gnassingbe
JF-Expert Member
- Jun 14, 2015
- 4,826
- 3,585
Umenena Mkuu, Mzee wangu kastaafu mwezi wa nne tar 18 mwaka huu, hadi leo hajapata pensioni yake PSPF, mimi mwenyewe niliacha kazi tangia januari nimefuatilia michango yangu nssf, hadi sasa sijapata! Yani haya mashirika ni hopeless kabisa!
Mkuu jaribu kuelewa tunachokilalamikia hapa, usilete ushabiki tu! Mimi binafsi nimepewa majibu hayo ya kusikitisha na hao PSPF. Kwanini nidanganye hapa?
Ni kweli kabisa mfuko wa PSPF una hali mbaya kifedha. Nimethibitisha hili hivi karibuni, baada ya kuwasiliana nao ili nijue kwanini wamekua wakimzungusha mzee wangu katika kupata mafao yake, baada ya kuwa amestaafu kwa muda mrefu sasa!
Bila kutafuna maneno, nilijibiwa kwamba fedha hakuna, wanasubiri hazina itakapopeleka makato ndipo waweze kulipa. Na kwamba haijulikani ni lini, ila niendelee tu kuwasiliana nao kila nitakapopata nafasi.
My take: Kwa kweli hali ni mbaya, Serikali inabidi ichukue hatua haraka iwezekanavyo, ili kunusuru wazee wetu hawa!
Labda niongezee au nifafanue pale ulipoishia. Kwa PSPF Kuna Matatizo mawili, ambayo yote chanzo ni Serikali yetu iliyoko madarakani, na nitaelezea kama ifuatavyo;-
1) Pre-'99
Mwaka 1999 serikali iliuomba huu mfuko kuwachukua staff wake wengi tu na kuwasajili kwenye mfuko kana kwamba walikuwepo toka zamani (kabla ya (1999). Hivyo basi mfuko huu uliamua kuwaingiza kwenye database yake hata wale ambao hawakua wamechangia. Yaani mfano mtu kaanza kazi Serikalini tuseme mwaka 1985 na akachangia mafao yake hazina Mpaka mwaka 1998, mtu huyu alihamishiwa PSPF mwaka 1999 na labda kama atastaafu mwaka 2000, PSPF watamlipa mafao ya kuanzia mwaka 1985 ingawa kwao kachangia kuanzia 1999 tu.
Makubaliano haya yalikua kama ni Mkopo ambao hazina/serikali ingedaiwa na huu mfuko sababu mfuko unalipa mafao ambayo makato yake haukuyapokea, na toka ahadi au makubaliano hayo ya deni yafikiwe huo mwaka 1999, serikali haijawahi kuilipa huu mfuko ingawa mfuko umeendelea kuwalipa wastaafu mafao yao yote pamoja na pensheni Mpaka mwaka jana.
2) Monthly Salary Deductions
Hapa napo Kuna delays. Toka January mwaka huu, serikali imeshindwa kupeleka makato inayowakata wafanyakazi wake kwenye mishahara yao. Wewe ukipokea Pay slip yako inaonesha umekatwa PSPF ila in actual sense hiyo hela haijaenda bado kwa watu PSPF.
Deni la kwanza ambalo ni historical linatokana na fact kwamba ni kubwa mno, zaidi ya 1 trillion, hivyo serikali inayolia deficit kwenye bajeti yake kuondoa hela kama hii ni tatizo. Deni hili aliliacha mkapa, na dalili zote ni kua JK nae ataliacha, ingawa likiwa limeongezeka.
Na deni la pili nalo ni hiyohiyo deficit ya serikali, maana hata mishahara yenyewe ni kwa manati ingawa inalipwa.
Data hizi ni kutoka Hazina ambao ndio wadaiwa, hivyo hazina shaka kabisa

Ndo mtulipe
Ndugu yangu alikuwa anashughulikia mafao yake wiki ya juzi wamemwambia hundi ipo tayari ila pesa hakuna, bi mkubwa wangu kastaafu toka mwaka jana mwanzoni hadi leo hajapata mafao yake mbaya zaidi hata mwajiri wake ambaye ni manispaa anapaswa amlipe nauli hadi leo wanasema hawana pesa na hawajali kabisa hizi halmashauri hizi watendaji wake wanatia hasira
Kwan nawe unadai!!! Pia mie cpo huko bana ni wajamaa wa MK ndo wamesema
Toa kitu kidogo uone utakavyohudumiwa fasta.
We Ulidhani MK nini kwa mfano? Halafu tutafutane basi wewe aiseeMK?
MK bar au?
hebu refusha maelezo.
Sie wengine vilaza
Mkuu,Ahsante kwa ufafanuzi wa kina mkuu, kuna watu humu wamezoea kupotosha kila ukweli kwa maslahi yao binafsi na waliowatuma. Bila kupima kwanza hasira wanazoweza kuziibua kutoka kwa wengine, ambao kimsingi ndio wahanga wa haya mambo!
Nafikiri sote kwa pamoja tuendelee kuisihi Serikali yetu ifanye linalohitajika kwasasa, ili kuwaondolea adha hii wazee wetu. Kwa kweli inatia uchungu sana, mzee anapoishi kwa matumaini, asijue ni lini hasa atafanikiwa kupata haki yake. Bado tuna imani na Serikali yetu, na kwakua imekua ikijitambulisha kwamba ni SIKIVU, MAHILI NA MAKINI, huu ndio wakati sasa wakudhihirisha hayo kwa vitendo.
Ha ha ha Mama samia si ana matrillioni ya kugawa vijijini mwambieni awakopeshe PSPF
Sasa hizi ahadi zamagufuli anategemea kuzitimiza na nini ilihali JK ashakopa mpk mifuko ya ndani imeisha
We Ulidhani MK nini kwa mfano? Halafu tutafutane basi wewe aisee
Sema tukiwa tuko wenyewe tuonane.
Maana kila siku Twittet uko na mkeo na mimi niko na mme wangu
Kesho njoo bila mkeo nami nitamuaga mume wangu kuwa naenda kwa shangazi kule Mbezi mwisho, afu tukutane.
Au njoo Pm
Hahahaa! Ninyi mmeugeuza uzi wa watu kuwa wa kimahaba, eti?
wapuuzi kama nini