Pumzika kwa amani Plasidia Rugalema

conductor

JF-Expert Member
May 29, 2013
718
569
Ijumaa ya 24.1.2020,saa 8:15 Usiku ulinipigia simu kuwa Umefika Igoma-Mwanza kuwa unatoka Musoma,mahakamani kwa shughuli kama sehemu ya kazi za mwajiri wako (TAKUKURU), Ulikuwa na Furaha kubwa na jinsi ulivyokuwa unachangamka basi hatukujua kama mauti yako mbioni kukunyakua, sikujua kama Jumatatu ya 27.1.2020 haitakukuta hai,ama haitaisha ukiwa hapa duniani.

Uliahidi tena kunipigia simu weekend tuendeleze mjadala na mawazo ambayo tayari tuliokuwa tumeyaanzisha tangu 31.12.2019 . Maongezi na namna ya mipango haikuonyesha una dosari yoyote ya kiafya au una wasawasi wowote katika safari ya mbeleni, ulinambia kuwa tukianza mradi lazma tuweke kila kitu kisheria kwani isijetokea mwajiri wangu akasema nina utajiri wenye mashaka, ukizingatia kazi zetu zina mazingira mengi magumu

Hatukujuana leo wala jana,tangu uko form three miaka ya 2000, mpaka unakwenda kusoma Sheria Tumain umekuwa mtu mchangamfu sana, uwezo wako darasani ulitosha kabisa kutoa mchango wako kwa Taifa kama ambayo umekuwa mweledi na mchapa kazi mwema. Ulishinda mazingira ya kurubuniwa rushwa, uliheshimu Sana kazi yako, ulinambia kazi Hiyo uliipenda Sana kwani, ukiwa mdogo,babu yako alikuwa ameajiriwa kiwanda cha kahawa huko Bukoba,wakati wa uongozi wa Mkapa, TAKUKURU walizulu kwa babu yako na kumnyanyasa babu yako, huku wakiacha kila kitu shaghalabaghala ndani ya nyumba, hawakionyesha ustaarabu.

Wakaondoka na babu yako ,na unaamini kabisa babu yako HAKUWA NA TUHUMA ZA RUSHWA, tangu hapo ukahaidi kufanya kazi ya TAKUKURU, ukaongeza kwa kunambia kuwa kiukweli licha ya kuitumikia TAKUKURU babu yako hawa kumtendea haki, na hamna Sehemu katika kaz zetu tunashauriwa KUTUMIA UBABE, Kama uliokuwa unaukumbuka alitendewa Babu yako, na kusema ndo maana ULIFANYA KAZI kwa weredi Sana. Ulikuwa rafiki yangu kwa namna ambayo uliniweka huru katika harakat zako.

Hukuonyesha hofu kabisa kuwa KUNA hata Dalili ya kufa muda wowote. Jana 26.1.2020, siku ya Jumapili saa 10:10 asubuh ulinipigia simu kwa bahati mbaya sikuipokea ,na sikukutafuta siku Mzima, leo Juma tatu 27.1.2020,Saa 1:14 Napiga simu nakuta inaongea, badae napata message "call you later" sikushutuka maana nilijua ni mida ya kazi, baada ya muda unatuma message "piga", napiga kwa kuzooea matani yetu nikisema "we Bisho NTONGO" umeishakula, Sauti iliyopokea simu ya KIUME, na ikasema jina Langu "..

vipi Mr Y", nikastuka nikidhani simu anayo mme wake. nikauliza aliyepokea simu "plasidia yuko wapi"?, akasita kidogo alafu akasema yuko BUGANDO, nikastuka nikauliza we nani, Akijibu Mimi MDOGO Wake, Nikauliza anaumwa akasita tena kidogo, Akasema "AMEFARIKI" sikuamini neno hilo kiukweli, baada ya muda nikapiga tena nikajibiwa hivyo hivyo. "MUNGU WANGU" nikapatwa na ganzi hapo hapo, baadae Kweli vyanzo vingine vya taarifa vikadhihirisha PLASIDIA RUGALEMA Kweli amefariki na haijulikani kilicho muua mpaka hapo Madaktar watakopo dhibitisha.

Huko nyuma amewahi nambia ana ATHMA, hata hivyo sijawah sikia akiipa nafasi kubwa kumuadhiri, amewahi nisimulia anavyoweza kuhoji mtu kiasi ambacho mtu anatoa jasho na mwishowe anakiri kosa, amewahi nisimulia alivyombana mwanaume mmoja mpaka akasema ukweli lakin alinisimulia Huyo mtu alikufa kwa pressure (akionyesha kusikitishwa na kifo cha mtuhumiwa huyo, )aliniomba nithuru mwanza anionyeshe mradi wake wa Samaki unavyokwenda vizuri Sana, nami nimuunge mkono, hakutamani kabisa afikishe umri wa kustaafu Akiwa mwajiliwa wa serikali alitaka Afanye Biashara ya kilimo mapema mno, alinambia kadri anavyokuwa kiumri anazidi kuwa na woga wa kuwabana watuhumiwa, lakin la muhimu aliniadithia ambavyo amewahi kuwa na kesi mahakamani, Mara paap akiwa mahakama macho yakapofuka akiamini ni ki KIPAPAI.

Yote hayo yalidhihirisha alikuwa MWOGA wa kufa kama kawaida ya binadam, na leo HATUKO nae hapa duniani,
Nilichojifunza: binadam ni wepesi Sana mbele ya kifo, hamna ajuaye kesho yake, na si Kila kifo kina Dalili ya kukuchukua, kingine ni Kama kilicho mchukua Rafik yangu PLASIDIA R.

Wakat tunamuombea MWANGA wa milele ndugu yetu mpendwa, BASI TUJIANDAE kwa Namna utaweza kuupokea umauti wako au ndugu yako au Rafiki yako muda wowote. naogopa hata kupanga safari kwenda msibani maana Rafiki yangu NDO AMEKUFA.

MUNGU ilaze roho ya placidia Rugalema mahali Pema peponi, naipa pole sana familia yake na watoto wake, na mama mzazi wake.

Tulio hai Leo na wakiristo wenzangu TUISOME SANA ZABURI 35.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pumzika kwa AMANI PLASIDIA RUGALEMA
IMAG0207.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poleni sana wafiwa Mwenyezi Mungu awape nguvu kipindi hiki kigumu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Poleni,tuombe na kusali kila inapobidi,it always comes as fast as lightning,where there is no negotiations,it's just a pick of the soul,and that is the end...
 
Pole sana.

Raha ya milele uwape ee Bwana na Mwanga wa milele uwangazie ndugu zetu Marehemu wapumzike kwa amani. Amina
 
Mimi nna uwezo wa kumuangalia mtu na kufahamu kuwa atakufa hivi karibuni, Pacidia tayari alionesha dalili hizo muda mrefu.


"Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa"

Poleni mnapishi huku mkiwa mmebeba ujinga wa kukosa maarifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiukweli maisha yetu ni mafupi sana sema hua tunajisahaulisha tu kwa kiburi cha uzima. Ndani ya dakika moja unaweza kubadilika jina na kila kitu chako kinaishia hapo. Mungu awatie nguvu wafiwa na amlaze mahali pema rafiki yako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom