Profesa Muhongo amekengeuka!

Profesa Muhongo amekengeuka!

Longo longo pro muhongo siyo asili yake. kumshauri aende kivukoni kusoma siasa ni kumwambia aende kusoma longo longo. Mzee huyu haangalii sura wala chama. Ulivyokuja ndivyo atakavyokujibu. Kutaka kuonyesha matokeo ya mh Sendeka nayo ni sawa maana alitaka kuonyosha uelewa wa mtu huyo. tuwe wakweli hivi hatuoni mabadiliko ktk sekta ya umeme tangu pro muhongo awe waziri? kwa nn tusione kwamba huyu pro ameziba liziki za watu ndiyo maana anasakamwa? Hatukumbuki dili la mafuta mazito? Nani asiyeelewa Dr mengi anavyopenda kuabudiwa lkn pro hamuabudu na ndiyo chanzo cha wawili hawa kutoelewana? Mnataka serikali iwekwe mfukoni na watu wa aina ya Dr mengi? Watz bw angekuwa mpole mngemsodoa!! Anaonyesha makucha mnalalamika! kwani amezuia asichunguzwe km kuna tuhuma za kweli dhidi yake? Bila aibu unashauri wizara iongozwe na vihiyo mikataba ya kimataifa wataipambanuaje. Unasemaje matokeo ya mtu ni siri wakati hubandikwa ktk mbao za matangazo na sasa unayaona kiganjani? Huyu ni mzee wa makavu kavu. SHIKAMOO PRO MUHONGO.

Mkuu, tafakari kabla ya kuandika. Matokeo ya Ole Sendeka yatasaidiaje kutatua ufisadi na mgawo wa umeme unaoikumba nchi hii? Hivi unakumbuka kwamba Profesa huyu huyu naliwahi kusema umeme hautapanda bei lakini mwezi huo huo umeme ukapanda bei? Wewe unaishi nchi gani? Unajua jinsi bei ya juu ya umeme inavyotuumiza? Inaonekana wew huishi Tanzania--ungekuwa hapa nchini ungegundua madudu yaliyopo kwenye Wizara hii ya Umeme.

Hlafu naomba nikukumbushe kwamba Prof alimshambulia Ole Sendseka--hajamuongelea Dr Mengi hata kidogo. kama hujui jambo ni bora ukauliza watu waliopo Tanzania. Sio unajichimbia huko nchi za watu halafu hujui shida tunayopata kwa kukosa umeme wa uhakika ktk nchi hii. Na fedha za umeme zimeliwa na mafisadi, watu tunalalamika wewe unaleta masikhara. You can't be serious!

cc:[MENTION]msalani[/MENTION] lusungo Simiyu Yetu mwa 4 T2015CCM FaizaFoxy Mchambuzi Ritz [MENTION]lizabon[/MENTION] siafu dume

umeme haupandi ng'o.jpg
 
Last edited by a moderator:
Kuna thread ndani humu ilimchambua Prof na nakumbuka aliyeandika alidai ya kuwa Prof anaugua ugonjwa wa grandios,nahisi unahusu majisifu.
Tatizo kubwa ni kuwa ameamini anamshambulia Sendeka lakini asijue (pamoja na usomi wake) ya kuwa anamshambulia mpaka spika na hata baadhi ya mawaziri.
Mambo haya ya kufanya vitu bila kutafakari repurcussion yake inaelekea yanajengeka kwani hata Mwigulu nae ameingia katika mkumbo huyo akitamani kuwa Rais ili awakomeshe (Rais aliyemteua kashindwa????).
Muhongo amezoea kufundisha wanafunzi wa chuo kikuu na anaona wote ni wanafunzi lakini akumbuke bunge hilo hilo lilimtoa EL (strong person) na naamini yeye hana killo kama za EL katika siasa.

