Nikacgungulia na kuona mkokoteni wa punda na mtu akimpiga yule Punda aliekuwa amebebeshwa matikiti kwenye mkokoteni.

Nilitoka nje na kumwambia huyu Punda ni wa kwako?
Ndio
Kwanini umpige wakati yeye ndio anakuingizia kipato na kulisha familia yako?
Kimya
Nikamuuliza tena umetoka shamba huko manane ya usiku Je umembebea hata maji na majani ya kula?
Hapana
Huoni kama humtendendei haki kiumbe anaekuingizia kipato?

Nikamwambia kwanza amtoe huo uzito shingoni
Nikamletea ndoo ya maji Punda

Nikamwambia siku nyingine Mpe haki yake anayostahili huyu kiumbe

Alipata somo na kuapa hata rudia kumpiga bali atampa haki anazostahili.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom