CAMARADERIE
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 4,419
- 1,929
Kahama tumepoteza kwa wachimba dhahabu, Selous tumepoteza kwa ajili ya uranium, Ifakara na Rufiji tumeuza kwa walima jathropa ( whatever) sasa rukwa na mpanda kwa hao wazungu. Loliondo ndo kapewa mfalme wa Qatar, Wakorea nao wananyemelea maeneo. Tunakwenda wapi? Tunafanya nini? Kwa nini?
Walahi hii inchi inauzwa hivi hivi kidogo kidogo wajukuu watabaki na nini jamani?
Watanzania tunafaidika nini, kizazi kijacho kitafaidika nini?
Duh, hivi viongozi wetu wana uchungu na nchi hii kweli au ni usingizi na udenda tu.
Utafikiri sie ni machizi waliopata mirathi.......wao kuuza na kuuza mwisho wankuwa ombaomba na kujisifu vijiweni ''tulikuwa na nyumba mtaa wa Congo tukauza 850''