Hiyo ni moja kati ya paranoid symptoms kwa wale wenye paranoid personality disorder, inaitwa Grandiose Identity, na kwakuwa ana poor insight hawezi jua kuwa anahitaji medication
 
Ni kweli mkuu tpaul..huyu muhongo anaweza kuwa na nia nzuri sana.. ila anavyoelezea nia yake na uchapakazi wake anaeleza kwa majivuno na dharau mno, sijajua hapo wizarani itakuwaje..najaribu kuangalia tatizo ni nini kila hoja inayomchallange anakimbilia kwenye kutaja shule na jinsi uprofessor wake unavyokubalika na anatoka nje ya hoja labisa..sioni kama ina tija kwa taifa..na kuna kitu kina nishangaza sana kwa sisi watanzania kilakitu kina elimu nyuma yake..hata kutengeneza keki, unaweza usijue niweke sukari kiasi gani kama hujasomea, unaweza kuwa dr unafanya craniotomy au jiolojia ukiona jiwe tu unajua madini yaliyopo chini.. Lakini ukashidwa kabisa kutengeneza keki au ukashidwa lets say kuziba pancha.. Ile tabia ya kudhani kila mtu aliyekuzunguka hajui lolote ni tabia ya macowards na watu wanaoogopa challange..naona hata mwigulu na kuna watu ka akina zito, tibaijuka wana hivyo vijitabia..
 
Mhongo angekuwa na pesa tungekoma,anavyodharau wajasiliamali kama mengi na hali uchumi wake haufikii hata 1/8 ya uchumi wa Mengi. Prof. Mhongo hovyo kabisa.
 
Hiyo ni moja kati ya paranoid symptoms kwa wale wenye paranoid personality disorder, inaitwa Grandiose Identity, na kwakuwa ana poor insight hawezi jua kuwa anahitaji medication

Professor Muhongo anaumwa ugonjwa unaitwa grandiosity.

Grandiosity-refers to an unrealistic sense of superiority - a sustained view of oneself as better than others that causes the narcissist to view others with disdain or as inferior - as well as to a sense of uniqueness: the belief that few others have anything in common with oneself and that one can only be understood by a few or very special people.

Muhongo!!!!!!!!!!!!! Msomi wa hovyo kuwahi kutokea hapa nchini. Bado tunayo safari ndefu sana, kama anaamua kusema UONGO kwamba kesi ya IPTL na Tanesco imekwisha wakati mwezi huu (tano) wametangaza mawakili wao wapya watakao wawakilisha huko mahakama ya ISCID baada ya kumpiga chini mkono,

Mawakili hawa wamepewa tenda hiyo kwa dau lenye thamani ya 56 bilioni na jumatatu wanaweza kulipwa malipo ya awali ya kazi hiyo.

Cc:[MENTION]lizaboni[/MENTION]
 
kama utakuwa umehudhuria shule nadhani umesoma kwa miaka saba tu. Soma vzr post yangu nimesema kwani prof amezuia asichunguzwe?
unaweza kuwa umesoma kwa miaka 20 na usielimike, muda wa kukaa darasami siyo determinant ya kuelimika, ndiyo maana tunao maprofesa weziiiiiiiii tangu hasubuhi hadi juioni, jan-dec, .....
 
Muhongo kawashika pabaya!

Tumeshikwa pabaya au yeye ndiyo ameshikwa pabaya?Hivi kwanini kama kitu chauwongo uanze kumkashfu mtu anayetaka kujua ukweli?Ukweli na matusi wapi na wapi.Ila sababu anaujua uKWELI na anauogopa UKWELI ndiyo maana ameanza kujisifu amesoma anaakili na wenzie hawana akili.Kuwa na kiongozi kama huyu ni sawa na hakuna.Huyu shule yake yote hajaelimika ila amefuta uJINGA tu.
 
