1. Juzi na jana Mwenyekiti wa CCM (T) ambaye pia ni Rais wa Tz, katika vikao vya chaguzi za UWT na UVCCM alieleza kuwa, kuna watu wananunua uongozi na kura zinauzwa. Kwamba kuna watu wanatumia rushwa na kuna makundi ya wanaowania Urais ujao; akawaasa wajumbe wasiwapigie kura watu hao. Sasa wewe msomi, Mkumbo kamwambie na Rais Kikwete atoe ushahidi wa rushwa na au hayo makundi vinginevyo aombe msamaha.
2. Baada ya hicho kikao cha Bunge kuahirishwa, katika kipindi cha dakika 45 kwenye ITV, Mh. Job Ndugai (Naibu Spika) alisema waziwazi kuwa kulikuwa na sababu zaidi ya moja zilizosababisha kuvunjwa Kamati ya Bunge inayosimamia Wizara ya Nisahati na Madini. Moja wapo ni kuwa Wabunge wenyewe ndani ya kamati walikuwa wanalalamikiana kwa kuwatuhumu wenzao ndani ya kamati hiyo kuhusika na vitendo vya rushwa. Sasa kawambie na hao Wabunge waombe msamaha, kabla ya kumwambia Mh. Job Ndugai na pia Mh. Anna Makinda naye athibitishe ni akina nani hao waliokuwa wakilalamika la sivyo nao waombe msamaha kwani haiwezekani katika kadamnasi ya waelewa katika Bunge zima la nchi, Waziri mmoja kichaa akaibuka na kusema kuna harufu ya rushwa halafu Spika avunje tu Kamati kwa kauli hiyo ya mtu mmoja bila kujiridhisha na yaliyosemwa au kuwepo sababu nyingine za kimazingira au vinginevyo.
3. Julai 14, 2012 saa 10.00 jioni, Dr. Mkumbo ulisema kuwa Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigullu Nchemba ni mzinzi. Je uliweza kupeleka mahakamani ushahidi wa uzinzi? Basi kama hujawahi kutuonesha jinsi ulivyokuwa ukishuhudia kwa kupiga chabo au CCTV footage ulizokuwa umetegesha tendo la uzinzi wa mtu au kuwashawishi Mh. Mwigulu na waliyekuwa wakizini naye wenyewe wakiri kuwa ni wazinzi basi omba msamaha. Wewe Mhadhiri, Mzamivu wa Saikolojia, utajidharirisha sana Dr. Mkumbo kudoubt anachosema msomi mwenzako simply kwa kuwa wewe uko CHADEMA na yeye CCM katika suala zito la rushwa inayoitafuna nchi yetu ambalo kwa ushahidi wa kimazingira vinadhihirisha wazi pasi na shaka kuwa rushwa ipo Tanzania. Waziri Sosper alisema na kuwataka baadhi (sio wabunge wote) wenye migongano ya kimaslahi na TANESCO & Wizara wasifanye hivyo, alisema pia kuwa Mkurugenzi Mhando alikuwa anafanya biashara na mkewe ndani ya TANESCO, alisema pia kuwa kuna waliokuwa wanaiba umeme kupitia vishoka na akataja hata Shule za akina Mchungaji Lwakatare n.k, alisema pia wazi kuwepo kwa hujuma za kutunga migao ya umeme (power rationing) kwa kisingizio cha uhaba wa uzalishaji wa nishati jambo ambalo ni tofauti na kukatwa umeme tokana na uharibifu au ukarabati wa miundombinu katika baadhi za sehemu. Hayo yote hayakusemwa na Mawaziri waliopita wala Viongozi wa kamati za bunge akina Mh. Makamba au rafiki yako Mh. Zitto ambao yeye alibaki kumsifia na kumtetea Mhando kuwa ni msafi na mahesabu ya vitabu vya TANESCO kuwa ni masafi. Nawe unaingia kichwa kichwa unaunga mkono mafisadi eti oh leta ushahidi katika jambo la wazi kama hili?
4. Kwa vile wewe ni mshauri ndani ya CHADEMA, mweleze vile vile Mh. Lissu atoe ushahidi ndipo uamini akiyoyasema ambapo yeye hata aliwataja Wabunge waliohusika katika tuhuma za rushwa na za migongano ya maslahi. Usiniambie kuwa Lissu ni kilaza kiasi kile cha kusikia tu eti Waziri anasema bungeni halafu yeye naye akakimbia faster mbele ya TV na na kucut na kupaste tuhuma just kwa sababu zimesemwa na Waziri.
5. Hivi majuzi nilikusifu ukuongoza kongamano zuri UDSM la kumenzi Baba wa Taifa Nyerere. Sasa mbona baba wa Taifa, J. K Nyerere kwa shahidi tu za kimazingira kasema mara kadhaa kuwa nchi yetu inanuka rushwa au kuwa serikali ni corrupt. Na sijawahi kukusikia ukisema kuwa huamini aliyosema Nyerere maana hakutoa hard evidence za kuwepo rushwa. Sasa naamini yule kijana aliye kukumbusha kuwa Wahadhiri wengine hamufanyi tafiti na kuandika papers, ni kweli! Nakukumbusha kuwa, Nyerere alieleza kuwa dalili za serikali corrupt, ni kutokusanya kodi; hakusema kuwa ni Mkurugenzi T, tarehe U, saa V aliyeonekana katika surveillance camera W, akipokea Tsh. X, wakiwepo askari Y na Afisa wa Takukuru Z.
Sasa huu ni mfano mzuri sana wa jinsi ambavyo watu wenye maadili na uthubutu wanaweza kuona mbali kwa utafiti wa kimazingira na kusema hapa kuna rushwa kama vile mazingira aliyoyaona huyu Profesa wa ukweli Sospeter lakini akina viegeugeu Zitto wakawa wanazunguka usiku kucha wakizuia Mhando asichukuliwe hatua.
Msomeni kiona mbali, Carl Sagan, Astronomer akitamka, Absence of evidence is not evidence of absence!"
Waziri Sospeter hakuna kuomba radhi wala hakuna ku regret whatsoever! Mh. Spika unda Kamati nyingine na watuhumiwa wasogezwe kwenye vyama vyao. Mh. Kikwete wale Mawaziri na Watendaji wakuu wengine wanaolala na kuamka business as usual na kukuita tu Dr. Dr. bila mpango fukuza! Wanaochakalika bila uwoga kama huyu Sospeter (ambaye ni wewe ulimleta in the first place) na anaonekana kusimamia maadili na maendeleo wape support ya nguvu, maana hawa ndiwo watakaoiokoa CCM (kama inaokoka) wala sio UVCCM maana hawa Mawaziri na Makatibu wakuu ndio wasimamizi wakubwa wanaoweza kuhakikisha kuwa kero za wananchi zinapungua na viwango vya maisha ya wananchi vinapanda. Wananchi hawajali uprofesa wake wala ustadi wa kuomba miongozo bungeni bali wanataka kuona nguzo na bili za umeme zinapungua kwa mwananchi wa chini, umeme unawaka wakati wote, wachimbaji wadogo wanawezeshwa, mikataba yote inakuwa wazi na iwe ya kumfaidisha Mtanzania zaidi ya mwekezaji. Mambo kama haya ndiyo darubini yetu kwa huyu Profesa. Akianza kukatishwa tamaa tu, mafisadi nao (bila kujali itikadi za vyama) wanaanza kupeperusha bendera zao. Hii ni karne nyingine hatukubali kupotoshwa!