TANZIA Professor James Shaba afariki dunia. Alifanyia postmortem mwili wa Hayati Sokoine

He


Prof Shaba, alikuwa mtu muungwana mno. Hakuwahi kuwa na majivuno ya aina yoyote, a very simple man, mpenda utani na always kicheko kipo mdomoni mwake. Pia alikuwa Mwalimu mzuri sana katika fani yake. Alikuwa na marafiki wa cadre zote hasa wahudumu ambao alipenda kutaniana nao. Nakumbuka ofisi yake pale Central Pathology Laboratory (Histology) alikuwa hakosi wageni wa kwenda kumsalimia na kupata matibabu.

Tuliwahi kumuuliza kama haogopi cancer ya mapafu kutokana na uvutaji mwingi wa sigara akajibu kwani nikifa kwa malaria mapafu yangu yatakuwa na kazi gani?


Pumzika kwa amani Profesa James Shaba, Nguli wa Pathology.
Thats the Prof Shaba I know, kwa mara ya kwanza tulionana katika mazingira nimeeleza huko nyuma, tukawa na maongezi mazuri sana yaliyofanya nisimsahau, he left me a good impression.
 
Yes they are brothers, na wana Dada yao kifaa kweli kweli!, Mzee Mayalla akiwa RSO wa Mtwara, (Wazee wa Kisukuma hawazeekagi), si macho ya Dingi yakaispot, kufunga kufungua kabinti kakajiriwa Idara, mara paap!, kidume hicho!, kikapewa jina la ..., Dingi akahamishiwa Mwanza, huko ikamkuta ile soo ya 1976!, baada ya soo kuisha 1980 si dingi akatia timu kumdai mwanae!, ndipo akaambiwa hao ni wa Makua, ni matrilinier, watoto ni mali ya Mama na wanatumia jina ubini wa kikeni!. Hata che Nkapa ni ubini wa kikeni!. Katika vitu vingumu Msukuma kuelewa ni damu yake kuibiwa na Mwanamke!. Hivyo mimi tuna undugu na kina Shaba, huyo dogo wetu tutamsaka kumkomboa tumrudishe Usukumani!.
P
Mwananzengo, mazee alikuwa sharp!
 
Pamoja na yote postmortem ya Edward Moringe Sokoine hakuandikwa au kuwekwa wazi.

Na ndiyo maana wanae walipoamua kuhamisha mwili pale ulipozikwa ulisimamiwa na wabeba mtutu.

All in all asingewezza kupingana na Mwalimu
Kwa sasa siyo siri!
Word of mouth(majunguuuuz) ni kwamba ajali ya Edwadi aligongana na Shaba, maana alianza kuwa much know kuliko wajuvi wa kisasa.
 
Prof Shaba ninamkumbuka kuwa Ni MTU wa huruma Sana na ubinaadamu uliopitiliza, Ni kwamba alikuwa kwenye kazi maalumu nje ya Dar na ikatokea yeye kupangwa pia kusimamia mitihani ya wanafunzi (M.A/Clinical officers), mwanafunzi mmoja alikamatwa Vibaya na wakataka kumfukuza chuo, Prof alitetea utafikiri ndugu yake na mwisho Yule kijana akapewa supp ya mwaka na mwisho ikaja kutiki, RIP Prof!
 
Yes they are brothers, na wana Dada yao kifaa kweli kweli!, Mzee Mayalla akiwa RSO wa Mtwara, (Wazee wa Kisukuma hawazeekagi), si macho ya Dingi yakaispot, kufunga kufungua kabinti kakajiriwa Idara, mara paap!, kidume hicho!, kikapewa jina la ..., Dingi akahamishiwa Mwanza, huko ikamkuta ile soo ya 1976!, baada ya soo kuisha 1980 si dingi akatia timu kumdai mwanae!, ndipo akaambiwa hao ni wa Makua, ni matrilinier, watoto ni mali ya Mama na wanatumia jina ubini wa kikeni!. Hata che Nkapa ni ubini wa kikeni!. Katika vitu vingumu Msukuma kuelewa ni damu yake kuibiwa na Mwanamke!. Hivyo mimi tuna undugu na kina Shaba, huyo dogo wetu tutamsaka kumkomboa tumrudishe Usukumani!.
P
Lakini Paskali uko muwazi Sana. Yaani hata Stori za Dingi wako unazitoa humu? Hongera Sana kwa Hilo.
 
Poor you!
Una tatizo linakusumbua, linaweza kuwa phsycological.
Hunifahamu wala sikufahamu, hivyo nijigambe ili iwe nini haswa!

Mambo niliyoweka hapa pengine wewe bado hujazaliwa na kama ulikuwa umezaliwa basi ni kinda usiyeweza ku comprehend matatizo ya wakati huo.
Nashukuru kwa member aliye post kuwa kuna kitu amejifunza kutokana na andiko langu, na kuwa limemsaidia kwenye research yake.


Nikutonye tu kuwa, watu tunafahamu mengi mengi zaidi ambayo hatuthubutu kuyaweka hadharani kwa mustakabali wa nchi hii na vile vile usalama binafsi.
Tuna vifua!

Dr Shaba musimwone kuwa alikuwa mjinga kukaa kimya na kuongea only in parables.

Unapoanza kwenda personal on historical facts ambazo wengine wameziishi, tatizo liko kwako.
Ni sawa na kuanza ubishani na mtoto ambaye hata meno hayajaota.
Nimekwisha kueleza haupo makini hata kidogo katika maoni yako.
Hapa unadai hunifahamu, na wakati huo huo unajifanya wewe mjuaji wa hayo mambo kuliko ninavyo yajua mimi.

Tatizo ni kuwa huna kumbukumbu na wala hujishughulishi kutaka kujua huyo unayejibishana naye rekodi yake ipoje humu JF, ili usiparamie tu kumpachika majina kwa kujipa wewe ujuaji zaidi ya mambo unayodhani yeye hayajui.

Hapa unataka kutumia umri wako kulazimisha watu waamini unayoyajuwa wewe, bila kujali huyo unayejadili naye pengine ni zaidi yako katika uzoefu wa hayo hayo unayotaka kudanganya juu yake.

Mwisho niseme, hicho kitabu hakuna, ni danganya toto tu. Na jinsi unavyopinda pinda katika kutoa visingizio vya vitisho, ni dhahirikuwa hukuwa na msaada wowote katika utumishi ndani ya mashirika hayo uliyotumikia. Ni wazi ulikuwa ni sehemu ya kuyahujumu yasifanikiwe. Ulikuwa ni sehemu ya tatizo, na siyo sehemu ya ufumbuzi.
 
Lakini Paskali uko muwazi Sana. Yaani hata Stori za Dingi wako unazotoa humu? Hongera Sana kwa Hilo.
Mkuu Kuta, KUTATABHETAKULE , mimi ni very open and transparent, the same ilikuwa kwa Dingi wangu, tulikuwa ma besti sana, tangu mdogo ananipitisha anga zake na kona zake. Wazee wa Kisukuma, hizo ndio zao!, na mimi nimekuja kujikuta nimerithi, saa hizi niko over 50 naitafuta 60 lakini bado nafyatua ... Changamoto za kupata mtoto mchanga ukiwa umri wa kustaafu, unakuwa ni Baba Babu. Dawa ni kujipanga kabla, vinginevyo ni kubebesha watu mizigo yako maza wa dogo atampitisha kwenye Damu ya Yesu, ili kuiflush the Sukuma blood ili asiwe kama Dingi yake na babu yake!.
P
 
Nimepitia bandiko kuhusu Prof Shaba , nitajadili hoja chache

1. Kwamba Umri wa Prof.
Niwakumbushe Prof alioa mwaka 1963. Mtoto wake Hamish alifariki Marekani mwaka 2001 akiwa na umri wa miaka 36. Leo mtoto huyo angekuwa na miaka 58 takribani 60 ambao ni umri wa kustaafu. Wastaafu wa Tanzania tunawaita Wazee seuse Mzee Prof Shaba.

2. Kwamba alikata kinywaji kikali. Ni kweli lakini kinywaji kikali kinategemea lishe pia. Ukinywa gongo halafu ukaamkia mihogo na kushindia kauzu na karanga mustakabali wako si mwema.
Pombe kali si tatizo, bali unatumia vipi na unajitunza vipi.

3. Kwamba kwanini alikwenda Marekani, hakuacha alama katika utumishi wake.
Prof Shaba ni mmoja wa Wasomi wakubwa Barani Africa. Tukiangali kwa haraka, kundi lake ni la akina Prof Mathew Luhanga, Prof Msuya wa Bicohemistry, Prof Makene , akina Prof Mmari, Prof Sarungi n.k.

Prof Shaba ni mhadhairi 'pioneer' wa Faculty of Medicine (University of Dar es Salaam) miaka ya 70 hadi ilipokuwa college (MUCHS) na kuwa MUHAS ya sasa

Watu waliopitia Medicine katika mikono ya Prof Shaba ni maelfu na Universities za Medicine zinafundishwa na Wanafunzi na vijukuuWanafunzi waliopita mikono ya Prof Shaba.

Ndiyo maana leo Taifa linazizima. Prof Shaba ni moja ya Wahadhiri walioipaisha University of Dar es Salaam

Alama aliyoacha Prof Shaba hutaiona katika majengo, madaraja kama la Mfugale au viwanja vya Mpira.

Prof Shaba ameacha alama katika fikra za watu , alama itakaoishi milele kwasababu kila mwanafunzi ni zao lake.

Prof Shaba alikuwa mtu mzuri sana, alipenda sana Wanafunzi tena akisimama nao wanapoonewa.

4. Kwanini alikwenda Marekani! Ala! mtu ana watoto wake kwanini asiende kuishi mahali anapotaka

Yeyey alisomesha wakwakwe nao wakamlea Baba yao, tatizo lipo wapi.

Alikula pensheni ya kazi zake kupitia watoto wake. Prof Shaba hakutegemea hizi pensheni za ''Wenza' !

Ahsante ! ahsante , ahsante na Pumzikwa kwa Amani Prof J. Shaba.
Asante sana Mkuu Nguruvi3, umemtendea haki Prof. Shaba.
P
 
Mimi kutokubaliana nawe katika baadhi ya maswala yanakupaje wewe ujuzi wa kujua kwamba nina tatizo la kisaikologia?
Wewe ni mtaalam pia katika eneo hilo?

Alimaanisha psychological au? Ina maana hata kuandika hajui huyo mzee halafu ndo kaandika kitabu basi hiyo elimu ya kipindi hiko ni ya mashaka makubwa.
 
Rashid Mfaume Kawawa alikuwa waziri mkuu wa mwisho wa Tanganyika January 1962 mpk 9 December 1962.

Kuanzia 10 December 1962 mpk February 1972 nafasi ya waziri mkuu ilifutwa.

Mwaka 1972 February nafasi ya waziri mkuu ilirejeshwa na Rashid Mfaume Kawawa akawa waziri mkuu wa kwanza wa Tanzania mpk mwaka 1977.

Kawawa alifuatiwa na Sokoine
Waziri mkuu wa kwanza wa Tanganyika huru alikuwa ni hayati Julius Nyerere.

Huo ndo ulikuwa ni utaratibu kwa makoloni ya Uingereza ambayo yalianza kupewa uhuru wao.

Hata Zimbabwe Hayati Bob alikuwa waziri mkuu mwaka 1980 kabla ya kuwa raisi kamili mwaka 1987.

Tanganyika ikaitwa "Republic" yaani Jamhuri ya Tanganyika.

Hayati Mwalimu alikuwa ni waziri mkuu ambae alipewa muda wa kuongoza serikali ya mpito (caretaker government) mwaka 1961 ambayo baadae ilikuja kuvunjwa mwaka 1962.

Kwahiyo tokea Disemba 9 mwaka 1961 hadi mwaka 1962 Tanganyika iliongozwa na serikali ya mpito ikiwa chini ya waziri mkuu Julius Kambarage Nyerere.

Baada ya makabidhiano yote na wakoloni kukamilika mwaka huohuo wa 1962 Tanganyika ikawa na serikali yake kamili huku hayati Mwalimu akiwa raisi na waziri mkuu wake akawa Rashid Mfaume Kawawa.

Mzee Kawawa alikaa kwenye uwaziri mkuu kwa miezi 12 tu na mwezi disemba mwaka 1962 nafasi ya waziri mkuu ikavunjwa na hakukuwa na waziri mkuu hadi mwaka 1972 mwezi February Hayati Kawawa alipoteuliwa kuwa waziri mkuu na akakalia kiti hicho hadi mwezi Februari mwaka 1977 nafasi hiyo alipopewa Hayati Edward Moringe Sokoine.

Mzee Kawawa na Mwalimu walitokea mbali sana kwenye siasa za nchi hii na ni waasisi khasa, Kawawa akiwa anamsaidia Nyerere kuunda TANU, Chama cha wafanyakazi na akawa makamu wa raisi Nyerere.

Pia mzee Rashid Kawawa alishika nafasi ya waziri wa Ulinzi na kusaidia kuanzisha JWTZ ya leo na JKT, na amewahi kuwa makamu mwenyekiti wa CCM na hata katibu mkuu wake.
 
..msipotoshe.

..Sokoine angekuwa kadungwa risasi mwili wake usingeguswa na Daktari yeyote.

..Na mwili wa Sokoine ulilazwa Karimjee Hall na wananchi walipewa fursa ya kumuona na kutoa heshima zao.

..ukiacha hilo, familia, watoto wa kiume wa Sokoine, walimfanyia Mzee wao Mila za Kimaasai kabla ya kumzika.

..Na mila hizo zinahusisha kumpaka marehemu mafuta yanayotoka ktk kidari cha ng'ombe dume.

..Madai kwamba Sokoine aliuwawa sio ya kweli, bali ni story za kijiweni za Watanzania.

..Prof.Shaba hakuhamishiwa Marekani na watu wa usalama. Alikwenda huko kuishi na wanawe baada ya kustaafu miaka ya mwisho ya 90.

..Watoto wote wa Prof walikuwa wakiishi Marekani.
Okay.
 
Hii sijawahi kusikia, ila Mwandishi wake wa habari alijuwa ni Acadoga Chiledi, na gari yake ndio ilikuwa 3rd car nyuma ya Sokoine, hivyo ajali imetokea mbele yake!, he had an interesting story to tell, akihadithia tuu bila ku documents, he is deceased now!.
P
Ila Paskali you know so many things and so many people in high places, it buffles me?
 
Back
Top Bottom