Pump za maji kwa ajili ya umwagiliaji. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pump za maji kwa ajili ya umwagiliaji.

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Red Giant, Jan 19, 2013.

 1. Red Giant

  Red Giant JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2013
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 8,945
  Likes Received: 5,063
  Trophy Points: 280
  Wakuu naomba mtu mwenye ujuzi nazo anisaidie. Nataka kujua pump yenye uwezo wa kuvuta maji kina cha mita 10 na kumwagilia ekari mbili inaweza kugharimu kiasi gani? Pia nilitaka kujua kama kilimo kwanza wanauza na hizi pump. Natanguliza shukrani.
   
 2. Mu-Israeli

  Mu-Israeli JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2013
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 2,456
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Kuna pump inatumia mafuta (petroli) yenye uwezo wa ku-pump lita 500 kwa dakika.
  Ina uwezo wa kupeleka maji mita 30 (horizontal), na kupandisha maji juu (max. head) mita 20.
  Ni pump ya kichina inauzwa sh.300,000. Ina connection ya bomba la inch 2.
  Kama uko Dar es Salaam, kuna duka liko karibu na stesheni, karibu kabisa na ofisi za TRA stesheni.
  Maelezo zaidi utayapata kwa jamaa webnyewe wanaoziuza hapo dukani.

  Pump yenyewe inafanana na hii hapa (lakini sio hii).
  [​IMG]
   
 3. s

  sambu JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2013
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 45
  Hapa kuna taarifa muhimu zinakosekana. Unalima zao gani- Kila zao lina mahitaji tofauti ya maji. Na utamwagilia kwa njia ipi? Kama ni kwa mirija au kwa mifereji. Na shamba lako liko umpali gani toka chazo cha maji (je kuna mlima? Ukijibu haya itakuwa rahisi kukushauri aina ya pampu.
   
 4. Kubota

  Kubota JF-Expert Member

  #4
  Jan 30, 2013
  Joined: Oct 21, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 60
  Kama vipi nenda TUNAKOPESHA Ltd (kama bado wapo hewani) siku zote huwa wanakopesha pump. Wanazo pump imara sana aina ya JD.
   
 5. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #5
  Jan 30, 2013
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,645
  Likes Received: 1,679
  Trophy Points: 280
  Mkuu nataka kuamini kuwa ulikusudia kuandika/kusema mita 300!
   
 6. Mu-Israeli

  Mu-Israeli JF-Expert Member

  #6
  Jan 30, 2013
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 2,456
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Hapana, hii pump ni ndogo ndio maana bei yake ni ndogo, hivyo inapeleka maji mita 30 tu (horizontal).
  Pum hizi ndogo jamaa wanazitumia kutolea maji mtoni ili kuyapandisha na kuyafikisha shambani. Baada ya hapo, maji yanasambaa shambani kwa mifereji ya umwagiliaji.
  Kuna pump nyingine kubwa zinapeleka maji mita 100 (horizontal) na kupandisha maji juu (max. head) mita 50.
   
 7. Mutensa

  Mutensa JF-Expert Member

  #7
  Jan 31, 2013
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 426
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Hivi kuna kikomo cha kusukuma maji "horizontally"? au hii ni kama unasukuma maji "horizonally" na "vertically"?
   
 8. Mu-Israeli

  Mu-Israeli JF-Expert Member

  #8
  Jan 31, 2013
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 2,456
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Kipimo cha kusukuma maji horizontally kipo. Jinsi umbali (horizontal distance) unavyoongezeka, ndio inahitaji pump yenye nguvu zaidi kusukuma maji.
  Maji yakiwa kwenye bomba ambalo liko horizontal yanahitaji nguvu ya kuyapeleka mbele, hivyo umbali unavyoongezeka ndio mzigo wa maji unapokuwa mkubwa ndani ya bomba, na hivyo kuhutaji nguvu kubwa zaidi kutoka kwenye pump.
   
 9. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #9
  Feb 5, 2013
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 21,657
  Likes Received: 4,525
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 10. MSEZA MKULU

  MSEZA MKULU JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2013
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 3,737
  Likes Received: 4,443
  Trophy Points: 280
  nashukuru wadau kwa kutujuza taarifa hizi za muhimu. MIMI NINAHITAJI KUJUA KAMA NINAWEZA PATA PUMP YENYE UWEZO WA KUVUTA MAJI KILOMETA KAMA MOJA NA NUSU KUTOKA KWENYE CHANZO CHA MAJI. GHARAMA KWA UJUMLA PAMOJA NA PIPE NDEFU KIASI HICHO NI SHILINGI NGAPI? NATANGULIZA SHUKURANI.
   
