Profesa Muhongo: Nimekuta 'madudu' ya kutisha TANESCO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Profesa Muhongo: Nimekuta 'madudu' ya kutisha TANESCO

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by engmtolera, May 21, 2012.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  May 21, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Monday, 21 May 2012 | Geofrey Nyang'oro

  WAZIRI wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amemkaanga mtangulize wake akisema baadhi ya madudu aliyoyakuta katika wizara hiyo ni makubwa ambayo hawezi kuyasema hadharani.


  Profesa Muhongo ni miongoni mwa Mawaziri wapywa walioteuliwa Mei 3, mwaka huu kushika wadhifa katika baraza jipya la mawaziri ambapo kabla ya uteuzi huo aliteuliwa kuwa mbunge kupitia viti maalum na Rais.

  Profesa Muhongo mwenye taaluma ya Jiolojia alitoa kauli hiyo juzi, alipokuwa akizunguza na wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani katika mkutano wao uliofanyika katika viwanja vya makao makuu ya Shirika hilo jijini Dar es Salaam.

  Katika mkutano huo wafanya kazi walitaja mambo kadhaa yanayolifanya shirika hilo kushindwa kujiendesha kuwa ni pamoja na mikataba mibovu iliyoingiwa na Serikali kwa Kampuni ya kufua umeme na vitendo vya baadhi ya watendaji wizarani ambao hujihusisha na hujuma dhidi ya shirika hilo.

  Akijibu hoja mbalimbali za wafanya kazi alisisitiza kuwa, suala la mikataba mibovu iliyoingia na Serikali inajulikana na wananchi wote lakini akasema hata yeye alipoingia wizarani amekuta mambo mabaya ambayo hawezi kuyasema hadharani.

  "Ninyi mnazunguzia mikataba mibovu na mnataka tuifute, wafanyakazi wa Tanesco ni watu waliokwenda shule tuongee vitu vinavyowezekana, ile ni mikataba….siyo kwamba mimi natetea mikataba mibovu yapo mambo niliyoyakuta huku ni makubwa hata mimi siwezi kuyasema hadharani" alisema Muhongo na kuongeza:


  "Suala la mikataba huwezi kulibadilisha kwani imeshatufunga , Serikalini nne zimeingia mikataba, awamu ya kwanza ya pili ya tatu na hata ya nne, sisi katika awamu yetu tunawaahidi hatuwezi kuingia mikataba mibovu ndio sababu nikagusia kuwa mimi kama waziri siwezi kusaini mkataba wowote unaohusu umeme bila kushirikisha Tanesco,TPDC" alisema Muhongo.

  Profesa Muhongo pia alitaja mambo mengine aliyodai ameyakuta wizarani na kuyafanyia kazi katika kipindi kifupi cha siku 18 alizokaa kwenye wadhifa huo kuwa ni pamoja na suala la uhusiano mbovu baina ya wafanya kazi wa wizara hiyo, Samico, Tanesco na TPDC ambapo kila upande unafanya kazi kivyake na kushutumu upande mwingine.


  "Nimekuta hakuna ushirikiano baina ya Wizara, TPDC, Samico na ninyi Tanesco,mbaya zaidi kila upande unatupia lawama upande mwingine, nimenza kwa kulifanyika kazi hilo na kuanzia sasa sisi wote ni timu moja kazi yetu ni kuhakiksha tunatoa huduma bora ya umeme kwa watanzania" alisema Muhongo.

  Muhongo alisema yeye ameshaanza kazi na moja ya mambo aliyoyafanya ni kurejesha rasimu ya mapendekezo ya muswada wa kurekebisha sheria ya umeme iliyokuwa imeandaliwa bila kushirikisha pande zote zinazohusika na masuala ya umeme ikiwamo Tanesco na TPDC.

  "Kuanzia sasa pale wizarani kila kitu kitakuwa wazi,mimi sitasaini mkataba wowote bila kuwashirikisha ninyi,sitaruhusu vitendo vya hujuma na mtu yeyote wala kuruhusu kutungwa kwa sheria bila ya kuwashirikisha"alisema Muhongo.

  Kuhusu jitihadi za kutafuta ufumbuzi suala la umeme alisema, kesho Jumanne Maofisa kutoka TPDC,Tanesco na Wazara ya Madini wanatarajia kukutana na Naibu waziri wa Nishati ya umeme, George Simbachewene kujadili na kuandaa mkakati wa kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la umeme nchini.

  Alitaka wataalamu wa umeme kujadili namna ya kulitoa Taifa katika mtindo wa kutegemea chanzo kimoja cha umeme wa maji na badala yake kuangazia vyanzo vingine ambavyo ni makaa ya mawe na gesi.
  Pia waziri huyo alitaja vyanzo vingine kuwa ni umeme wa upepo,Jiothramu na jua ambao alisema vyanzo hivi vikitumika vizuri vitalisaidia taifa.

