Pumzika kwa amani Plasidia Rugalema

Pole,sana kwa kumpoteza mpendwa wako.
Kuishi ni zawadi tu............................
 
Poleni sana ni workmate wa rafiki angu pia hapo Takukuru Mwanza. Inasikitisha kifo cha ghafla hivyo jamani
 
  • Thanks
Reactions: ram
Hivi kuna sababu gani ya kumtendea mwingine ubaya kama mwisho wetu wote ni kifo?

Apumzike Kwa Amani Mwendazake.
 
Poleni Sana inasikitisha kwakweli. May her soul rest in eternal peace
Ijumaa ya 24.1.2020,saa 8:15 Usiku ulinipigia simu kuwa Umefika Igoma-Mwanza kuwa unatoka Musoma,mahakamani kwa shughuli kama sehemu ya kazi za mwajiri wako (TAKUKURU), Ulikuwa na Furaha kubwa na jinsi ulivyokuwa unachangamka basi hatukujua kama mauti yako mbioni kukunyakua, sikujua kama Jumatatu ya 27.1.2020 haitakukuta hai,ama haitaisha ukiwa hapa duniani.

Uliahidi tena kunipigia simu weekend tuendeleze mjadala na mawazo ambayo tayari tuliokuwa tumeyaanzisha tangu 31.12.2019 . Maongezi na namna ya mipango haikuonyesha una dosari yoyote ya kiafya au una wasawasi wowote katika safari ya mbeleni, ulinambia kuwa tukianza mradi lazma tuweke kila kitu kisheria kwani isijetokea mwajiri wangu akasema nina utajiri wenye mashaka, ukizingatia kazi zetu zina mazingira mengi magumu

Hatukujuana leo wala jana,tangu uko form three miaka ya 2000, mpaka unakwenda kusoma Sheria Tumain umekuwa mtu mchangamfu sana, uwezo wako darasani ulitosha kabisa kutoa mchango wako kwa Taifa kama ambayo umekuwa mweledi na mchapa kazi mwema. Ulishinda mazingira ya kurubuniwa rushwa, uliheshimu Sana kazi yako, ulinambia kazi Hiyo uliipenda Sana kwani, ukiwa mdogo,babu yako alikuwa ameajiriwa kiwanda cha kahawa huko Bukoba,wakati wa uongozi wa Mkapa, TAKUKURU walizulu kwa babu yako na kumnyanyasa babu yako, huku wakiacha kila kitu shaghalabaghala ndani ya nyumba, hawakionyesha ustaarabu.

Wakaondoka na babu yako ,na unaamini kabisa babu yako HAKUWA NA TUHUMA ZA RUSHWA, tangu hapo ukahaidi kufanya kazi ya TAKUKURU, ukaongeza kwa kunambia kuwa kiukweli licha ya kuitumikia TAKUKURU babu yako hawa kumtendea haki, na hamna Sehemu katika kaz zetu tunashauriwa KUTUMIA UBABE, Kama uliokuwa unaukumbuka alitendewa Babu yako, na kusema ndo maana ULIFANYA KAZI kwa weredi Sana. Ulikuwa rafiki yangu kwa namna ambayo uliniweka huru katika harakat zako.

Hukuonyesha hofu kabisa kuwa KUNA hata Dalili ya kufa muda wowote. Jana 26.1.2020, siku ya Jumapili saa 10:10 asubuh ulinipigia simu kwa bahati mbaya sikuipokea ,na sikukutafuta siku Mzima, leo Juma tatu 27.1.2020,Saa 1:14 Napiga simu nakuta inaongea, badae napata message "call you later" sikushutuka maana nilijua ni mida ya kazi, baada ya muda unatuma message "piga", napiga kwa kuzooea matani yetu nikisema "we Bisho NTONGO" umeishakula, Sauti iliyopokea simu ya KIUME, na ikasema jina Langu "..

vipi Mr Y", nikastuka nikidhani simu anayo mme wake. nikauliza aliyepokea simu "plasidia yuko wapi"?, akasita kidogo alafu akasema yuko BUGANDO, nikastuka nikauliza we nani, Akijibu Mimi MDOGO Wake, Nikauliza anaumwa akasita tena kidogo, Akasema "AMEFARIKI" sikuamini neno hilo kiukweli, baada ya muda nikapiga tena nikajibiwa hivyo hivyo. "MUNGU WANGU" nikapatwa na ganzi hapo hapo, baadae Kweli vyanzo vingine vya taarifa vikadhihirisha PLASIDIA RUGALEMA Kweli amefariki na haijulikani kilicho muua mpaka hapo Madaktar watakopo dhibitisha.

Huko nyuma amewahi nambia ana ATHMA, hata hivyo sijawah sikia akiipa nafasi kubwa kumuadhiri, amewahi nisimulia anavyoweza kuhoji mtu kiasi ambacho mtu anatoa jasho na mwishowe anakiri kosa, amewahi nisimulia alivyombana mwanaume mmoja mpaka akasema ukweli lakin alinisimulia Huyo mtu alikufa kwa pressure (akionyesha kusikitishwa na kifo cha mtuhumiwa huyo, )aliniomba nithuru mwanza anionyeshe mradi wake wa Samaki unavyokwenda vizuri Sana, nami nimuunge mkono, hakutamani kabisa afikishe umri wa kustaafu Akiwa mwajiliwa wa serikali alitaka Afanye Biashara ya kilimo mapema mno, alinambia kadri anavyokuwa kiumri anazidi kuwa na woga wa kuwabana watuhumiwa, lakin la muhimu aliniadithia ambavyo amewahi kuwa na kesi mahakamani, Mara paap akiwa mahakama macho yakapofuka akiamini ni ki KIPAPAI.