 11. m

  mgiriki Member

  #11
  Mar 2, 2013
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Jamani mmi nina shamba liko maeneo ya hai masama rundugai, shamba hili linataka pamp ili uweze kupandisha maji kutoka mtoni hadi shambani na mto huo haukauki maji. Naomba mweye uwezo wa kuapata pamp na mipira ya nch 4 tuwasiliane kwa mob: Tukalime tujikwamue na umasikini
   
 12. f

  f2rk JF-Expert Member

  #12
  Mar 7, 2013
  Joined: Jan 19, 2013
  Messages: 278
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Rundugai! ekari gani? ubia unakuwaje?
   
 13. f

  fukunyungu JF-Expert Member

  #13
  Mar 7, 2013
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 724
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35


  Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
   
 14. Whisper

  Whisper JF-Expert Member

  #14
  Mar 7, 2013
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 502
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Guys, somo zuri sana. Nawafuatilia kwa makini kwani na mimi napata somo. Thanks for your valuable inputs.
   
 15. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #15
  Mar 7, 2013
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Wakuu tupo pamoja somo muhimu sana hasa kwetu wajasilimali.
   
 16. f

  fukunyungu JF-Expert Member

  #16
  Mar 10, 2013
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 724
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Rundugai ndo wapi?
   
 17. M

  Mateshi Member

  #17
  Mar 12, 2013
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Hongereni sana kwa wale mnaotaka kujiunga na Kilimo cha umwagiliaji....Mimi sina utaalam sana ila naweza nikachangia kitu kwenye hii mada...jaribu kupitia hizi pump below..ni nzuri sana
  1.WT40XK3C...Honda trash pump kama shamba lako ni kubwa...4inch
  2.Honda WT30XK4C...3inch
  3.Honda WH20X high pressure water pump...2inch
  4. Honda WB30...3inch
  hizo pump kuna ya 4m hadi ya 1m..hizo ndo pump nzuri kwa mashamba ya kuanzia ekari tano..Mashamba yanamwagiliwa kwa mifereji..yaani unakuwa na point moja(center) ambapo utakuwa unapump hayo maji, afu from there unayasafirisha kwa mfereji..hiyo point jitahidi iwe katikati au sehemu yenye muinuko zaidi katika shamba lako..
  Unaweza kuzipata hizo pump kwenye duka la Honda lililopo kariakoo, lipo karibu na zilipokuwa ofisi za scandnavia..
  Kumbuka, kama unataka kufanya kilimo cha umwagiliaji kitu cha kwanza muhimu ni ubora wa pump..nakushauri achana na pump za kichina kama pesa yako ni yakuunga unga maana zinahitaji maintenance za mara kwa mara...they look cheap but they r expensive...
  Ukiweza pata pump za Diesel ni much better
   
 18. Kubota

  Kubota JF-Expert Member

  #18
  Mar 13, 2013
  Joined: Oct 21, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 60
  Kwa umbali huo unaweza kupata pump hiyo maana hakuna lisilowezekana. Cha muhimu kuzingatia si umbali pekee bali kiasi cha mwinuko kilichopo toka kilipo chanzo cha maji! Kama ni mwinuko mkubwa utahitajika kuwa na pump yenye nguvu sana. Siyo rahisi kukadiria bei ya pump kwa vile inategemea na mwinuko. Kwa umbali huo na mwinuko huo jiweke kwenye makadirio ya Millioni 2 hadi 4 kwa kuzingatia figure za Mkuu Mateshi hapo juu. Kwa umbali huo unahitajika kuwa na Tsh Milioni 1.5 kwa kununua mpira wa 3". Au unaweza kutumia pump ndogo unajenga tanki kubwa kwenye chanzo cha maji, pump inalijaza tanki hilo na ule mkandamizo wa maji kwenye tanki unayasukuma maji kwenda shambani kwako. Pump ndogo kujaza tanki zinauzwa laki 3/4. Ila mziki uko kwenye kutengeneza tanki ambapo utajikuta umerudi kule kule sawa na kununua pump ya bei kubwa.
   
 19. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #19
  Mar 14, 2013
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mkuu pump gani zinafaa kwa kisima cha chini kama 80m-100M? kwa ajili ya umwagiliaji?
   
 20. MSEZA MKULU

  MSEZA MKULU JF-Expert Member

  #20
  Mar 15, 2013
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 3,737
  Likes Received: 4,443
  Trophy Points: 280
  mkuu nashukuru sana maana ni kitambo nimekuwa nikisubiri feedback kama hizi. ngoja nikajaribukufanya detailed research then niangalie ni njia hipi ni sahhi zaidi katika kufanikisha hili.
  ahsante. Maana nikikuwa nahofu juu ya bei ya mpira utakao range umbali ambao niiukadilia.
   
Loading...