  Katika mkutano huo pia Waziri huoaliwatangazia neema ya kupatikana kwa gesi katika shirika hilo aliposema bombo la kusafirisha gesi linalojengwa kwa sasa ni mali ya serikali.

  "Ninachotaka mimi tuache yote yaliyopita kwani tukijikita kushughulika na hayo tunaweza kushindwa kutekeleza hii mipango tuliyojiwekea,hivi sasa bomba la gesi linalojengwa ni mali ya serikali lakini pia Mgodi wa Kiwira taratibu za kuurejesha serikalini zimekamilika na utakuwa chini ya Samico"alisema Muhongo.

  Kuhusu mikataba alisema hatua za kufanyia marekebisho mikataba hiyo, zinaendelea ndani ya wizara kama ilivyofanyika kwa ile ya madini ambayo kwa sasa inalipa asilimia 4 ya mirabaha badala ya asilimia tatu ya awali.

  Waziri huyo alitaja pia hatua ambazo wizara imefanya kwa sasa kuwa ni kupitia na kubaini namna Kampuni zilivyoingia na kufanya kazi ya kusafirisha gesi ambapo alisema, kuna kampuni nyingi zinazofanya kazi hiyo.


  Wafanya kazi na wizara
  Wafanya kazi katika mkutano huo walitaja mambo waliyodai ni kero kwao na yanayoangamiza Shirika hilo ikiwamo mikataba ya kuuziana umeme kwa bei kubwa na kuuza kwa bei ndogo.

  Mmoja wa wafanyakazi hao, Kamil Mwalangwa kutoka kituo cha kuzalisha umeme wa Mega watts 100 alisema:

  "Katika kituo cha Mg 100 kuna makundi manne yanayonunua gesi kwa ajili ya kuzalisha umeme,Kampuni ya Tegeta,Simbion, Songas na sisi Tanesco,lakini sisi bei tunayouziwa ni kubwa tofauti na wenzetu,nini sababu inayotufanya tununue kwa bei ya juu?alihoji na kuongeza:


  "Mheshimiwa Waziri pamoja na kununua kwa bei hiyo wakati mwingine sisi huamuriwa kuzima mashine zote ili kampuni nyingine ziweze kuzalisha na kuuza umeme na maagizo haya hutoka ngazi za juu"alisema Mwalangwa huku akishangiliwa na wafanya kazi wengine.

  Alisema kwa sasa muda wa matengezo wa injini zinazofanya kazi katika eneo hilo umepita na shirika halina vifaa vya ziada (spea)wala fedha za kununulia jambo alilodai ni hatari na wakati wowote mitambo hiyo inaweza kuzima na kuongeza tatizo la umeme nchini.

  Mwalangwa litaja tatizo jingine litakalolikumba Shirika hilo kuwa ni kuharibika kwa mitambo kutokana na kuwasha na kuzima kila wakati kwa lengo la kupisha mitambo ya kampuni nyingine kuwasha mitambo yao na kuuza umeme.

  Alison Mwambaga mmoja wa wafanyakazi wa Tanesco , alipendekeza kwa waziri huyo mwenye dhamana kufuta mikataba yote mibovu ukiwamo wa IPTL kwa kuwa ndiyo inayoliangamiza shirika hilo na Taifa kwa jumla.

  GAZETI MWANANCHI
   
 2. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hata aliyemtangulia mwanzo alianza hivi hivi ngoja azoee ofisi ndo mtajua mtanzania alivyo.
   
 3. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Ameanza vizuri lakini isje kuwa ni "upepo tu, utapita" au nguvu ya Sprite!!!!

  Tiba
   
 4. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  WAZIRI wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amemkaanga mtangulize wake akisema baadhi ya madudu aliyoyakuta katika wizara hiyo ni makubwa ambayo hawezi kuyasema hadharani.

  Profesa Muhongo ni miongoni mwa Mawaziri wapywa walioteuliwa Mei 3, mwaka huu kushika wadhifa katika baraza jipya la mawaziri ambapo kabla ya uteuzi huo aliteuliwa kuwa mbunge kupitia viti maalum na Rais.

  Profesa Muhongo mwenye taaluma ya Jiolojia alitoa kauli hiyo juzi, alipokuwa akizunguza na wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani katika mkutano wao uliofanyika katika viwanja vya makao makuu ya Shirika hilo jijini Dar es Salaam.

  Katika mkutano huo wafanya kazi walitaja mambo kadhaa yanayolifanya shirika hilo kushindwa kujiendesha kuwa ni pamoja na mikataba mibovu iliyoingiwa na Serikali kwa Kampuni ya kufua umeme na vitendo vya baadhi ya watendaji wizarani ambao hujihusisha na hujuma dhidi ya shirika hilo.

  Akijibu hoja mbalimbali za wafanya kazi alisisitiza kuwa, suala la mikataba mibovu iliyoingia na Serikali inajulikana na wananchi wote lakini akasema hata yeye alipoingia wizarani amekuta mambo mabaya ambayo hawezi kuyasema hadharani.

