Profesa Muhongo: Nimekuta 'madudu' ya kutisha TANESCO

Kama huyu Professor akitibu Matatizo ya Umeme Tanzania na kurekebisha Ufisadi Wizarani na Tanesco hapo tutaona hatuna

Haja ya kuwa na Mawaziri ambao ni Wabunge sababu wanachungana. Ni kuwa na Mtu huru ni rahisi kumshutumu na

kumchunguza na anachaguliwa kwa sababu ya Resume yake na sio kubebana Oh Huyu ni January Makamba ah huyu ni

William Ngeleja kijana huyu atafaa hata kama hana Qalification za kuongoza hiyo Wizara.
 
Muhongo unapigana na system ambayo huiwezi. marais wawili hasa Mkapa amefanya madudu ambayo ukiyaingilia unapoteza "unga". Yangu macho!!!! Muulize Tibaijuka, amefika wapi na ardhi!!!
 
mwazno unaonekana mzuri lakini viini macho vya jinsi katika serkali ya JK ni vingi hebu tusubiri.sasa huyu dogo Ngeleja kenda wapi nilidhani atakuwa segerea muda si mrefu!
 
Muhongo unapigana na system ambayo huiwezi. marais wawili hasa Mkapa amefanya madudu ambayo ukiyaingilia unapoteza "unga". Yangu macho!!!! Muulize Tibaijuka, amefika wapi na ardhi!!!
Usimkatishe taamaa, haya mambo kuna siku yataisha tu, ni taratibu. Lakini akiwepo mtu makini yataaisha, mimi nina imani na huyu profesa, ataweza tu.
 
Pamoja na kukuta Madudu ya ovyo hapo wizarani bado ngereja anabandika mabaongo ya kujisafisha jimboni kwake. Hii inatisha
 
Pamoja na kukuta Madudu ya ovyo hapo wizarani bado ngereja anabandika mabaongo ya kujisafisha jimboni kwake. Hii inatisha

Anajua hakuna wa kumgusa wala kuulizia alilolifanya pale wizarani
Mkuu hii nchi bana fanya yote ila kama hujagusa maslahi ya wakubwa utapeta tuu au ukijifunza kula na wakubwa huna maneno
 
....Sasa kama hataki kuyasema madudu hayo hadharani ili Watanzania tuyajue anasubiri kwenda kuyasema kaburini!? :shock:

Kuhusu kuvunja mikataba iliyojaa madudu mbona ule mkataba wa Dar City Water Lowassa aliuvunja na haukuwa na negative impact yoyote kwa nchi baada ya kuuona hauna maslahi kwa Tanzania!?
 
mbwembwe tu hizo yaani huyo akipigwa viuno viwili tu anatepeta mauzauza yale yale
 
"Mheshimiwa Waziri pamoja na kununua kwa bei hiyo wakati mwingine sisi huamuriwa kuzima mashine zote ili kampuni nyingine ziweze kuzalisha na kuuza umeme na maagizo haya hutoka ngazi za juu"alisema Mwalangwa huku akishangiliwa na wafanya kazi wengine.
kwa ufahamu wangu mdogo nilikuwa najua gridi ya taifa haitoshelezi mahitaji! kumbe kuna mitambo huzimwa wakati mwingine! nilitegemea mitambo yote inge operate at full capacity!
 
Hii hadithi ya madudu huko TANESCO hatuihitaji. Yeye atueleze jinsi alivyojiandaa kukata mirija/mizizi ya madudu hayo ambayo imejikita barabara kwa waliomteua kukalia kigoda hicho na washikaji wao muhimu. Vitu kama Richmond-Symbion, IPTL, Songas, havijitokezi kwa majaliwa tu.
 
Usimkatishe taamaa, haya mambo kuna siku yataisha tu, ni taratibu. Lakini akiwepo mtu makini yataaisha, mimi nina imani na huyu profesa, ataweza tu.

Una wishes nzuri kama wote tulivyo, lakini kwa system ya TZ, tutakumbushana humu jamvini. Just take note of this thread. Mfano, (nasema mfano si yeye) kama JK ndiye mwenye madudu, atafanya nini huyo Prof.
 
Huyu naye ni walewale! Ameanza vibaya! Ni mambo gani hayo ambayo hawezi kuyasema? Anakaa kimya kwa faida ya nani? Cheo alicho nacho ni kwa manufaa ya nani? Ndio yaleyale mazingaombwe ya CCM ya kutunziana siri na kulindana! Tanzania ndio nchi pekee duniani ambapo hujuma, utapeli na wizi wa mali ya umma ni siri ya serikali!! Bado tuna safari ndefu!!
 
Back
Top Bottom