Mwalimu NYerere alitoa elimu bure, matokeo yake baada ya miaka 20 nchi ilitembelea magoti.
CHADEMA (Mh Slaa) japo ya kujua hilo bado ilisisitiza kutoa Elimu bure kwa watanzania wote ili ishinde uchaguzi 2010, lakini ikaanguka. Hii ni kutokana na ueleo mkubwa wa watanzania na kuelewa kuwa hizo ni PROPAGANDA ZA UONGO.
Nasubiri majibu yenu kabla sijaendelea na sekta nyingine.
Naanza kwa kukuambia hiyo elimu uliyonayo ni sumu haikusaidii kitu.
Wewe nadhani ni mchumi zumbukuku usiyejua taratibu za pato la mahali kama DSM, Kili linavyogawanywa mara linapokusanywa. Kwa sababu hali siyo hivyo kwa taratibu za makusanyo ya mapato.
1. Wakusanyaji ni halmashauri na TRA. TRA hupeleka makusanyo hazina kwenye kapu moja ambalo baadae mgao unafanywa na watawala wa CCM kwa vipaumbele vyao. Kwa upande mwingine halmashauri hupanga matumizi yake kwa uwezo wake wa makusanyo pamoja na kuingiliwa na seikali kuu. (Serikali kuu iliua serikali za mitaa na bado inazishikilia kama luba)
2. "
Mwalimu NYerere alitoa elimu bure, matokeo yake baada ya miaka 20 nchi ilitembelea magoti". Kauli hii ni dhahiri inaonyesha ulivyo mvivu wa kufikiri. Kwa taarifa yako ilipovunjika jumuiya 1977 Tanzania tulikuwa tunaongoza kielimu na kiuchumi. Hayo kwa taarifa yako na wapuuzi wenzio yalikuwa sababu mojawapo ya uvunja jumuiya. Njoo kwenye Azimio lenu la Zanzibar lililofuta vipaumbele vya kitaifa na kuweka vipaumbele vya kuvunja maadili. Ulitegemea elimu na uchumi kwenye mfumo holela vizingatie dhana ndogo ya msingi ya kutumia rasilimali kwa kipaumbele cha kitaifa? Mwalimu Nyerere uliye na usongo naye kwa kutoa elimu bure kabla hajafariki aliasa kuwa kweli kuna aliyoyakosea, lakini mazuri yalikuwepo wenzie, wewe na wapuuzi wenzio watawala wachumia tumbo hata yale mazuri mmeyafilimba.
3. Kwa upeo wako mfupi na mahali ulipo unaona ya CDM hayawezekani; kwa bahati mbaya sana huzungumzii mafanikio mbadala kwenye yaliyotajwa kama elimu bure, nafuu ya gharama za ujenzi na utawala wa sheria ambavyo kwa sasa ni bidhaa adhimu.
Nikupe somo kidogo
1. Rasilimali za taifa zinasimamiwa kihuria na kiholela mifano madini, watu, shughuli zote za uchumi na mbaya zaidi ombwe la uongozi la CCM.
2. Ili kuwe na mafanikio katika kufikia elimu na uchumi bora tuache majaribio. CDM hawatafanya majaribio watafanya kweli kama wanavyofanya kweli. Watawala baada ya mwalimu hawakujifunza cho chote toka kwa awamu yake. Walianza majaribio yaliyoshindwa ndiyo maana mtu ama wewe huoni uwezekano wa watu makini ndani ya CDM kutimiza yaliyo kwenye ilani yao. Pia ndiyo maana wewe na wapuuzi wenzio mnahofu ya mabadiriko kwa sababu ndani ya dhamiri zenu mnasutwa na dhulma, ufisadi ambao mnahofu mtapatilizwa
3. Utawala huu na CCM ni batili wenye akili na hekima wanajua. Katika hali hiyo ni sawa na mwamba ngozi anayevutia kwake badala ya wapiga makasia wanaopeleka chombo pamoja. Nina maana baadhi yetu tunaotawaliwa hatuoni chembe ya jitihada ya kitaifa kuendelea pamoja; wewe mwenyewe tafuta pengo la walionacho na wasionacho katika kila kona.
Wimbo wenu wa Maisha Bora kwa kila Mtanzania umeitikiwa na Bora Maisha kwa kila Mtanzania, ule mwingine wa ARI MPYA, NGUVU MPYA NA KASI MPYA YA UFISADI nao umedhihirisha upuuzi unaokinzana na ukweli.
Kwanza una mapungufu ya uelewa wa lugha unapotumia neno propaganda, wenye propaganda ni nyie mlioshindwa kutekeleza majaribio yenu.
Halafu unazungumza sekta zingine ambazo ni za kufikirika kwa sababu hata Rais wako dhaifu hajui maana ya sekta. Mfano mara wachanganye sekta ya elimu na sekta ya elimu ya juu, mara utamaduni nayo ni sekta, mara benki ni sekta. Hiyo yote inatokana na kutafuta umaarufu kwa kwadanganya watu kwa nahau. Huna sekta nyingine labada sekta ya Lumumba
Kwa sasa huu mjadala wewe unatafuta pa kutokea ila tafakari na chukua hatua kwa sababu kwa sasa hata uongo wo wote ukisemwa na CDM watu wataona ni kweli kwa sababu watawala na chama tawala WANANUKA