PSPF tekelezeni mnayoyatangaza bila longolongo

saivan

Member
Dec 1, 2016
15
8
Nawashauri PSPF kuwa waungwana kutekeleza huduma wanazozingaza kwa wakati bila usumbufu kwa wateja wao kwani wana shida ya kuweka vikwazo vinavyoweza kuwakatisha tamaa wateja.

Mfano fao la uzazi limekuwa na usumbufu mkubwa hasa mikoani.
Pia ajirini watu competent huko mikoani au waliopo waelekezeni kutoa huduma kwa wepesi huu sio muda wa kulala tena.
MFANO Pwani, Lindi, Tabora, Tanga nk
 
Mtoa mada haujawa specific wewe huo utafiti uliufanya lini ukagundua kuwa PSPF ina wafanyakazi incompetent? Maana umetaja mikoa bora hata ungetaja mkoa mmoja hoja yako ingekuwa na mashiko.
Achana na hoja nyepesi kama hizo.
Lakini pia kama ni hoja za ushindani, ni ushindani wa kijinga you can not win the market kwa kumchafua competitor/competitors kwa hoja nyepesi kama ya mleta mada hapa.

Kajipange halafu urudi tena, hii tumeishtukia unajaribu kuwatengenezea PSPF negative publicity.
 

Pia hoja nyepesi kama hizi si za kuleta kwenye hili jukwaa.
Hili ni jukwaa la siasa. Peleka hoja yako hii iliyokaa kishilawadu kwenye jukwaa la umbea kule utaeleweka ila sio hapa. Pia uwe na valid evidence ya findings zako.
 
Screenshot_2017-04-01-11-31-35.png


Kwa hoja zako zilivyo unaonekana hujui ushindani. Maana hoja zako naona ni kuiponda PSPF maana thread zako zinajionyesha.
Huo ni ushamba.

Umejiunga JF tarehe 1 Dec. 2016. Umeanzisha thread tano (5) tatu kati ya hizo zinahusu PSPF.

Mbili kati ya hizo unafanya comparison PSPF vs LAPF. Ni kichekesho kulinganisha The giant (PSPF)yenye wanachama takribani Laki nne na ushee almost tano na kibushuti (LAPF) chenye wanachama ambao hawajafika hata Laki na ishirini. Ni sawa na kulinganisha RANGE ROVER VOGUE na Kibajaji.
Na declare interest, Mimi ni mwanachama wa PSPF na naijua vizuri sana PSPF. Kama kuna mapungufu ni yale ambayo yanapatikana katika kila taasisi. Ambayo ndo hutoa fursa ya kufanya improvement.
PSPF don't take serious watu wa namna hii. Ila kwa mtazamo wangu huyu atakuwa ni miongoni mwa wafanyakazi wa LAPF amabye ndie atakayekuwa anaaminiwa kuendesha hizi propaganda za mtandaoni, bahati mbaya ana akili za KIBASHITE.
Wanachama wenu tuko pamoja nanyi na tunawahakikishia kuwasapoti kwa namna yoyote ile.
Sasa kwa kuwa huyu jamaa anawafanyia hivi wala PSPF msihangaike nae/nao.
Mimi binafsi ntaanza kuja na Data zinazoihusu LAPF namna wanavyowalaghai waajiriwa wapya kwa ahadi ya huduma wasizokuwa nazo. Mfano mkopo wa nyumba za makazi LAPF husema wanatoa, ila mwanachama akienda humwambia aende WATUMISHI HOUSING COMPANY (WHC).
 
Pspf kwa nini hawataki kulipa watu hela zao?

Inachukua muda gani kwa shirika hili kulipa wadai?

Watu wanafuatilia mwaka mzima pesa hawalipwi,

Nadhani wana matatizo makubwa
 
Back
Top Bottom