Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 6,323
- 8,236
Profesa wa sayansi, uhasibu, hesabu au engineering hasomei kuzungumza siasa majukwaani bali anasomea fani yake.
Lakini pia Dokta wa sayansi, uhasibu, hesabu au engineering hasomei kuzungumza majukwaani bali anasomea fani yake.
Nitaendelea kuwafundisha watanzania wasio nauelewa juu ya professionalism za wasomi wetu Tanzania.
Huwezi kumlinganisha profesa wa sheria na profesa wa sayansi katika kuielezea sheria lazima profesa wa sheria ataonekana anajua kuelezea sheria kuliko profesa wa sayansi. Vivyohivyo huyu wa sayansi ataonekana yuko vizuri kwenye sayansi yake.
Jambo moja ambalo watu wengi wanashindwa kulielewa ni kuhusu professionalism. Kuwa profesa au dokta haaminishi kwamba amesoma kila kitu amekimaliza hapana kuna specialization.
Wengine wanabobea kwenye physics, wengine kwenye hesabu, wengine kwenye uhasibu, wengine kwenye kiswahili na wengine kwenye siasa, n.k
Sasa mtu kuwa profesa wa kiswahili haimaanishi kwamba hata kiingereza anakijua, au hata sayansi anaijua au hata siasa anaijua au hata kuongea kisiasa anajua.
Tuache kuchanganya katika hilo lasivyo tutaendelea kuwalaumu watanzania wenzetu. Mara huyu haongeii kiswahili kizuri huyu hajui siasa, mara huyu hazungumzi kiingereza kizuri mara huyu hajui sheria.
Kila mtu anajua vizuri kile alichokisomea, tofauti ni kwamba kunabaadhi ya mambo ukiyasomea yanatumika moja kwa moja kwenye jamii katika mazungumzo ya kila siku. Na kuna mengine ukiyasomea hayatumiki kwenye mazungumzo ya kawaida.
Mfano vipi mtu aliyesomea historia akachukua na siasa kidogo, au vipi mtu aliyesomea civics, hawa wanakua vizuri sana mdomoni wakiwa jukwaani.
Naomba nimalize karibuni kwa maoni sasa.