Maendeleo hayaletwi na mtu mmoja huletwa kwa mipango iliyoandaliwa na serikali. Hakuna siku maendeleo yalisimama yamaendeleo yalikuwepo yapo na yataendelea kuwepo hata bila ya Muhongo. Hoja hapa ni dharau, majisifu na kujikweza. Daima watu wenye maendeleo huwa hawajisifu, matendo yao ndiyo yanayoonesha Wizara madini na nishati inawataalam wengi wanayoifanya itende kazi sio Muhongo peke yake. Kuchukuwa sifa za wizara mtu mmoja ni uwizi wa michango ya watu wengine na ubinafsi unaopindukia.
Hata kama ungefanya vizuri namna gani, haikupi haki ya kujikweza na kuwatweza wengine. Kufanya vizuri darasani hakutegemei akili peke yake, kunategemea pia mazingira inawezekana kabisa wale wasio na vyeti kama yeye wana IQ kubwa kuliko yeye. Mao wa china alipata alama ndogo katima mitihani yake ya kidato cha nne lakini alikuja kuonekana ana akili kubwa katika masomo yake ya juu na akaandika vitabu vingi na kubadilisha maisha ya wachina Darwin alionekana kuwa na akili kidogo darasani lakini katika utafiti wake aliandika nadharia ya survival for the Fittest ambayo hakuna mwanasayansi aliyeipinga mpaka sasa. Muhongo katika jamii ya watanzania ana nini cha kumkumbuka hata akifa leo. Yawezekana Sendeka ana manufaa zaidi kwa jamii ya watanzania kuliko alivyo Muhongo. Economic value ya Muhongo iko chini kuliko John John Mnyika ingawaje yeye Muhongo anamfananisha Muhongo na Zero.
Sio lazima unapotaka kumweleza mtu jambo lolote lenye manufaa umtweza, unaweza kufikisha ujumbe wako pasipo kujisifu wala kumtukana mtu. It is not only what you say, but how do you say it, it is not only how you say it, but where do you say, not only where do you say it, but to whom are you saying. Bungeni sio mahali pa kutukania matusi ni mahali pa hoja. Kutokujua hivyo ni ujinga hata kama una degree 100. Kumshambulia mtu binafsi badala ya kujibu hoja ni ujinga. Ujinga maana yake ni kutokujua unachopaswa kukijua. Mbunge ambaye kwa utambulisho wa kibunge anaitwa Mheshimiwa Muhongo kumfanananisha na zero ni kukosa kujua kuwa unawatukana wananchi wote anaowawakilisha. Usipolijua hili kwa hakika u mjinga hata kama unavyeti lukuki. Vyeti vya msomi vinapaswa kuaishiri kilichomo kichwani mwa mwenye vyeti. Hakika kama vyeti havisaditifu akili uliyo nayo ni sawasawa na Bure bora hata ya Sendeka.
Longo longo pro muhongo siyo asili yake. kumshauri aende kivukoni kusoma siasa ni kumwambia aende kusoma longo longo. Mzee huyu haangalii sura wala chama. Ulivyokuja ndivyo atakavyokujibu. Kutaka kuonyesha matokeo ya mh Sendeka nayo ni sawa maana alitaka kuonyosha uelewa wa mtu huyo. tuwe wakweli hivi hatuoni mabadiliko ktk sekta ya umeme tangu pro muhongo awe waziri? kwa nn tusione kwamba huyu pro ameziba liziki za watu ndiyo maana anasakamwa? Hatukumbuki dili la mafuta mazito? Nani asiyeelewa Dr mengi anavyopenda kuabudiwa lkn pro hamuabudu na ndiyo chanzo cha wawili hawa kutoelewana? Mnataka serikali iwekwe mfukoni na watu wa aina ya Dr mengi? Watz bw angekuwa mpole mngemsodoa!! Anaonyesha makucha mnalalamika! kwani amezuia asichunguzwe km kuna tuhuma za kweli dhidi yake? Bila aibu unashauri wizara iongozwe na vihiyo mikataba ya kimataifa wataipambanuaje. Unasemaje matokeo ya mtu ni siri wakati hubandikwa ktk mbao za matangazo na sasa unayaona kiganjani? Huyu ni mzee wa makavu kavu. SHIKAMOO PRO MUHONGO.
 
Mshamba kama wewe hutaweza kuacha kushabikia kisa ni Prof na anatokea Musoma , tembea uone ma Prof wenzake Duniani ni wa aina gani kaka .

Aanze na Profesa Kapuya kisha amwone pia Profesa Majimarefu wa kule Koogwe.
 
Akina Mkwawa, Lumanyika, Isike, Kinjeketile, nk, hawakuwahi kuliona darasa lakini wana maana kubwa sana ktk historia ya nchi yetu kuliko hili 22cer linalojidai kwamba limesoma huku likishindwa kutuondolea mgawo wa umeme na kusambaza umeme vijijini. majitu kama haya ndiyo yanayorudisha nyuma maendeleo ya nchi.

hivi kumsahihisha/kumuelimisha mtu mpaka UMTUKANE? na huko chuoni alipokuwa akifundisha alikuwa anawatukana wanafunzi wake kama hivi? na inasikitisha sana kwamba kuna baadhi ya watu wanaunga mkono matusi haya. hv tunakwenda wapi jamani? nchi yetu haitaendelea kamwe tukiwa na mawaziri mazuzu kama hili limuhongo--hakika tutasubiri sana. ni bora hata wizara hii ingeongozwa na John Komba au Profesa Majimarefu kuliko kuongozwa na hili tukanaji.
 
Back
Top Bottom