Ndugu yangu muathirika mwezangu, maneno ya Prof MUHONGO ilikuwa siasa tupu. Sisi tupo KWAMUROMBOO Arusha, kata inayoongozwa na maCCM tukapambana tukimshirikisha DIWANI. Tukidhani watajiosha. Diwani alipoona ngoma nzito akamualika meneja mkoa aje ajibu kero zetu. Tulichoambulia nikukatishwa tamaa jumla, na kwamaelezo yake yule Meneja hakuuma maneno. Namnukuu: ' Ndugu zangu tunauhaba mkubwa wa nguzo kwenye shirika iliyotokana na kushushwa kwa gharama za kuunganisha umeme. Kwa mkoa wetu tu tunahitaji nguzo 20,000. Na waliokwisha lipia tunadaiwa nguzo 2000 hadi Januari 2013. Lakini hadi leo tar 25/5/2013 tumeletewa nguzo 300 tu! Sasa mtaona ni jinsi gani tunapungukiwa, tunaowaomba tu kuweni na subira' Mwenye akili fanya tafakari.