Pumzika salama mdogo wangu rose

davina

Senior Member
Jan 21, 2012
113
87
Leo ni siku ambayo umenijia sana akilini mwang ikiwa ni miaka sita tangu ulipotutoka mdogo wangu Rose ukiwa na miaka 12 ni kumbu kumbu mbaya ambayo haitafutika katika ubongo wangunimelia sana , nimemlaumu Mungu sana lakini sasa naanza kuamini kuwa sintakuona tena duniani,,Nakuombea pumziko la milele nategemea siku moja tutakuwa wote Mbinguni tukifurahia uzima wa milele
 
Ulikuwa na matumaini ya kumwona hadi leo?

Pole sana mwanangu Rose!...miaka 12 ulikuwa baDo kabisa hujajua dunia ni nini!
Lakini kwetu sisi wenye Imani tunaamini katika kutaniko kuu, ambapo WIMBO WA DAUDI UTAIMBWA NA JESHI LA MALAIKA.
 
Bwana alitoa akatwa jinalake lihimidiwe!
Pole mpendwa sote tusafari moja
 
Davina, naomba sana futa usemi wako kuwa "umemlaumu MUNGU sana". I beleive MUNGU ni mtu/kitu chA JUU saana huwezi kutamka hivyo. Tushukuru kwa Kila jambo, ukisoma Bible kitabu cha Ayubu kuna mahali Mke wa Ayubu akamwambia Ayubu amkufuru MUNGU ila afe, Aybu akamjibu akamwambi ....je tupate mema tu tusipate na mabaya? sasa swali hili nakuuliza na wewe pia, ulitaka upate mema tu usipate na mabaya pia???
 
Pole sana mipango ya Mungu hayana makosa kila mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke ataonja mauti. Tunapaswa kushukuru kwa kila jambo. Kila mtu ana mwisho wake wa maisha haya
 
Pole sana Davina, kumbuka Imeandikwa katika kitabu cha Ayubu kuwa mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake ni chache lakini pia kazi ya Mungu haina makosa twapaswa kushukuru kwakila jambo ili mapenz yake yatimie maana Bwana anahaja nasi. Usilie ila tumaini kuwa iko makusudi ya Mungu ndo maana ikawa hivyo...kikubwa nikutazama amelala katika nani ili siku itakapofika ya mwisho ujua atakuwa upande upi kisha nawe ujisafishe na kuchagua pakutumikia. Amen.
 
Leo ni siku ambayo umenijia sana akilini mwang ikiwa ni miaka sita tangu ulipotutoka mdogo wangu Rose ukiwa na miaka 12 ni kumbu kumbu mbaya ambayo haitafutika katika ubongo wangunimelia sana , nimemlaumu Mungu sana lakini sasa naanza kuamini kuwa sintakuona tena duniani,,Nakuombea pumziko la milele nategemea siku moja tutakuwa wote Mbinguni tukifurahia uzima wa milele
Kwanza pole sana.

Hapo kwenye highlighted point naona kama unamkosea Mungu, huwezi kusema una mlaumu Mungu, naona unajitafutia dhambi za bure.
 
pole sana kwa kuondokewa na mdogo wako kumbukumbu ambayo haiwezi kufutika daima. Yote ni mapenzi ya Mungu na maamuzi yake yaheshimiwe!
 
Pole sana davida, jitahidi kuupokea ukweli dear. I know sometimes mtu unatamani hata kuzirudisha siku nyuma, lakini ndo hivyo tena haiwezekani!! Nakusihi usivunjike moyo mpendwa wangu wala kulaumu kwa vyovyote.....kwani Mungu bado anakupenda!!
 
Pole ndugu....kazi ya mungu.
Duuh nimeshanga kumbe kuna watu wana-like mpaka habari za huzuni/misiba, looh JF kiboko
 
pole sana davina njia alopita rose ni yetu sote,kumbuka kumshukuru mungu kwa kila jambo kwani duniani tunapita sisi sote ni wasafiri.
 
nashukuru sana wana jamiiforums kwa ushauri na michango ya kimawazo ambayo mmekuwa mkitoa.MUNGU AWABARIKI SANA..LOV U ALL
 
Back
Top Bottom