Hana uzalendo wowote huyu. Uzalendo wa kweli ilitakiwa kuuonyesha siku ile ile wakati anasoma budget yake bungeni kwa kumwaga kila kitu hadharani sio kutufichaficha baadhi ya mafuta yake.[/QUO
Wewe bunge si kijiwe cha kubishana simba na yanga. Lazima uwe na data zote ndipo uwataje watu.
Mimi namuunga mkono Prof huyu mahiri. Ana msimamo na alisimama kidete kuwakatalia makampuni ya kihuni yaliyotaka kununua mafuta kwa bei ndogo Puma kisha kuuzia serikali kwa bei kubwa. Mimi wasiwasi wangu ni kuwa atahimili hayo maadili yake kwa muda gani kabla hajaingizwa kwenye fisadi strong room ya JK na CCM.
Simama kidete Prof. Najisikia fahari kubwa kwa watu wa mkoa wangu wanapkuwa weledi na kukataa kuperekeshwa na mafisadi. Wewe ni mtoto wa Mara anakotoka mwalimu JK. Tafsdhali rudisha heshima ya mkoa wetu unaochafuliwa kila siku na wanasiasa tumbo kama Wasira na wengine.