Yote hayo yalidhihirisha alikuwa MWOGA wa kufa kama kawaida ya binadam, na leo HATUKO nae hapa duniani,
Nilichojifunza: binadam ni wepesi Sana mbele ya kifo, hamna ajuaye kesho yake, na si Kila kifo kina Dalili ya kukuchukua, kingine ni Kama kilicho mchukua Rafik yangu PLASIDIA R.

Wakat tunamuombea MWANGA wa milele ndugu yetu mpendwa, BASI TUJIANDAE kwa Namna utaweza kuupokea umauti wako au ndugu yako au Rafiki yako muda wowote. naogopa hata kupanga safari kwenda msibani maana Rafiki yangu NDO AMEKUFA.

MUNGU ilaze roho ya placidia Rugalema mahali Pema peponi, naipa pole sana familia yake na watoto wake, na mama mzazi wake.

Tulio hai Leo na wakiristo wenzangu TUISOME SANA ZABURI 35.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana conductor ila je alikua mwana JF au. Pia kuna mengi sio vizuri kuyasema kama vile alimhoji mtu mpk akafa unazan kama ni ndugu yangu mie ntachukuliaje kifo chake. Ila ni kweli unapokua kiumri hofu ya kufa inaongezeka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Life's too short, inasikitisha sana. Japo tumejawa na kiburi na dharau lakini death is inevitable!!

Hapa ndipo siri ya maisha ilipo, na hata hatujui what's next after we are gone! Damn death!!
 
Poleni wafiwa. Mungu awe mfariji wenu. Mwandishi naona unamwandikia kana kwamba atakusikia soma Mhubiri:9.5
"kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.
Mhubiri:9.6
Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote lililofanyika chini ya jua"
Biblia inachotuasa ni kwa tukeshe tukiomba. Soma 1 Wathesalonike:5.2
Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.
1 Wathesalonike:5.3
Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.
1 Wathesalonike:5.6
Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.
1 Wathesalonike:5.17
ombeni bila kukoma. Pia soma
1 Wathesalonike:5.2

ombeni bila kukoma. Cha kujifunza hapa ni kwa mtu akishakufa hukumu yake hutokana na alivyokufa na ni kati yake na Mungu mwenyewe. Kama alikufa na dhambi sisi tulio hai hatuwezi kubadilisha chochote. Hivyo maneno "rip,alale pema peponi,mwanga wa milele umwangazie nk. ni maneno ya kujidanganya na ya kipagani. Tijiandae muda wote tungali hai kwani tukifa hakuna tena nafasi,tukeshe kwani hatujui
tutakufa lini au Yesu wetu atakuja lini. Rejea pia kitabu cha
Ufunuo:22.11
Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.
Ufunuo:22.12
"Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo"
Kitafikia kipindi hapatakuwa na msamaha tena,Roho wa Mungu atakuwa ameondoka na Yesu atakuwa ameacha kazi ya uombezi na kuwa Mhukumu. Tukeshe na kuomba na kila mtu na ajiandae muda wote kwani tukifa hakuna kuombeana. Wafu hawajui neno lolote!

Siku za mwanadamu duniani sio nyingi na zimejaa taabu. Ni kama mvuke, maua ambayo huchanua na kunyauka..........Tujiweke tayari kwakuwa hatujui saa wala siku. Haya ni maandiko ya Biblia takatifu. Mungu akisema amesema lazima itimie. Mungu mhukumu wa haki ndiye ajuaye mahali alikofikia rafiki yako. Poleni sana kwa msiba
 
Poleni wafiwa. Mungu awe mfariji wenu. Mwandishi naona unamwandikia kana kwamba atakusikia soma Mhubiri:9.5
"kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.
Mhubiri:9.6
Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote lililofanyika chini ya jua"
Biblia inachotuasa ni kwa tukeshe tukiomba. Soma 1 Wathesalonike:5.2
Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.
1 Wathesalonike:5.3
Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.
1 Wathesalonike:5.6
Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.
1 Wathesalonike:5.17
ombeni bila kukoma. Pia soma
1 Wathesalonike:5.2
Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.
1 Wathesalonike:5.3
Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.
1 Wathesalonike:5.6
Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.
1 Wathesalonike:5.17
ombeni bila kukoma. Cha kujifunza hapa ni kwa mtu akishakufa hukumu yake hutokana na alivyokufa na ni kati yake na Mungu mwenyewe. Kama alikufa na dhambi sisi tulio hai hatuwezi kubadilisha chochote. Hivyo maneno "rip,alale pema peponi,mwanga wa milele umwangazie nk. ni maneno ya kujidanganya na ya kipagani. Tijiandae muda wote tungali hai kwani tukifa hakuna tena nafasi,tukeshe kwani hatujui
tutakufa lini au Yesu wetu atakuja lini. Rejea pia kitabu cha
Ufunuo:22.11
Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.
Ufunuo:22.12
"Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo"
Kitafikia kipindi hapatakuwa na msamaha tena,Roho wa Mungu atakuwa ameondoka na Yesu atakuwa ameacha kazi ya uombezi na kuwa Mhukumu. Tukeshe na kuomba na kila mtu na ajiandae muda wote kwani tukifa hakuna kuombeana. Wafu hawajui neno lolote!

Sent using Jamii Forums mobile app
Sina cha kuongeza hapo zaidi ya kuzingatia hayo maaandiko YOTE
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom