Profesa Wangari Maathai afariki dunia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Profesa Wangari Maathai afariki dunia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by joseeY, Sep 27, 2011.

 1. joseeY

  joseeY Senior Member

  #1
  Sep 27, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  MSHINDI wa Tuzo ya Amani ya Nobel kutoka Kenya, Profesa Wangari Maathai, amefariki dunia katika Hospitali ya Nairobi alikokuwa akitibiwa ugonjwa wa saratani. Maathai, aliyeshinda tuzo hiyo mwaka 2004, alikuwa mwasisi wa Shirika la Mazingira Kenya. Mkurugenzi wa Green Belt Movement, shirika ambalo Profesa Maathai alilianzisha, Profesa Karanja Njoroge alithibitisha kutokea kwa kifo hicho. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Profesa Njoroge alisema Maathai, aliaga dunia saa 10:00 alfajiri ya kuamkia jana katika hospitali hiyo alikokuwa akipatiwa matibabu. Alisema wakati wa kifo chake, Profesa Wangari alikuwa na wanafamilia na marafiki.

  Profesa Maathai ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 71, ameacha watoto watatu; wawili wa kiume na mmoja wa kike. Profesa Maathai alianzisha vuguvugu la Green Belt mwaka 1977 na alifanya kazi na wanawake kote nchini kuboresha maslahi yao na kuhifadhi mazingira.

  Alikuwa mtetezi mashuhuri wa matumizi bora ya maliasili na shughuli zake zilitambuliwa mara kwa mara kote duniani. Baada ya taarifa ya msiba kutangazwa, Rais wa Kenya Mwai Kibaki ambaye yupo New York, Marekani katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa (UN), alituma salamu za rambirambi kwa Wakenya wote kutokana na msiba huo mkubwa.

  JK, Kofi Annan watuma rambi rambi Rais Jakaya Kikwete naye alituma salamu zake za rambirambi kupitia mtandao wa Twitter. Katika salamu hizo, Rais Kikwete alisema Afrika imepoteza mwanamke shupavu na Mwenyezi Mungu amlaze pema pemboni.

  Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan alisema Profesa Maathai, atakumbukwa milele na kuheshimiwa. Historia ya Profesa Maathai Wangari Muta Maathai alizaliwa Aprili Mosi, 1940 katika Kijiji cha Ihithe, Wilaya ya Nyeri, Kenya. Mwaka wa 2004 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani iliyo mfanya awe mwanamke wa kwanza Mwafrika kuipata Januari 2003 - Novemba 2005, Alikuwa Mbunge na Waziri Msaidizi katika Serikali ya Mwai Kibaki. Mwaka 2007, katika maandalizi ya uchaguzi wa Kenya, Profesa Maathai alisimama upande wa Rais Kibaki lakini hakuteuliwa na Chama cha PNU kugombea ubunge kupitia Chama cha Mazingira Green Party.

  Elimu na tuzo Maathai alihudhuria shule ya msingi ya Ihithe, halafu shule ya upili ya Loreto Convent, Limuru. Baada ya kuhitimu sekondari, alienda ng’ambo kusoma Bayologia nchini Ujerumani na Marekani. Mwaka wa 1967, alipata shahada ya kwanza ya baiolojia kutoka Chuo Kikuu cha Benedictine, Marekani. Aliendelea na masomo yake katika Chuo Kikuu cha Pittsburg ambako alipata shahada ya uzamili.

  Alirejea Nairobi na kupata shahada ya uzamivu (PhD) kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi katika somo la udaktari wa wanyama. Kuanzia mwaka wa 1977, Maathai alikuwa Profesa msaidizi wa anatomia ya wanyama huko Nairobi akiwa mwanamke wa kwanza kupata uprofesa katika Chuo Kikuu cha Nairobi.

  Tuzo alizopata
  Baadhi ya tuzo alizopata ni pamoja na ile ya Mwanamke wa Dunia (1983), Tuzo ya Goldman kwa Mazingira (1991), Elder of the Burning Spear (2003) kutoka Serikali ya Kenya, Tuzo ya Nobel ya Amani (2004) na Legion D’Honneur (2006) kutoka Serikali ya Ufaransa.

  Mwaka wa 1977, Maathai alianzisha shirika la Green Belt Movement ambalo linajihusisha hasa na mazingira, haki za raia na demokrasia. Ndoa na familia Mwaka wa 1969, Wangari Muta (jina lake la kuzaliwa) alifunga ndoa na Mwangi Maathai, mwanasiasa wa Kenya na kupata watoto watatu, Waweru, Wanjira na Muta, lakini walitengana baadaye.
   
 2. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  RIP Prof
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  RIP Prof Wangari.
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  Masikini zile pesa sijui kama alizimaliza zote ama alitumiakwa furahaa loh
  mungu amuweke mahala pema peponi jamani
  KAMA NAONA NDUGU ZAKE WATAKAPOPAMBANA NA ZILE ZIFUTA JASHO HOPE WATOTO NI WAKUBWA
   
 5. M

  Mwana wa Kitaa Member

  #5
  Sep 27, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu amlaze pema peponi.
   
 6. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  R.i.p....................
   
 7. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,046
  Likes Received: 6,492
  Trophy Points: 280
  R.I.P Profesa wetu.
   
 8. kidadari

  kidadari JF-Expert Member

  #8
  Jan 6, 2018
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 2,338
  Likes Received: 1,198
  Trophy Points: 280
  RIP
   
 9. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #9
  Jan 6, 2018
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,739
  Likes Received: 537
  Trophy Points: 280
  Wewe nawe!
   
 10. kidadari

  kidadari JF-Expert Member

  #10
  Jan 6, 2018
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 2,338
  Likes Received: 1,198
  Trophy Points: 280
  shida nn kwan hakufariki?
   
Loading...