PreGE2025 Project CHAUMA itafeli mapema sana kama ilivyofeli Project G55

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
372,655
Reaction score
863,523
Mafioso wana kaulimbiu yao inasema usifanye jambo kwa kukurupuka wala kwa shinikizo maana hutafaulu kutokana na makosa mengi ya kiufundi.

Katika hali ya kuchanganyikiwa baada ya kushindikana kuuharibu uchaguzi wa CDM, plan B ya CCM ikawa ni kulitumia kundi lililoshindwa.
Njaa haina baunsa.. Watu wakajaa kwenye mfumo, wakajazwa shekeli na ufadhili wa kuunda G55.. Hili likatikisa kidogo tu kabla ya kukataliwa na hadhira
Halikuwa na maandalizi
Halikuwa na mfumo
Halikuwa na ajenda
Halikuwa na utararibu
Halikuwa na maono
Na mbaya zaidi asilimia 99 ya wajumbe walikuwa wa asili moja

Likabaki kama kundi sogozi la umbea fitina na majungu.. Kwakuwa halikuwa na ajenda wala maandalizi.. Umbea ule na majungu yale yakawarudi na kuanza kushutumiana na kutoaminiana tena..

Kwasasa linapumulia mashine baada ya wengi kujitoa.. Ni kama limesambaratika

Baada ya kugundua hilo kosa kubwa la kiufundi ikaletwa sub project nyingine ya viongozi mbalimbali kujiondoa CDM

Hawa wameahidiwa mengi ikiwemo kupata platform ya kujiweka busy!
Project CHAUMA ndio inafuata.. Hapa pamewekezwa pesa nyingi bila mikakati ya kueleweka .. Hapa ndio litakuwa jalala kuu la wale wote kutoka CDM walio na watakaokubali kuchuuzwa kwa bei ya mnada wakiwemo wale mabaki wa G55.

Project CHAUMA itafeli pengine hata kuzidi project G 55 kwakuwa ni wapigaji watakuwa wamekutana na masikini waliojaa majungu fitina na kijicho

Wawakilishi wa wafadhili wanajipigia hapo.. Wawakilishi wa maskini nao wanajipigia hapo hapo! Mwisho kitakachowafikia maskini ni mkia wa mbuzi.. Na vita ya anguko kuu itaanzia hapo🤣
Your browser is not able to display this video.
 
Mkuu, naskia Janabi ameshinda huko, itabidi tuandamane mana huko Uswisi napo hakuna tume huru ya uchaguzi ndo mana jamaa Kashinda 😂
 
Wamefirisika kisiasa hao MTU mwenye potential na uwezo mkubwa kisiasa na kijamii hawezi kujiunga CHAUMA haijalishi amepewa ahadi gani.


Kama alivyosema Mchungaji Msigwa kuwa G55 hawana ushawishi wowote na amewashauri waamie Ccm.

Pia katika hilo kundi ukimtoa Salimu Mwalimu hao wengine wanapoteza muda kwakuwa hawana ushawishi wowote .

Kinachowapata G55 ndo kilimpata Marehemu Captain Komba kuamini kuwa wao wameibeba chadema na kusahau hauwezi kuwa Mkubwa kuizidi taasisi iliyokupa huo ukubwa.

Captain Komba Alikopa mapesa kibao na kuanzisha miradi kibao akiamini hakuna CCM bila yeye kila alipodaiwa marejesho alitaka Ccm imlipie na baadae yakatokea yakutokea.

G55 Bila shaka ni kakikundi ka watu wachache ambao waliamini kabisa kuwa wataendelea kupata ulaji CDM na kunufaika mambo yote ya CDM.

Ila ndo hivyo mambo yakaenda kinyume.
 
ilishafeli tayari chauma ubwabwa
 
excellent analysis!

hapo ni TAL anayewasumbua alafu yupo Jela, ngoja atoke sasa.
 
Mrema alikuwa anaandaa ajenda baada ya kumaliza kreti ya serengeti lager huku Mchome akiwa amshepewa vitu. Hapo unategemea watoke na ajenda gani?
 
Hamna project humo - kwanza washaanza kukamatana mashati kisa mgawo haufiki kama ilivyotakiwa kuwa.
 
Mrema alikuwa anaandaa ajenda baada ya kumaliza kreti ya serengeti lager huku Mchome akiwa amshepewa vitu. Hapo unategemea watoke na ajenda gani?
Hahahahaaq
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…