Pumzika kwa amani Bibi bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe

Dah, pole Sana aiseeeee ila wewe ni kigego, yaani hadi Bibi anakusihi ukamuone na hujaenda kumuona hadi Amepumzika ndio Unajifanya kuwa na Uchungu! Umekosa baraka aiseee, ulikua busy kiasi cha kushindwa kabisa kwenda? Lakini angekua Demu anakuita hata Kama yuko wapi ungekopa nauli na kazini ukasingizia msiba au ugonjwa! Dah Umeniangusha saana!

Mimi sina Wazazi kwa sasa ila nawashauri nyie Wenye Wazazi au Walezi, jifunzeni kuwapenda kwa Vitendo sio kwa maneno maana siku hawapo mtawakumbuka saana.

Sasa Unaweza kukuta Huyu kalelewa na Bibi yake kwa shida Leo hii hakwenda kumuona hadi Amepumzika!

Pole Sana aiseeeee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimependa comment yako mkuu, ubarikiwe sana
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Elli, umeongea maneno kuntu sana. Na umeongea kwa hisia kali.

Vijana wengi tunakosea sana hapa.
Utakuta tunawapenda wazazi na walezi wetu kwa maneno au wakati hatuna kitu.

Ila tukishakuwa mbali nao tunasahau kuwa hata kwenda kuwaona tu ni moja ya upendo na zawadi kubwa kwao na pia wanafarijika mno.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenena vema mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpwa, Mzazi hata akiwa kichaa! Mpende tu, kuna watu wanatafuta hawana mtu wa kumuita Mama au Baba!

Nilienda home siku hio, Nyumba iko tupu, ni makaburi yamebaki tu! Hakuna furaha ya kwenda likizo Tena..... Dah naomba tuishie hapa!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bibi pumzika kwa amani

Ila bibi kijana wako jana alikua anataka picha za Marehemu Ruge akiwa kwenye jeneza huku akisema mwili utakua na tatizo kisa wapiga picha hawajaruhusiwa kuufotoa,je leo huyu mjukuuu wako atatuletea picha laivu?


Bibi tumeshamsamehe kijana wako ila siku nyingine asilete dhihaka kwenye misiba ya watu.

Duniani tunapita tu
 
Nenda kwenye msiba acha ulofa!
Sent by Diaspora
 
Huyo ni bibi..
Labda angekuwa ni ..." bibie "..angefika speed kali...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…