  "Ninyi mnazunguzia mikataba mibovu na mnataka tuifute,wafanyakazi wa Tanesco ni watu waliokwenda shule tuongee vitu vinavyowezekana,ile ni mikataba….siyo kwamba mimi natetea mikataba mibovu yapo mambo niliyoyakuta huku ni makubwa hata mimi siwezi kuyasema hadharani"alisema Muhongo
   
 5. bona

  bona JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2012
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ndio kusema anaogopa au aliyoyakuta hata yeye kuya solve hawezi, i get feelings uozo uliokua wizara hiyo ni mkubwa na una connect watu wengi sana wakubwa hadi kuanza kutatua inakua shida kubwa sana!
   
 6. msnajo

  msnajo JF-Expert Member

  #6
  May 21, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,464
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Aweke kulindana pembeni! Kama kuna jambo ambalo anaona kuwa ni uzembe kiutendaji na lililokuwa na maslahi binafsi kwa watangulizi wake, asifiche kitu. Nafikiri Mh rais alimwamwini akamkabidhi rungu. Profesa, fungua uwezo wako kiutendaji, na utudhihirishie kuwa haikuwa makosa kwa rais kukupa uwaziri. Wananchi tunatarajia mengi kutoka kwako.
   
 7. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #7
  May 21, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  na amkaange ngeleja kuhusu kumchomeka mtoto wake Tanesco IT dept..na kulipwa mamilioni ya shilingi...
   
 8. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #8
  May 21, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Maumivu ya kichwa huanza taratibu! Mkuu unaweza ukakuta tatizo ambalo hata kulitaja unaona kizunguzungu.
   
 9. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2012
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mmoja wa wafanyakazi hao, Kamil Mwalangwa kutoka kituo cha kuzalisha umeme wa Mega watts 100 alisema:
  "Katika kituo cha Mg 100 kuna makundi manne yanayonunua gesi kwa ajili ya kuzalisha umeme,Kampuni ya Tegeta,Simbion, Songas na sisi Tanesco,lakini sisi bei tunayouziwa ni kubwa tofauti na wenzetu,nini sababu inayotufanya tununue kwa bei ya juu?alihoji na kuongeza:
   
 10. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #10
  May 21, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Gymnastics (cross bar)
  mikataba inahujumu uchumi, sheria ya kudhibiti uhujumu uchumi ipo, kutokuitumia hiyo sheria ni kuuhujumu uchumi kwa zaidi ya makusudi.
  Yaani unamuachia mwizi aendelee kuiba kisa eti ameshaingia ndani. Tumieni uwezo wote kuhakikisha mnaondoa hasara hii kwa walipakodi wa tz.
   
 11. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #11
  May 21, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Gamba jipya hili nalo bora angepewa Feel ku njombe
   
 12. mbalu

  mbalu JF-Expert Member

  #12
  May 21, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ntamwona wa maana sana kama atasambaratisha madudu yote na wahusika ndani ya mwezi mmoja na akabadili mfumo mzima wa utendaji kazi.
   
 13. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #13
  May 21, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  hawezi, ameshindwa kuyataja hayo madudu atawezaje kuyatoa? Si atapiga kimya tu!!!
   
 14. C

  Cozcoz Member

  #14
  May 21, 2012
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jiwe walilo likataa waashi limekuwa jiwe kuu la pembeni mtu akianguka kwenye jiwe hilo litamvunja kabisa na likimwangukia lita msaga kabisa (CCM)
   
 15. M

  MTK JF-Expert Member

  #15
  May 21, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  Well waelewa tunajua kuyatamka madudu anayoyazungumzia hadharani sio sahihi kwa sababu yeye ni mwana taaluma na sio mwanasiasa per se! tumpe challenge Prof; kama ameyaona madudu hayo je anatarajia kuchukua hatua gani au ndio hivyo hiyo ni kauli ya kuomba sympathy ya wanachi ili asichukue hatua, if so Prof throw in the towel kabla hujachukuliwa na kimbunga!!
   
 16. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #16
  May 21, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Tungojee kwa matumaini umeme kushuka
   
 17. pgasper

  pgasper JF-Expert Member

  #17
  May 21, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 311
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Transparency iko wapi sasa?
  Hawezi kusema hadharani!
  My take:
  Atakapotoka kwenye iyo wizara baada ya "kupiga dili za uhakika" naye afichiwe maouvu yake.
  Prof Muhongo ni muovu from the start.
   
 18. pgasper

  pgasper JF-Expert Member

  #18
  May 21, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 311
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  no hope!
   
 19. pgasper

  pgasper JF-Expert Member

  #19
  May 21, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 311
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  huenda ndo sehemu ya "madudu"
   
 20. S

  Shekispia JF-Expert Member

  #20
  May 21, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 226
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kama makubwa na anayaogopa si aachie ngazi na sio kuleta longolongo za kujaza headlines magazetin.
   
Loading...