Profile Company:Azam Media Group

Kipaji Halisi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2012
Posts
2,280
Reaction score
1,366
nimetafuta kujua shughuli zao kabla sijaona
cjui wana uzoefu kiasi gani katika mambo ya Media.?hasa mpira..?

mwenye website anipe link..
 
Mkuu si kila kampuni lazima iweke profile yake kwenye mtandao, kama uko serious kabisa kuona profile yao nenda BRELA.
imefanya kazi ipi mbp tujiridhishe kuwa ina uwezo wa kuonesha mpira live..?
 
imefanya kazi ipi mbp tujiridhishe kuwa ina uwezo wa kuonesha mpira live..?
Mkuu kwani tatizo liko wapi, mpaka hapa TFF, Vilabu na kamati ya ligi hawana cha kupoteza, siku zote ligi ilikuwa haionyeshwi na hakuna kilichoharibika na wala vilabu hawakupata hela; Azam wametoa hela na ligi wanataka waonyeshe ili waingize hela wao sasa hapo wewe unaathirika vipi endapo watashindwa kuonyesha? Ni kama mtu anataka kuja kununua mahindi kwako ingawa hujawahi kuona akiwa na kifaa cha kubebea hayo mahindi lakini akakwambia mimi nitakupa hela na muda ukifika nitakuja kuchukua hayo mahindi, hela umeshapata kazi inakuwa ni kwake kuja kuchukua hayo mahindi asipochukua wewe huathiriki na chochote. TFF, kamati ya ligi na Vilabu (isipokuwa Yanga na Manji) wanachotaka ni hela na Azam wametoa, sasa mlitaka waseme tunataka kwanza tuone mkirusha matangazo ndo tuwape hii Zabuni wakati wenye kurusha matangazo tayari hawana uwezo wa kutoa hizo hela?
 
nimetafuta kujua shughuli zao kabla sijaona
cjui wana uzoefu kiasi gani katika mambo ya Media.?hasa mpira..?

mwenye website anipe link..

Nipe website za mama lishe ambao ndio wanaolisha vibarua wote nchini, wakiwemo wajenzi wa barabara na wabeba zege. Unataka kuanzisha zengwe la kitoto sana..
 
Nipe website za mama lishe ambao ndio wanaolisha vibarua wote nchini, wakiwemo wajenzi wa barabara na wabeba zege. Unataka kuanzisha zengwe la kitoto sana..
hahahahahahaha...we mie sina ttz ..cz najua shida yako?..
 

umeeleweka...ila hujajibu swali langu..ikiwa kwenye harusi tu mpiga picha mnataka muone picha kabla hamjapitisha kwenye kamati zenu...
 
umeeleweka...ila hujajibu swali langu..ikiwa kwenye harusi tu mpiga picha mnataka muone picha kabla hamjapitisha kwenye kamati zenu...
Mkuu mpiga picha ni tofauti maana yeye atapewa hela na maharusi watataka hizo picha, lakini ingekuwa kwamba yeye anatoa hela za kuwapa maharusi na wanakamati wote ili apewe kazi ya kupiga picha nani angehitaji kuona picha zake, watu wangelamba hela halafu wamsubiri siku ya sherehe aje kupiga hizo picha.
 
unajua kuwa star tv ilikua na mkataba wakuonesha hii ligi kuu yetu..na walishindwa hata zile mechi za dar ?au hata zile za mwanza?...star tv ambayo ni tv yenye coverage sehemu kubwa ya nchi?..na hata wakionesha ilikua madudu tu.... jiridhishe mwenyewe...usikurupuke mkuu...je azam akikuuzia king'amuzi halafu usione mechi ya simba na rhino tabora...?au azam na kagera bukoba ..utasemaje?....kumbuka sababu iliwafanya star tv kushindwa kuonesha mechi zote ?
 
Star TV walikuwa na mkataba wa kuonyesha mechi za Azam na wao walikuwa wanalipwa na timu pia iliyokuwa inacheza na Azam na yenyewe ilikuwa inapta mgawo, tena walianza katikati ya ligi.

Mkuu hata kama wangekuwa washafanya kazi na ukaiona, hiyo sio uthibitisho wa kwamba mechi zote utaona, kuna vitu vingi ambavyo vinaweza kusababisha mechi ikashindwa kurushwa live.
 
kumbe naongea na mtu mwenye kumbukumbu ndogo..hebu uliza vzr hicho unachosema ni cha mwaka jana tena mechi tano tu...
 
kumbe naongea na mtu mwenye kumbukumbu ndogo..hebu uliza vzr hicho unachosema ni cha mwaka jana tena mechi tano tu...
Basi mwenye kumbukumbu kubwa ngoja nikuache uendelee kukumbuka profile ya Azam Media Group.
 
Asipokuja kuyachukua hayo mahindi, mwakani utahifadhi wapi mahindi mapya? Ukiyawacha yaozee ghalani atakugeuka kudai hela yake, utakuwa nayo tu? Ndio maana aposaye huulizwa kwanza anakoishi kabla ya kukubaliwa! Au kuna ulikoona kinyume cha hivyo? Kama wapo, basi hiyo Azam TV iachane na uoneshaji wa Ligi, documentary ya maajabu hayo itawaingizia kipato kuliko hicho cha kuonesha ligi, maana itakuwa ni timeless masterpiece!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…